MAHUSIANO: NILIMTELEKEZA SUPERMARKET NA BILI YA LAKI NNE

Kuna huyu binti ambae ni secretary Wa kampuni flani hivi ipo ppf tower building, ambapo mimi huenda kikazi kwa kuagizwa na viongozi wangu, kutokana na kwenda pale Mara kwa Mara nikajikuta nimempenda yule binti na kumuomba awe wangu. Kinyume na matarajio yangu alinikubali haraka, kwa jinsi alivyo mzuri na sister duu wa nguvu nilidhani ningepambana kumbe sivyo.
Date yetu ya kwanza ilinishtua sana baada ya yeye kudai twende Sea Cliff Hotel, nilijikaza tukaenda, nilikua na 120,000 nilirudi kwangu na 1,500 usiku huo...

Date zilizofuata ni hivyo hivyo, mimi nampeleka Hongera bar, anakaa kimya through out the date anadai hapapendi hapo, namuomba achague, tunahama, anadai twende Collosium Hotel Osterbay, naenda ATM nakomba kila kitu then tunaenda hapo anapotaka, tukitoka hapo nakua na chini ya 2000 kurudi kwangu. Kwa gharama nilizotumia nikaona kukata tamaa pesa zangu zitakua zimeenda bure, nikajipa moyo niendeleee, ingawa kiukweli hadi hapo hali yangu kiuchumi ilikua imezorota sana, haikua na tofauti na mgonjwa alieko intensive care unit akipumua kwa mirija.

Yote tisa, kumi, wiki iliyopita niliahidiwa tunda na huyo binti, akaniambia tafuta a conducive and suitable place ili tuweze kumenya tunda, miadi ilikua ni last Saturday. Nilipanga kumpeleka rombo green view ambapo Chumba ni 25,000 cha kawaida, huwa sipendi kupeleka demu ghetto kwangu Mara ya kwanza kutokana na sababu za kiintelijensia na kiusalama, pia landlady ambae ni mbibi ni msumbufu sana akiona mgeni mwanamke. Saturday asubuhi alisema nimsubiri Maryland bar pale mwenge tuondokee hapo maana anakaa Mwenge Bamaga, Basi nikawa hapo nakunywa supu huku Gari nililoazima kwa Mshikaji wa kazini likioshwa. Nikiwa na shughuli kama hiyo huwa Mshikaji ananipa Gari mafuta naweka mwenyewe huwa inarahisisha mizunguko ya kwenda guest kuliko public means.

Kisa chenyewe

Demu alipofika akaniambia nimpeleke kwanza nakumat supermarket pale mlimani city nimnunulie mahitaji machache, vitu vidogo tu ndipo twende hotel nikasema poa. Nilikua na 150k mfukoni niliyokua nimepata kimagumashi Jana yake kazini, hivyo nikajua akitumia hela nyingi supermarket Basi ni 30-40k,
Surprisingly tulipoingia tu mule nakumat akachukua lile trolley kubwa lenye matairi la kusukuma, nikajiuliza hili lote anaenda kufanyia nini!

Kabla hajaanza kuchukua vitu nikaona nimpe 40k akae nayo kabisa atalipia mwenyewe, wakati naingiza mkono mfukoni akanizuia akasema "kwani una haraka gani? Subiri utalipia kwa cashier:' Nilipata mshtuko mkubwa kuona anachukua kopo kubwa la maziwa ya nido la 54,000 akachukua Cornflakes kubwa, sabuni za unga kubwa, spray za chooni, lotions, akachukua na pasi ya kunyoosha nguo, nilikua natiririka jasho pamoja na AC Kali iliyomo mule ndani maana hadi hapo kwa uchache ilikaribia laki nne kwenda tano ya vitu alivyokwisha chukua. Nilijua tukifika kwa cashier nitafedheheka, nitapata aibu ya milele, hivyo tulipofika kwenye foleni ya cashier palikua na foleni ndefu kiasi nikamwambia nimesahau na mimi nilihitaji kuchukua kitu, akasema poa,

Nikajifanya naenda kwenye mashelf ya bidhaa, nikamwangali hakua akitazama, nikapiga u turn kali kulikua na kundi la Wahindi wakitoka nje bila kununua kitu.
Nikajichanganya nao na kutoka nje ya jengo, nikatembea haraka kama vile nakimbizwa hivi, nikaingia kwa Gari nakuondoka kwa kasi eneo hilo, nikazima simu kabisa.

Wadau hivi lengo lake lilikua nini hasa kunifanyia kitu kama kile?

Mshahara ndo kwanza umeingia Leo 28th, siku hiyo nilikua nimepiga hela Jana yake kazini 150k ndio hiyo pekee nilikua nayo. Basi nimesalim amri, nikikumbuka hela zangu za dates zinaniuma sana. Jumatatu nimefungua simu nimekuta msg zake za whatsaap ni matusi mazito, kwamba mimi ni mshenzi wa washenzi, kwamba I will pay for what i did to her, kwamba mimi firauni.

Sasa mimi kosa langu ni nini hapo?

No comments

Powered by Blogger.