HISTORIA YA KWELI YA JAMBAZI MSOMI NA ALIYEFANIKIWA ZAIDI KATIKA AZMA ZAKE - Pt. 2

#2: UTEKELEZAJI WA TUKIO
Matukio yote ambayo Carl aliyafanya alikuwa anayetekeleza mwezi October au November ambapo maeneo mengi yanakuwa yapo kwenye kipindi cha winter au autumn ambapo kunaambatana na baridi kali pamoja na jua kuzama mapema! Pia matukio yake yote aliyatekeleza siku ya ijumaa na hii ndio iliyomfanya apewe jina la 'The Friday Night bank robber'...


Uchaguzi wake wa muda wa kufanya tukio ulimpa advantage kadhaa.. Kwanza kipindi cha winter na autumn jua linazama mapema kwa maana ya kwamba katika Masaa yale yale ambayo bank zinakuwa zinafungwa lakini katika kipindi hiki cha majira ya mwaka giza linakuwa limeanza kuingia hivyo inampa mwanya mzuri kufanya tukio.. Pia kufanya tukio ijumaa ilimaanisha kuwa ndio siku nzuri kwa bank kuwa na kiwango kikubwa cha Cash.. Lakini pia alitumia sababu ya kisaikolojia kuwa ijumaa wafanyakazi wanakuwa distracted kutokana na weekend kuanza hivyo umakini unakuwa mdogo..

Kwahiyo alichokifanya Carl kwanza ni kupaka 'harufu' kwenye nyumba zote zilizo karibu na bank ili kuwachanganya mbwa wa polisi wakija kujaribu kutafuta trail ya alikoelekea!

Now; siku ambayo Carl alikuwa anafanya tukio alivaa kinyago cha kutisha usoni ambacho kili-fit sawa sawa kabisa ili kuficha ngozi yake na! Pia alivaa manguo mengi ili kuleta muonekano kwamba ni mnene.. Na alikuwa akiingia ndani ya bank alitembea dizaini kama amechuchumaa mfano wa Kaa (crab)! Vitu vyote hivi alivyovifanya watu walihisi labda alikuwa na matatizo ya akili lakini hawakujua kuwa alivifanya kwa kusudi kabisa.. Alivaa kinyago cha kutisha ili kuleta effect ya kuogofya na kuficha tone ya ngozi yake, pia alivaa manguo mengi ili kuficha body size, na alitembea kama kaa akiwa kama amechuchumaa ili kuficha height!! Hii ilimsaidia sana kwani kwa miaka 30 FBI walishindwa kung'amua mtu wanayemtafuta alikuwa wa size gani, height gani au skin color ipi???

#3 KUVAMIA
Carl alikuwa anasubiri dakika 5 kabla bank haijafungwa ndipo alikuwa anavamia! Hii ilimpa possibility nzuri kuwa ndani kulikuwa na wafanya kazi pekee au Wateja wachache sana wamebakia... Akishavamia bank alitoa bastola na kuamuru watu walale chini na wasimuangalie! Mashahidi wanaeleza kuwa kwa ustadi mkubwa (labda kutokana na mazoezi ya karate) Carl aliruka kutoka alipo mpaka kwenye droo za ma-teller na kuweka fedha zote alizozikuta humo kisha kwa ustadi ule ule aliruka tena mpaka upande wa wateja na kuwaamuru tena kwa msisitizo wasimuangalie na kabla hawajang'amua kinachoendelea Carl alikuwa tayari ashatoka nje ya bank na kutokomea katika msitu ulio karibu..

Inaelezwa kuwa katika matukio yake yote aliyatekeleza ndani ya muda usiozidi dakika mbili! Yani chini ya dakika mbili alikuwa tayari amevamia, amekomba hela na ameshatokomea msituni..

Carl anaeleza mwenyewe kuwa akiingia ndani ya msitu alikuwa anakimbia kwa dakika kadhaa kama kumi hivi mpaka mahala ambapo anakuwa ameficha baisikeli kisha anaendesha mpaka ndani ndani kabisa ya msitu kulipo na handaki lake, akifika kwenye handaki kila kitu anakiacha hapo; fedha alizoiba, masks, nguo, gloves etc kisha anavaa nguo nyingine za kawaida anaendesha baisikeli anaondoka! Carl anasema kuwa ataendesha baisikeli kwa muda wa kama dakika ishirini au zaidi mpaka upande wa pili wa msitu ambapo kuna barabara na hapo kunakuwa kuna gari amepaki linamsubiri.. then anawek baisikeli ndani ya gari anaendesha kama raia wa kawaida na kuelekea nyumbani..

Carl anasema alikuwa anacha wiki au miezi ipite mpaka stori kuhusu tukio la ujambazi zianze kufifia ndipo anarudi kwenye ule msitu na kuchukua 'hela zake'... Baada ya hapo maisha yanaendelea na anaanza 'tafiti' kwa ajili ya tukio linalofuata..

#4: KUKAMATWA NA MAZINGAOMBWE YA HUKUMU
Kukamatwa kwa Carl kulikuwa kwa bahati mbaya mno! Kuna watoto walikuwa wanacheza katika msitu uliopo karibu na nyumbani kwao! Wakiwa ndani ya huo msitu waliokota PVC tube/pipe iliyokuwa imefichwa.. Baada ya kuifungua ndani walikuwa ilikuwa na bastola na vitu vingine kadhaa vinavyotia shaka. Wale watoto wakawataarifu wazazi wao na wazazi wao wakashauri vipelekwe polisi! Baada ya vitu hivyo kupelekwa polisi, vikachunguzwa na kukakutwa ramani.. Polisi walipoifuatilia ile ramani ikawqpeleka moja kwa moja kwenye handaki dogo ndani ya msitu! Kutokana na vitu vilivyokutwa ndani ya handaki hilo polisi wakapata wasiwasi kuwa inawezekana wanadeal na ishu serious kuliko uwezo wao hivyo wakawataarifu FBI! Baada ya FBI kuwasili iliwachukua masaa kadhaa tu kung'amua kuwa vitu hivyo vinahusiana moja kwa moja na Jambazi wanayemtafuta kwa miaka 30, The Friday night bank robber.

FBI walitumia alama za vidole walizozikuta kwenye ile handaki na pia walitumia kijarida kidogo kinachohusu kituo cha mafunzo ya karate kumtrack down Carl mpaka wakampata. Siku Carl anakamatwa alikutwa "ofisini kwake" Maktaba ya Philadelphia Free Library akiwa anafanya "tafiti"

Baada ya kukamatwa na kesi kufikishwa mahakamani ilikuwa ni dhahiri kuwa Carl atahukumiwa kifungo cha maisha au aghalabu miaka 115 pasipo uwezekano wa kupata parole kutokana na mashitaka yanayomkabili lakini mwisho wa siku Carl alikubaliana deal na FBI kuwa awaeleze nukta kwa nukta kuhusu matukio yote 50 aliyoyafanya, pia akubali kushirikiana na FBI kutengeneza programu maalum kuwasaidia maafisa wa FBI kutambua namna ya kuwabaini 'serial criminals', na pia awaelekeze kuhusu saikolojia ya ku-plan matukio ya uhalifu yaliyo perfect.!

Carl akakubaliana na masharti yote haya na mahakama ikapunguza adhabu yake kutoka kifungo cha maisha mpaka kifungo cha miaka 17 bila parole..

Hivyo basi ikifika 2021 Carl Gugasian anarudi uraiani! Inaelezwa kuwa huko gerezani Carl ni mtu mnyoofu mno na ni mfungwa wa kuigwa na ameendeleza desturi yake ya kupenda mazoezi hivyo yuko katika afya njema sana na wengi wanaamini atafika 2021 akiwa salama salimini na naamini kabisa Hollywood wanaomba usiku na mchana atoke salama ili wamfanye celebrity na watupe bonge la muvi.!!


Mwisho

Mwandishi: The Bold

Chanzo: JamiiForums

No comments

Powered by Blogger.