MONI CENTROZONE AMJIBU YOUNG DEE KWENYE NGOMA YAKE MPYA ALIYOMSHIRIKISHA BARAKA DA PRINCE

Msanii anayefahamika kwa jina la Moni Centrozone siku ya juzi aliachia ngoma inayokwenda kwa jina la Matango Pori akimshirikisha Barakah Da Prince. Kwenye chorus ya nyimbo hiyo amesikika Barakah akisema "Bongo kama ulaya
sitaki kwenda mtoni" wakati hivi karibuni msanii Young Dee aliachia ngoma inayokwenda kwa jina la Bongo Bahati Mbaya BBM akijaribu kuonyesha kiasi gani yeye ni mnyamwezi mpaka watu wanahisi amezaliwa BBM.
Nyimbo ya Moni ni kama imemjibu Young Dee kupitia mstari alioimba Baraka kwa chorus,  "Bongo kama ulaya sitaki kwenda mtoni". Be Radio wakishirikiana na BlackMutu Blog walijaribu kumtafuta Young Dee atuambie amepokeaje majibu ya nyimbo yake, lakini hakupatikana kwa simuj yake na wakati 
imepatikana ilikuwa ikiita bila majibu. Hata hivyo tulimpata mmiliki wa nyimbo hiyo, msanii Moni na akatuambia kuwa nyimbo yake sio jibu kwa nyimbo ya Young Dee. Moni anasema, "Young Dee ni mwanangu, chafu yangu kabisa na hatujawahi kuwa na beef kwahiyo napokwambia hii nyimbo sio jibu kwa BBM elewa ivo ivo ivo" alimaliza Moni. Ngoma ya Moni Centrozone imefanywa na Pancho Latino kwenye studio za B'Hits. 

Owk wewe kama shabiki unahisi nini, Moni kamjibu Young Dee ama nini?
 Ngoma ipi kali kati ya Matango Pori na Bongo Bahati Mbaya? 

No comments

Powered by Blogger.