GOOD NEWS: GHANA YAZINDUA GARI YAKE
Wakati unapoangazia swala la utengezaji magari mataifa ya
Afrika kwa kawaida hayaorodheshwi katika swala hilo.
Lakini hilo sasa huenda likabadilika kufuatia kuwasili kwa
kampuni ya magari ya Ghana Kantanka ambayo hivi karibuni yataanza kuingia
katika soko.
Miongoni mwa magari ya kampuni hiyo ni lile la lita mbili
aina ya 4 by 4 ambalo linatarajiwa kuuzwa kwa takriban pauni 14,000.
Lakini je,kampuni hiyo itaweza kukabiliana na ushindani
mkubwa kutoka kwa magari kama vile Toyota,Land Rover na BMW?.
Kwadwo sarfo ni mwana wa mmiliki wa magari hayo.
Babaake ni m'bunifu ambaye pia ni kiongozi wa dini.Hupata
fedha kutokana na kilimo na uchimbaji.
Magari ya Kantanka yanafananishwa na magari makubwa kama
vile Toyota Prado ama MItsubishi Pajero.
Mbele ya gari hilo kuna michoro ya kucha za chui pamoja na
nembo ya kampuni hiyo ya nyota ya Afrika.
Kulingana na raia mmoja wa Ghana uvumbuzi kama huo
haujafanyika nchini humo.
Tunapenda kununua bidhaa kutoka nje kwa hivyo italazimu
kufanyika kwa mauzo ya ziada kwa gari hizi za kantanka kukubalika.
Profesa Robert Ebo Hinson ambaye ni mkuu wa kitengo cha
mauzo katika chuo kikuu cha Ghana:Nadhani kile kilichotokea hapo awali ni
kwamba tumefanywa tuamini kwamba kile kinachotengezwa katika mataifa ya
magharibi ni
bora zaidi kwa sababu zote zile.
Wakati mwengine bidhaa zinazotengezwa kutoka Ghana haziwezi
kudumu.
Serikali ya Ghana inaelewa kikwazo hicho na tayari
imeanzisha kampeni kubwa ya kuwafanya wakaazi kununua bidhaa zinazotengezwa
nchini humo.
Waziri wa biashara daktari Ekow Spio Gabrah anaongoza
kampeni hiyo na anasema:Nitaendesha moja ya magari haya,kwa kweli niliketia
gari moja wakati lilipokuwa likitengezwa na nafurahi kuwa na moja kama gari
langu rasmi.
Waziri na rais wana uwezo wa kuendesha magari hayo kwa
gharama ya walipa ushuru.
Lakini je,raia wataweza kutumia fedha zao wenyewe kulipia
gharama za kulinunua gari hilo?
Inaonekana kwamba raia wengi kama alivyodai hapo awali
Professa wana wasiwasi kuhusu usalama wa gari hilo na kudumu kwake.
Je, unadhani wasiwasi huo huenda ukaathiri uzalishaji wa
magari hayo? Kulingana na Kwadwo Sarfo gari hilo la kwanza kutengezwa nchini
Ghana litapata umaarufu.
BBC Swahili
Leave a Comment