MAMA MZAZI WA TUPAC SHAKUR AFARIKI DUNIA

Afeni Shakur Davis, mama mzazi wa the late Tupac Shakur amefariki dunia akiwa na miaka 69, kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa Sausalto,California wamedai kuwa Afeni alifariki dunia usiku wa kuamkia jumanne ya tarehe 3 Mei akiwahishwa hospitali mara baada ya kupata taarifa ya simu ya dharura kutoka nyumbani kwake. Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi inayoeleza chanzo cha kifo chake. Taarifa kamili za chanzo cha kifo chake zitawajia pindi zitufikiapo.
Tupac ambae ni miongoni mwa rappers wanaoheshimika na jamii ya wanamuziki wa HipHop Ulimwenguni alipigwa risasi September 7 1996 jijini Las Vegas,Nevada na kufariki baada ya siku 6 akiwa na umri wa miaka 25.

No comments

Powered by Blogger.