BESIGYE AKUTANA NA UJUMBE WA UMOJA WA MATAIFA KWA MASHARTI

Kiongozi wa upinzani nchini Uganda, Kizza Besigye, akiamkiana na Balozi wa Uingereza, Alison Blackburne, huku wanadiplomasia wengine kutoka Uholanzi na Ireland wakiangalia wakati walipomtembelea kwenye makaazi yake, mtaa wa Kasangati, kando kidogo ya mji mkuu, Kampala, jioni ya jana.
Awali iliripotiwa kuwa polisi walikuwa wameukatalia ujumbe wa Umoja wa Ulaya kumuona kiongozi huyo, lakini baadaye ruhusa ilitoka kwa masharti kwamba wasizungumze na vyombo vya habari baada ya mkutano wao. Walimtembelea kuzungumza naye juu ya mustakabali wa Uganda baada ya uchaguzi wa Februari 18 uliompa ushindi Rais Yoweri Museveni na ambao unalalamikiwa na Besigye.






Chanzo: DW (Kiswahili)


No comments

Powered by Blogger.