MWANAJESHI WA MAREKANI AKIRI KUUA RAIA ZAIDI YA 2700 HUKO IRAQ

Mwanajeshi mmoja wa Marekani amekiri kuua kinyama zaidi ya Wairaki 2000 katika kipindi cha miaka mitano aliyohudumu nchini humo. Kwa mujibu wa televisheni ya Marekani ya Fox News, Sajenti Dailard Johnson aliye na umri wa miaka 48 anahesabiwa kuwa askari katili zaidi katika historia ya Marekani ambaye amekiri kwamba katika kipindi cha miaka mitano aliyohudumu nchini Iraq yaani kati ya mwaka 2005 na 2010, alichinja na kuwaua kinyama na kwa makusudi zaidi ya Wairaki 2,746. Akikiri kuhusiana na unyama wa jeshi la Marekani, Johnson amesema kuwa hakuna hata siku moja iliyopita katika kipindi hicho alichohudumu Iraq, bila ya kuua raia mmoja au wawili wa nchi hiyo. 

Akifafanua zaidi ukatili wake huo, mwanajeshi huyo wa Marekani anasema kuwa katika mauaji yake ya kwanza alikanyaga na kuponda kwa gari lake la kijeshi, basi moja lililokuwa limebeba abiria 13 na kuwaua wote papo kwa hapo. Jambo la kusikitisha zaidi ni kwamba mwanajeshi huyo katili alitunukiwa na jeshi la Marekani medali 37 za heshima na shukrani na kutajwa kuwa 'shujaa wa vita.' Katika hali ya hivi sasa askari huyo anaugua maradhi mengi ya kisaikolojia na tayari mke wake amemkimbia. 
Kuna visa vingi ambavyo vimeripotiwa kuhusiana na unyama na ukatili uliofanywa na wanajeshi wa Marekani huko Iraq. Ripoti za taasisi za kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa zinaonyesha kwamba tokea wakati wa kuvamiwa Iraq, wanajeshi wa Marekani wamehusika na visa vingi ambavyo vimepelekea kuuawa kinyama maelfu ya raia wa nchi hiyo wakiwemo wanawake na watoto wadogo.

Chanzo: CSMonitor

No comments

Powered by Blogger.