KING NA QUEEN WA RNB NCHINI TANZANIA HAWA HAPA || BLACKMUTU BLOG
Inawezekana kabisa kuwa wewe umeanza kusikiliza au kuupenda muziki kipindi Diamond Platnumz anatoka yaani miaka ya 2000's, kama ulikuwa unahisi King wa RnB ni Belle 9 au Ben Pol kama ambavyo anapenda watu wafahamu baaasi fahamu upo chaka.
Inawezekana kabisa ukabisha kutokana na kwamba nyimbo zao hazipigwi kwenye baadhi ya radio station Tanzania kama...
...Clouds Fm na nyinginezo lakini katikati ya ukweli uongo huwa unajitenga pembeni. Muziki wa Bongo una historia ndefu kutokea kipindi cha Kwanza Unit (K.U), Diplomat (DPT) na wengineo kama kina II Proud a.k.a Mr II a.k.a Sugu ambaye kwa sasa ni mbunge wa Mbeya mjini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Ukimsikiliza Rama Dee na Lady Jaydee utafahamu nini nachomaanisha kwani wapo wengi wanaimba lakini wanakosa ubunifu mzuri wa nyimbo zao na pia wengi wao sio waandishi wazuri ndiyo maana kila nyimbo wakitoa ni kuhusu mapenzi tuu mbaya zaidi kuna maneno lazima utasikia yakijirudia rudia kila nyimbo. Unaweza kumuweka Nuruelly, Q Chief na T.I.D kwenye list hii tatizo ni je! wameweza ku maintain status zao za muziki kwamba hata leo wakitoa ngoma itakuwa kali kama zamani? Jibu ni HAPANA
Kwa upande wa Lady Jaydee bado sijaona ni nani wa kumlinganisha naye kwani mtu pekee ambaye angeweza kufananishwa naye ni Ray C ambaye kwa sasa hafanyi muziki. Lady Jaydee ndiyo Queen wa RnB nchini Tanzania huku Rama Dee akiwa ni King wa RnB. Na kama unabisha fanya kusikiliza hizi nyimbo mbili, moja wa Lady Jaydee na nyingine ya Rama Dee ambazo ni mpya halafu utajau nini nachoongelea hapa..!!
DOWNLOAD "NDI NDI NDI" - LADY JAYDEE
DOWNLOAD "NDI NDI NDI" - LADY JAYDEE
Leave a Comment