HISTORIA YA KWELI YA JAMBAZI MSOMI NA ALIYEFANIKIWA ZAIDI KATIKA AZMA ZAKE - Pt. 1

Mwaka 2021 ulimwengu utashuhudia mmarekani aliyefanikiwa zaidi kutekeleza matukio ya ujambazi akitoka gerezani baada ya kutumikia kifungo cha miaka 17 baada ya kufanikiwa kuishawishi serikali na mahakama kupunguza kifungo chake kutoka miaka mia moja kumi na tano (115) mpaka miaka hiyo 17. Atakapotoka na kurudi uraiani atakuwa na miaka 69,
jina lake anaitwa Carl Gugasian au maarufu kama 'The Friday Night bank robber'! Muhalifu aliyeiumiza kichwa FBI kwa miaka 30 akitekeleza matukio 50 ya kuvamia na kuiba benki pasipo kukamatwa kitendo kilichopelekea FBI na waendesha mashitaka wa marekani 'kumsifu' kuwa ndiye muhalifu mwenye akili na aliyefanikiwa zaidi katika historia ya marekani (the most prolific bank robber)


Kumekuwa na kelele nyingi kutoka kwa 'mashabiki' wakiitaka Hollywood watengeneze muvi kuhusu maisha ya 'the friday night bank robber'! Jambo lililowashangaza wengi na ulimwengu wote ni jinsi gani binadamu mmoja aliweza kutekeleza matukio 50 ndani ya miaka 30 akiwa peke yake na FBI washindwe kujua identity yake wala kuwa na hata mbinu ya kuweza kumzuia au kumkamata.

Mbinu, weledi na nidhamu aliyokuwa nayo na kutumia kutekeleza matukio yake yalikuwa ni siri na kitendawili mpaka pale alipokamatwa na kuamua kuwasimulia FBI ili kujaribu kuwashawishi kumpunguzia adhabu ya kifungo.. Na hii ni historia yake 'kwa kifupi' tu
ALIWEKA DHAMIRA AWE "MUHALIFU MWELEDI"
Akiwa na miaka 15 Carl alitekeleza tukio lake la kwanza la ujambazi ambapo alijaribu kuiba fedha katika candy store bila mafanikio na alipigwa risasi tumboni na kukamatwa. Baada ya kukamatwa alipelekwa katika jela ya watoto ya Camp Hill kwa miezi 18.

Baada ya kutoka jela Carl alidhamiria sasa kuwa ni lazima awe muhalifu mwenye weledi wa hali ya juu kiasi kwamba atafanikiwa katika kila tukio na hatoweza kukamatwa na akadhamiria kama anataka kufanikiwa aibe fedha nyingi kwa wakati mmoja basi sehemu sahihi ya kuiba ni bank na kama anataka kweli awe muhalifu mweledi anatakiwa ajue namna sehemu hizo (majengo na mifumo) zinavyofanya kazi, afahamu namna ya kutumia silaha, ajue namna ya kujihami (self defense) na namna atakavyo toroka na fedha..

Baada ya kuweka dhamira hiyo Carl akachukua hatua ya kwanza na alichofanya ilikuwa ni kujiunga na Chuo kikuu cha Villanova ambapo alisomea Uhandisi wa umeme. Akiwa chuoni alitumia mwanya huo kujiunga na programu maalum ya jeshi la marekani kwa ajili ya kurecruit vijana walioko chuoni! Baada ya kumaliza Chuo akaenda kutumikia jeshi kwa muda mfupi kituo cha Fort Bragg na akiwa huko akapata mafunzo maalumu ya kijeshi (Special Forces and tactical weapons training)

Baada ya kupata mafunzo ya kijeshi Carl akarudi Chuo kusoma masters degree ya System Analysis na alipomaliza masters degree akafanya mafunzo ya awali kwa ajili ya shahada ya uzamivu katika Statistics. Pia mtaani alipokuwa anaishi alijiunga na kituo cha kufundisha mafunzo ya kujihami (karate and judo) ambapo alifanikiwa kupata mkanda mweusi (third degree black belt)

Baada ya kufanikiwa kufanya maandalizi yote hayo na kupata kila aina ya mafunzo na uzoefu aliyohitaji ili kuwa 'muhalifu wa daraja la kwanza' sasa ulikuwa ni wakati kwake kupita kila benki kukomba hela na kuudhihirishia ulimwengu kuwa hakujapata kuwepo na itachukua miaka mingi kutokea muhalifu professional kama yeye Carl 'the Friday night bank robber'..

#1: MAANDALIZI KABLA YA TUKIO
Moja kati ya vitu vilivyomsaidia Carl kufanya matukio ya uhalifu kwa mafanikio ni uwezo wake wa kuweka mkakati wa utekelezaji jinsi gani atakavyofanikisha azma yake! Ni dhahiri kuwa mafunzo ya kijeshi aliyoyapata yalimsaidia sana kuwa mwanamkakati mzuri wa kiufundi wa matukio! Carl alikuwa anatumia had I miezi kadhaa katika kupanga utekelezaji wa tukio moja tu..

Kwanza kabisa Carl ali scout bank zilizopo katika miji midogo. Baada ya kupata orodha ya benki katika miji kadhaa midogo then Carl aliangalia kati ya bank hizo ni bank gani haziko katikati ya mji (kwa maana kwamba ziko pembezoni/nje ya mji). Kisha Carl aliichagua bank moja wapo kati ya hizo na bank ambayo inakuwa haiko karibu sana na makazi ya watu au iko karibu na msitu basi bank hiyo anaipa kioaumbele katika orodha yake..

Baada ya kuamua ni bank gani atafanya tukio, Carl alianza tafiti juu ya tukio lenyewe atakavyolitekeleza... Kwanza kabisa Carl alianza kwa kusoma mandhari yanayozunguka bank na interest yake kubwa inaelezwa kuwa alitafiti zaidi msitu ambao unakuwa karibia na bank.. Inaelezwa kuwa Carl angeutembelea msitu huo na kuukagua nukta baada ya nukta, haijalishi ni muda gani angetumia mpaka kumaliza kuukagua!

Inaelezwa kuwa lengo lake lilikuwa ni kujua ni maeneo gani ya msitu ambapo watu huwa wanamazoea ya kupita au kutembelea, ni eneo gani la msitu limejificha zaidi, ni upande gani wa msitu unakuwa rahisi kuifikia barabara, ni eneo gani la msitu lina umajimaji na eneo gani ni kavu na kadhalika na kadhalika.. Inaelezwa kuwa Carl angeutafiti huo msitu na kuufahamu kuliko hata wenyeji wa eneo hilo husika.. Angeufahamu msitu nukta kwa nukta!

Baada ya kuufanyia tafiti msitu, inaelezwa kuwa Carl alikuwa anageukia kuitafiti bank yenyewe na wafanya kazi wake.. Kuhusu bank, angetafiti je hiyo bank inafungwa na kufunguliwa saa ngapi, ni siku zipi huwa wanachelewa kufunga, ni siku gani wanakuwa na kiasi kikubwa cha fedha n.k! Kisha akimaliza hapo anageukia kuwatafiti wafanyakaxi wa bank husika.. Hapa alitafiti kuhusu 'shifti' zao za kazini, nanj ni teller, nani ni manager na pia kitu kingine cha msingi alijitahidi kuwasoma personality zao..

Baada ya kumaliza kufanya 'tafiti' zake Carl alienda hatua ya pili ya maandalizi ambapo ilikuwa ni kuandaa 'makazi na stoo' yake ya muda katika msitu uliopo karibu na bank ambapo alichimba handaki dogo kwa ustadi mkubwa na kulificha kabisa kwa juu mtu asiweze kujua kwa namna yoyote ile.. Moja ya wapelelezi ambao walihusika kufanikisha kumkamata Carl anaeleza Bw. Carr anaeleza kuwa siku ambayo walifanikiwa kugundua na kuliona handani mojawapo ambalo lilichimbbwa na Carl walistaajabu (kumbuka Carl alikuwa na zaidi ya mahandaki 30 sehemu tofauti tofauti za nchi ya marekani)! Inaelezwa kuwa kinachostaajabisha kuhusu mahandaki ya Carl ni jinsi yalivyo chimbwa kiustadi na kujengewa kwa ndani kwa vitofali vidogo vidogo.. Pia handaki lilikuwa linampangilio wa hali ya juu wa kiwango cha kijeshi (military precision). Ndani ya handaki kulikuwa na kila kitu ambacho angekihitaji, silaha, nyaraka za 'research', kifurushi cha kujikimu (survival kit), madawa ya dharura (first aid kit), vinyago vya kuficha sura (masks), fedha taslimu, majarida ya mazoezi ya kawaida na kijeshi na vitu vingine vingi....!!!

Baada ya kumaliza maandalizi haya ya msingi Carl alijichimbia katika maktaba ya umma ya Philadelphia ambapo ndio alipafanya kama ofisi yake kwani inaelezwa kuwa alikuwa na mazoea ya kutumia muda mwingi hapo akifanya 'tafiti' na angekuwa hapo kwa wiki kadhaa ili ku-fainalize mpango wake na kufanya conclusion ya jinsi atakavyotekeleza tukio lenyewe..


Itaendelea makala ijayo...!


Mwandishi: The Bold

No comments

Powered by Blogger.