KITUNGUU SWAUMU HUTIBU MAGONJWA 30
Mungu anaposema watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa hamaanishi maarifa ya kutengeneza au kuendesha ndege, ni maarifa ya kawaida tu katika maisha yetu ya kila siku ambayo yanaweza kubadilisha afya na ustawi wetu. Moja ya mmea ambao umependelewa sana na Mungu kwakuwa na viinilishe vingi na mhimu sana kwa afya ya binadamu ni kitunguu swaumu. Kitunguu swaumu ni dawa karibu kwa kila ugonjwa.
Kitunguu swaumu ni jamii ya vitunguu ambayo kwa kitaalamu huitwa Allium sativum. Jamii hii ilianza kutumika katika mabara mbalimbali duniani hususani Asia, Afrika na Ulaya takribani miaka 6000 iliyopita. Matumizi makuu nyakati hizo yakiwa viungo katika mboga na tiba.
Historia inaonyesha kuwa, vitunguu swaumu vilianza kutumika nchini China mwaka 510 kabla ya Kristo na pia vilitumiwa na wanajeshi wa Ugiriki na Warumi. Aidha wasafiri wa vyombo vya baharini na vijijini pamoja na wakulima barani Afrika walivitumia sana. Kuna baadhi ya imani watu wanaamini kitunguu swaumu kina uwezo wa kufukuza hadi wachawi! hivyo kama unatokewa unapata usingizi wa usioeleweka au unakabwa kabwa na wachawi hebu jaribu kitunguu swaumu na utuletee mrejesho
Mwaka 1858, mtafiti na mwanasayansi wa nyakati hizo, Louis Pasteur aligundua uwezo wa kitunguu swaumu katika kuua vimelea mbalimbali vinavyosababisha magonjwa, na hivyo vikaanza kutumika kama dawa ya kusafishia vidonda na kuzuia kidonda ndugu hasa zama za vita ya kwanza na pili ya dunia. Isitoshe, mpaka sasa zipo dawa kadhaa zilizotengenewa kwa kutumia jamii hii ya vitunguu swaumu ikiwemo dawa ya kusafisha mdomo (mouth wash).
Huko sokoni tayari nimeviona vitunguu swaumu kutoka China na Afrika kusini ambavyo vyenyewe huwa vina punje kubwa nene na huwa rahisi kuvimenya, hata hivyo ili upate faida hizi zote hapa chini naendelea kukushauri utumie vitunguu swaumu vyetu vinavyolimwa hapa Tanzania kwani hivyo vya kutoka nje pamoja na kuwa ni rahisi kuvimenya lakini ubora wake si kama ule wa vitunguu vyetu.
Hakikisha kila mboga unayopika haikosi kitunguu swaumu ndani yake na ikibidi ukiweke mwishoni mwishoni unapokaribia kuipuwa mboga yako toka katika moto kwamba kisiive sana hata kupoteza viinilishe vyake. Kama una friza au friji ya kawaida unaweza kumenya vitunguu swaumu hata kilo nzima na kuvitwanga kidogo katika kinu, vifunge vizuri katika bakuli au mfuko wa plastiki na uvihifadhi katika friza au friji na hivyo kila unapopika unachukuwa tu na kukitumia ili kuepuka usumbufu wa kukimenya kila siku.
Lakini ili upate faida zaidi za kitunguu swaumu utatakiwa ukimeze katika maji au ukichanganye na mtindi kikiwa kibichi, yaani bila kupitishwa katika moto au kuwa kimepikwa.
1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
2. Kigawanyishe katika punje punje
3. Chukua punje 6
4. Menya punje moja baada ya nyingine
5. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
6. Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupenguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.
Katika zoezi hili nimetumia mtindi wa Tanga freshi na nimeona matokeo mazuri sana ikiwemo ngozi kuendelea kung'aa na kitambi ni kama kimeisha kabisa kwa siku 7, hivyo siyo lazima uwe mtindi uliotengeneza nyumbani bali hata huo wa dukani wa Tanga fresh bado ni mzuri pia (bila shaka Tanga fresh watanipa hela ya soda kwa kuwapigia promo)!
Fanya hivi kila siku au kila mara unapopata nafasi na hivyo utakuwa mbali na kuuguwauguwa. Mama mjamzito chini ya miezi 4 ni vema asitumie, kwa ujumla tu mjamzito uwe makini utakapotumia kitunguu swaumu kwa namna hii kama wewe ni mjamzito.
Kitunguu swaumu hutibu magonjwa 30
Haya ni baadhi ya magonjwa yaliyothibitika kutibika na yanatibika au kukingika na kitunguu swaumu:
1. Huondoa sumu mwilini
2. Husafisha tumbo
3. Huyeyusha mafuta mwilini (kolestro)
4. Husafisha njia ya mkojo na kutibu U.T.I
5. Hutibu amoeba, minyoo na Bakteria wengine
6. Huzuia kuhara damu (Dysentery)
7. Huondoa Gesi tumboni
8. Hutibu msokoto wa tumbo
9. Hutibu Typhoid
10. Huondoa mabaka mabaka kwenye ngozi
11. Hutibu mafua na malaria
12. Hutibu kifua kikuu (ukitumia kitunguu swaumu kesho yake unaweza kutokwa na makohozi mengi tu ambayo ni ishara kwamba kweli kinatibu kifua kikuu (TB)
13. Hutibu kipindupindu
14. Hutibu upele
15. Huvunjavunja mawe katika figo
16. Hutibu mba kichwani
17. Huupa nguvu ubongo. Kazi nzuri niliyopenda zaidi katika kitunguu swaumu.
18. Huzuia meno kung'ooka na kutuliza maumivu
19. Huongeza SANA nguvu za kiume pia hutibu uanithi (kushindwa kusimama kabisa uume)
20. Hutibu maumivu ya kichwa
21. Hutibu kizunguzungu
22. Hutibu shinikizo la juu la damu
23. Huzuia saratani/kansa
24. Hutibu maumivu ya jongo/gout
25. Huuongezea nguvu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula
26. Huongeza hamu ya kula
27. Huzuia damu kuganda
28. Husaidia kutibu kisukari
29. Husaidia kutibu tatizo la kukosa usingizi (ni kweli, na ni moja ya kazi nyingine ya kitunguu swaumu iliyonishangaza zaidi) pia kinaondoa msongo wa mawazo/stress na kukufanya uishi miaka mingi
30. Huongeza SANA kinga ya mwili na kwa muda mfupi, kijaribu na ulete majibu
Sifa kuu zinazokifanya kitunguu swaumu kuwa na uwezo na faida zilizoainishwa hapo juu ni kule kuwa kwake na viasili kadhaa (ingredients) ambavyo vinafanya kazi tofauti tofauti. Uwezo wake wa kiutendaji unatokana na mambo yafuatayo;
Vina uwezo wa kusababisha kutanuka kwa mishipa ya damu (vasodilation) kwa kubadilisha polysulfides zilizopo ndani yake kuwa hydrogen sulfides kwenye seli nyekundu za damu.
Husaidia uthibiti wa kiwango cha sukari mwilini kwa kushusha kiwango cha kemikali ya homocystine na kupunguza madhara ya kisukari.
Iwapo vitapondwa pondwa vizuri, vitunguu swaumu hutoa kemikali iitwayo Allicin ambayo ni dawa dhidi ya bateria, na phytoncide ambayo huua fangasi wa aina mbalimbali.
Harufu mbaya ya kitunguuu swaumu hutokana na gesi aina ya hydrogen sulfide ambayo hutolewa baada ya kuvila.
Nini madhara ya vitunguu swaumu?
Ukiacha faida zake, vitunguu swaumu pia vina hasara na madhara mbalimbali kwa mtumiaji. Madhara hayo ni pamoja na;
1. Harufu mbaya mdomoni ambayo hutokana na kemikali ya AMS (allyl methyl sulfide). Harufu mbaya hii, hata hivyo, yaweza kupunguzwa kwa kunywa maziwa, kunywa maji mengi au kutafuna karafuu. Na nimeshuhudia nikinywa kwenye mtindi hii harufu ni kama haipo kabisa na hata ukijamba haikutokei ile harufu mbaya sana kama ukinywa vitunguu swaumu katika maji
2. Kwa baadhi ya watumiaji, vinaweza kuwaletea mzio au mcharuko mwili (allergies au inflammatory reactions)
3. Kichefuchefu, Kutapika na kuharisha. Ikikutokea kuharisha siku mbili tatu furahi kwani ni njia mojawapo ya mwili kujisafisha
4. Huweza kusababisha hatari ya kuvuja damu, kwa sababu huzuia kazi ya seli sahani (platelets) zenye kusaidia kuganda kwa damu kushindwa kufanya kazi yake vizuri, na hususani kwa mama wajawazito, baada ya upasuaji au mara baada ya kujifungua.
5. Huingiliana katika utendaji kazi wake na dawa kadhaa kama vile warfarin, antiplatelets, saquinavir, dawa za shinikizo la damu kwa ujumla hasa calcium channel blockers, na antibiotiki za jamii ya quinolone kama vile ciproflaxacillin.
6. Aidha, vinaelezwa pia kuwa na madhara kwa wanyama jamii ya paka na mbwa.
Kumbuka kitunguu swaumu kinaweza kuwa na faida nyingi zaidi ya hizi lakini bado nakushauri utumie kiasi kidogo (punje 6 tu) kila siku kwa kipindi kirefu wiki 2 au 3 hata mwezi ili uone faida zake zaidi. Ikikutokea tangu umeanza kutumia kitunguu swaumu kichwa kinauma zaidi unaweza kupumzika siku mbili hivi na baadaye unaendelea hivyo hivyo.
It is not my first time to visit thios web site, i aam
ReplyDeletebrowsing this web page dailly and take pleasant data from here all the time.
Thanks for that... keep on coming!
Delete