MKE WANGU HAPENDI KUONGOZANA NA MIMI, NIFANYAJE!!?

Wife amekuwa hapendi kuongozana nami katika safari mbali mbali misiba, sherehe, outing na kadhalika, sio kwamba anakataa moja kwa moja bali atatafuta sababu ili twende tofauti, na akikubali kwenda anakuwa uncomfortable na uwepo wangu.
Mwezi uliopita wa 12 tulisafiri wote kwenda up country nyumbani kwao mkoani kwa mapumziko ya end year, tulianzia mkoani kwetu, mwisho tukamalizia kwao, sasa tukiwa kwao, mdogo wake wa kike ndie alikuwa akizunguka nami mjini kutalii na kunionesha sehemu mbali mbali, wife alikuwa akinipiga chenga ndipo shemeji akaamua kunipa kampani...
Tuliijadili sana hii tabia ya dada yake ambayo hata yeye akasema ameiona kwa muda mrefu sana, anashindwa kuelewa tatizo ni nini? Sababu sina ulemavu, mwonekano wangu ni wa kawaida, wakiitwa ma handsome siwezi kutoka, lakini pia wakiitwa wabaya pia siwezi kutoka, ni wa kawaida. 
Siku ya kuondoka Arusha, tukawa na ugomvi mkubwa sana kwamba nakosaje aibu kiasi kile, kuzunguka na mdogo wake hadi watu kunielewa vibaya, kiasi kuwa akakataa kabisa kwa hasira shemeji asije na sisi Dar maana huwa tunaishi nae, hadi wazazi wao walipomuamuru akakubali.
Tabia hii imenichosha sana kufikia hatua najiona sina thamani, tukienda harusini au outing ya pamoja na marafiki pamoja na waume zao utashangaa kila nikitaka kuchangia mada ananiminya mkono nisizungumze labda nitaongea jambo la kumuaibisha wakati mimi kwanza sio muongeaji, waume wa marafiki zake wataongea wee mimi nipo kimya, mimi nikichangia tu ni ugomvi, ananikosoa mbele yao kila nalochangia tena kwa kunishushua, hivyo nakaa kimya muda wote hadi wengine waulize mbona huongei.
Nilishajiuliza huenda huwa naongea pumba, hata hivyo hapana, mimi huwa ni mtu mwenye kuchagua maneno sana kabla ya kuongea.


Sasa naomba mnisaidie mawazo, tatizo ni nini hasa? Ni suala la muda mrefu hivyo nimeshachoka, nataka kufanya mabadiliko, nahitaji mke mwenye kunithamini na ambae yupo proud of me nahisi huyu hanipendi Ingawa tuna watoto wawili.

No comments

Powered by Blogger.