HIZI NI SABABU SITA (6) ZA KWANINI UENDELEE KUJIVUNIA SANAA YA TANZANIA

#repost from @kuzatz - Tanzania imepiga hatua kubwa kwenye kiwanda cha burudani barani Afrika. Hebu soma baadhi tu ya mafanikio haya katika nusu ya kwanza ya mwaka 2015 na uone jinsi tulivyo kwenye nafasi nzuri:

1.@diamondplatnumz anawania vipengele vitatu kwenye tuzo za #MTVMAMA2015, atatumbuiza July 18 kwenye kilele chake jijini Durban, SA, ana wimbo mkubwa Afrika#Nana #Sankoro aliomshirikisha Flavour ambayo tangu itoke May 29, ina views zaidi ya milioni 2. Ameshirikishwa kwenye collabo kubwa na wasanii wa Afrika ukiwemo wimbo wa Iyanya ‘Nakupenda’, Love Boat wa KCEE na mwingine wa Donald.

2. @vanessamdee anawania tuzo ya msanii bora wa kike kwenye #MTVMAMA2015, ana video kubwa Afrika ya wimbo wake #NobodyButMe aliyomshirikisha rapper wa Afrika Kusini, K.O. Mwezi ujao ataonekana kwenye jarida kubwa la Marekani la Essence.3.@officialalikiba ana video kubwa ya wimbo wake #ChekechaCheketua ambayo ndani ya saa 24 ilikuwa na views zaidi ya laki moja, ni balozi wa kampeni ya kimataifa ya kuzuia ujangili kupitia shirika la #WildAid na jana alikutana na balozi mwenzie, @lupitanyongo. .4.@ladivamillen alishinda tuzo ya kwanza na kipekee ya #GlobalGood kwenye#BETAwards mwaka huu. Naye pia mwezi ujao ataonekana kama model kwenye jarida la Essence la Marekani (global issue). .

5. Wimbo wa @joh_makini #NusuNusu umekamata nafasi ya kwanza kwenye chart ya video 10 za Afrika kwenye kituo cha MTV Base. .

6. @fidq ametajwa kwenye jarida la ‘SA Hip Hop’ miongoni mwa rappers 20 bora barani Afrika.
Kwanini usiendelee kujivunia sanaa ya Tanzania? #KuzaKiwandachaBurudaniBongo#TanzaniaKwanza

No comments

Powered by Blogger.