DOM DOWN CLICK - FASIHI SIMULIZI ALBUM | COMING SOON | BLACKMUTU BLOG
Ni mojawapo kati ya ule mwendelezo wa kutoa santuri kutoka kwa wasanii wanaoiwakilisha vyema kabisa Dodoma, Tanzania katika harakati za muziki. Wanafahamika kama Dom Down Click na hivi karibuni baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhan DDC watakuletea album itakayofahamika kwa jina la
"Fasihi Simulizi" ikiwa ni upishi wake Bello bin Laden katika studio za AJ Records zinazopatikana mkoani Dodoma maeneo ya Area D. Kuwa karibu na sisi upate kufahamu ni jinsi gani unaweza kupata hiyo santuri pindi itakapoachiwa rasmi.
Wakati tunaendelea kuisubiri "Fasihi Simulizi" hebu chukua muda wako kuisikiliza hii ya DDC aliyoshirikishwa One Six, inaitwa "Kata Nyau"
Leave a Comment