CHANZO CHA BIFU LA DIAMOND PLATNUMZ NA DIVA LOVENESS LOVE HIKI HAPA

Msanii wa Kizazi kipya Diamond Platnumz na Mtangazaji wa Clouds Fm, Diva Loveness love wamejikuta wakirushiana maneno hewani kwasababu ya ugomvi wao chinichini ambao unaonekana ni wa muda mrefu.
Vita hiyo ya maneno ya watu hao ambao waliwahi kuimba wimbo wa pamoja ‘Piga simu’ imeanza baada ya Mtangazaji wa kipindi cha XXL, Bdozen kuwauliza kama washamaliza tofauti zao (hazijulikani) ndio Diamond akadakia na kumuuliza mtangazaji huyo kwanini huwa anamsema vibaya baada ya hapo ndio wakaanza kurushiana maneno makali....

Diamond alisikika akisema anawaza kwanini "hakumkaza" labda ndio heshima ingekuwepo lakini Diva alijibu hilo haliwezekani kwasababu Diamond sio Type yake. Mtangazaji wa kipindi cha XXL Bdozen alilazimika kuzima Mic kwasababu hakukuwa na dalili za watu hao kupatana licha ya kujaribu kuwapatanisha.
Baada ya Muda kidogo, Diva aliamia kwenye mtandao wa Twitter, akialalamika kuwa Diamond alimtishia kumpiga, @diamondplatnumz Umeni disrespect On air as a Media Personality. And Umetishia Kunipiga studio ryt? au sababu mwanamke?!—Diva (@DivathebawseDiamond hajamjibu hadi sasa lakini manager wa Diamond, Salaam amemjibu Diva kuwa Twitter si mahala sahihi ya kupeleka malalamiko yake.

No comments

Powered by Blogger.