DOMTOWN STAND UP ALBUM Vol. 1 IMEACHIWA, FANYA KUISIKILIZA AU KUIDOWNLOAD BUREE HAPA
Ile Album ambayo ilikuwa ikisubiriwa kwa hamu na wadau wa #MuzikiMuzuri imeachiwa tarehe 22 April kwa mtandao ikijumuisha nyimbo 33 kutoka kwa wasanii wa Dodoma na special songs appearance ya nyimbo za Mangwea na Mez B ikiwa ni katika kuwaenzi na kuheshimu kile ambacho wamefanya katika muziki wa Dodoma na Tanzania kwa ujumla. Chamber squad, Makole Hexagon, DLF, Machizi Reality na wengineo walionyesha kwamba inawezekana kutoka nje ya mipaka ya mkoa, nchi na hata bara kwa kutumia kipaji na wao wamekuwa mfano hadi leo tunaweza kuwasikia Watawala na Ukoo, Central Zone, DDC, Host Zee Ving'ang'a, Slimsal, One Six na wengineo wengi wakifanya vile ambavyo waliowatangulia wamekuwa wakifanya.
Haya ni mafanikio kimuziki ambao ukichukuliwa serious unaweza kuwa njia ya kujipatia kipato kwa wasanii ambao watajitambua na kutambua ni nini wanapaswa kufanya pindi wanapopata majina, ndiyo maana kwa kutambua uwepo wao ndiyo maaana hata idea ya kuja na online Album ambayo itakuwa inatoka mara mbili kwa mwaka ikijumuisha nyimbo za wasanii toka Dodoma ambao baadaye tukiungana tunaweza fanya show ama hata tour za kutangaza muziki wao ndani na nje ya mkoa wa Dodoma.
Domtown stand up vol. 1 ndo hii imetoka na unaweza kuisikiliza ama kuidownload BUREE ukazipata nyimbo 33 za wasanii wa Dodoma kwa pamoja. Marehemu Mez B hatuponaye tena xoxo Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi na kwa kuangalia hilo sitegemei kuona One Six ama Friday wanalala baada ya kukaza buti na kuonyesha ni vipi tunaweza kuziba pengo la Muziki Muzuri ambao tulikuwa tukipata kutoka kwake.. the same to Albert Mangwea ambaye nae hatupo naye. Take your time then sikiliza online Album hii ya Domtown stand Up ikiwa ni volume 1 na pia kama wewe ni blogger ama una website na unapenda kuitangaza Album hii, waweza fanya hivyo kwa kuchukua link yake HAPA. Muziki Muzuri ndo kile kitu kila mtu apenda kusikiliza kwa masikio yake xoxo take your time and listen to the Album below na pia waweza ku'share na marafiki kwa social networks.
Leave a Comment