IMENIBIDI MIMI NDIYO NIONE AIBU BAADA YA KUISOMA HABARI HII..! KAMA NI WEWE UNGEFANYAJE??

Kwa muda mrefu sasa, nimekua nikisumbuliwa na mambo ya mapenzi hasa kazini, nikaamua nifuate ushauri wenu niachane na mapenzi ya sehemu za kazi, nikafanya hivyo. Hapo katikati nikakutana na Dada mmoja wa makamo na mwenye watoto wawili wa 9 na 12 yrs yeye ana 36 yrs mimi nina 32 yrs tukawa tuna date, kwa kweli anajiweka vizuri sana huwezi jua kama ana watoto au ana 36 yrs. Akaniomba niamie kwake tuishi wote maana amepanga nyumba nzima na wanawe wote wapo boarding, nikaona poa tu sio mbaya, nilikua nakaa na mdogo wangu wa kike ambae yupo tu home alipata matatizo kazini, nikamuomba akaishi kwa kaka yetu mkubwa ili niepukane na kodi kwa kuhamia kwa mwanamke wangu.

Tangu nimehamia kwa mwanamke wangu ni miezi miwili, sasa juzi nashangaa...

 ...ananiambia eti kodi imeisha tunatakiwa kulipia nyingine hivyo tuchangie nusu kwa nusu, wakati mwanzo akiniomba tukae wote alisema yeye ana uwezo wa kulipa kodi mwenyewe kama siku zote, sasa nashangaa kanigeuka hiyo ni haki kweli?Mimi nilikokua nimepanga mwanzo nilikua nalipa kodi ya 60,000/= per month, hapa tulipo sasa ni 400,000/= sasa anataka nichangie 200,000/= na land lord anataka kwa mwaka mi ntaweza wapi hiyo kodi?
Si bora nirudi kule kwa mwanzo. Yeye alidai anataka kuishi na mwanaume amechoka upweke hivyo nimsitiri atagharamia kila kitu nashangaa sasa anakuja na lugha mpya.Kwanza mimi sikua nampenda nilimsaidia tu, sipendi kuchukua mwanamke mwenye watoto, hapa nilipanga nijibanze kwake hadi hapo baadae, sasa najikuta naingia kwenge budget nisiyotarajia. Nyumba yenyewe ndugu kila siku wanapishana humu, chakula kikipikwa utadhani kuna msiba, mi nilishazoea gharama ndogo kabisa, kwanza huwa nakula town nikirudi ni kulala tu.

Nashangaa yeye ananifosi nichangie gharama za uendeshaji nyumba kinyume na makubaliano, kwa hali hii nyumba yangu itaisha kweli? Sikutaka kuoa ili nikamilishe hiyo nyumba, bora nisepe tu. 

Wadau mna mawazo gani juu ya hill?

No comments

Powered by Blogger.