#DOMTOWNSTANDUPALBUM KUACHIWA TAREHE 22 APRIL 2015
Ikiwa imebaki wiki moja kabla ya ukusanyaji wa nyimbo za
wasanii kutoka Dodoma ambao kwa pamoja wataunda album ambayo itakuwa ikipatikanika
mtandaoni mara mbili kwa mwaka ikijumisha ngoma ambazo zimeachiwa mwaka husika
na zile ambazo hazijawahi kusikika kabisa masikioni mwa mashabiki wa #MuzikiMuzuriAfrika na duniani kote.
Kama wewe ni msanii na ungependa nyimbo yako / zako ziwepo
ndani ya hii album hujachelewa sana kwani mwisho wa kupokea nyimbo hizo ni
tarehe 18 Aprili 2015 saa 5:59 usiku. Hivyo basi unaweza kutuma nyimbo zako kwa
email address: imcascos@gmail.com kwa
BlackMutu ama jmsofe@gmail.com kwa James
Msofe wa www.capitaltz.com ambao kwa
pamoja na wadau wengine wataachiwa album hii siku husika.
Tarehe 20 mwezi huu tutaachia majina ya wasanii na nyimbo
zao ambazo zitapatikana katika album project ya #DomTownstandUp ikiwa ni Vol. 1
katika muhula wa kwanza wa mwaka 2015. Baadhi ya wasanii ambao nyimbo zao
tayari zimeshatufikia ni pamoja na Wise One, Prince Tozzie, Central zone, Crown
Jay, Jahlex, Andre K, J Man na wengineo ambao kwa pamoja list ya nyimbo zao
itatoka tarehe 20 na piaaaaa kwa album hiyo kutakuwa na special surprise kutoka
kwa Toz B ambaye ni mdau mkubwa sana wa muziki wa Dom mahali ambapo amekulia
kabla ya kwenda South Africa mahali ambapo anaishi kwa sasa. Fanya kusubiri io surprise kutoka Durban, South Africa hadi Dodoma, Tanzania.
Leave a Comment