FREEMAN MBOWE, YUSUPH MANJI NA MCHUNGAJI GWAJIMA WATAJWA NA MAKONDA SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA
Mbunge wa Hai Freeman Aikaely Mbowe, mfanyabiashara mkubwa nchini, Yusuf Manji na Mchungaji Josephat Gwajima wametajwa kwenye orodha ya pili ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya watu mashuhuri wanaohusishwa kwenye biashara ya madawa ya kulevya. Makonda amemtaja pia mbunge wa zamani wa Kinondoni, Iddi
Azan na mfanyabiashara maarufu wa nguo, Hussein Pambakali kwenye orodha hiyo.
Ameielezea orodha hiyo kuwa ni ya wale ambao wanahisishwa na biashara hiyo haramu na wengine wana taarifa muhimu zinazoweza kuwasaidia polisi kuwatia nguvuni vinara wa biashara hiyo. Watu hao watahojiwa na polisi kama ilivyofanyika kwa watu waliotajwa kwenye orodha ya kwanza iliyohusisha pia mastaa wa muziki na filamu. Wengine wanaohitaji ni pamoja na wamiliki wa Slipway na Yatchy Club.
Makonda amesema haya:
“Leo tunaingia awamu ya pili ya kampeni ya kutokomeza baiashara haramu ya madawa ya kulevya, kampeni hii ambayo inahitaji watu wenye hofu ya mungu. Niwaombe tuungane sote kumuunga Mkono Rais wetu Dkt John Pombe Magufuli ili kutokomeza bishara hii.
“Watu wanachanganya, kuna tofauti kubwa kati ya kuitwa na kukamata, unapoitwa na mkuu wa mkoa unapewa haki yako ya msingi ya kusikilizwa, kwa hiyo hawa watu wajitokeze waje tutasikiliza maelezo yao. Kati ya hao 65, kuna wengine ni wauzaji wa madawa, wengine wamiliki wa kumbi za starehe ambazo ndani yake biashara hii inafanyika na wengine wanaufahamu vizuri huu mtandao hivyo watatupa ushirikiano ili kuwakamata wahusika.
“Kampeni ya madawa ya kulevya siyo ya kufanya kimya kimya, tunataka hata mtoto wa shule ya msingi aelewe kama madawa ya kulevya ni hatari. Alisema Makonda.
Orodha ya awamu ya pili ya Makonda ina jumla ya majina 65.
Chanzo: ZeDegree
Leave a Comment