PICHA: ITAZAME HAPA NDEGE MPYA YA MCHUNGAJI GWAJIMA

Historia ya ndege hiyo ya Askofu Gwajima,toka ilipotengenezwa,wamiliki wake wa mwanzo na usajili wake ulivyokuwa ukibadilika kutokana na wamiliki. Na mara ya mwisho kabla ya kuwa katika "Order" ilikuwa inamilikiwa na "Gori Aviation LLC" mpaka tarehe 04.04.2017.
Juu na chini ndio muonekano wa ndege aina ya BAe/Hawker 125-800A na "N609RB" ni namba ya usajili wake kwa utaratibu wa US na sio "aina ya ndege".
Hiyo ndege ya Askofu Gwajima ni moja ya ndege za anasa za Wafanyabiashara na matajiri,hupendelewa sana na watu wa North America. Ni ndege aina ya British Aerospace/Hawker 125-800A (BAe 125-800B) na si Gulfstream kama ilivyoadikwa na vyombo vingi vya habari na mitandao ya kijamii. British Aerospace Plc ni kampuni ya kutengeneza ndege(Jet Business Aircraft) kwa ajili ya "Executive",yenye makao yake makuu Farnborough,Hampshire-United Kingdom.Kampuni hii ndio haswa "Manufacturer" wa ndege inayotazamiwa kumilikiwa na Askofu Gwajima..!!

Kwanza hakuna ndege aina ya "Gulfstream N609RB".
Gulfstream ni jina la kampuni ya utengenezaji wa ndege iliyoko huko Savannah,Georgia(US),wakati "N609RB" ni namba za usajili wa ndege husika na si aina ya ndege. Ndege zote kama yalivyo magari huwa na namba za usajili,ni kama vile kuwa na gari aina ya Toyota Carina yenye usajili wa T459 DDT,hiyo "T" ni maana gari imesajiliwa Tanzania japo inaweza kuwa imetengenezwa Japan.

Hivyo ndege zote zinazosajiliwa US huanza na herufi "N".Ni kama vile ndege zote zinazosajiliwa Afrika Kusini huanza na "ZS",ndege zinazosajiliwa Tanzania huanza na "5H",majirani Kenya huanza na "5Y" wakati Uganda "5X",na ndio maana bombadia zetu mojawapo imesajiliwa kwa "5H-TCB",au ile ya Rais ni 5H-ONE au ile chopa ya Askofu Gwajima imesajiliwa kwa 5H-OLY.
A post shared by Bishop Josephat Gwajima PhD 🌍 (@bishopgwajima) on
Kuandika Askofu Gwajima kanunua ndege aina ya "Gulfstream N609NB" ni sawa na kusema Tanzania imenunua ndege aina ya "Gulfstream 5H-TCB",wakati ile ya ATCL ni aina ya "DH-8 Q400" yenye usajili wa 5H-TCB. Haya ni makosa yanayopaswa kurekebishwa maana hata waandishi wa habari wa magazeti ya Kiswahili na Kingereza wameibeba habari hii na kuandika Askofu Gwajima anunua ndege aina ya "Gulfstream N609RB",
kitu ambacho si sahihi kabisa kabisa.
Kwa Afrika Mashariki na Ukanda wa maziwa makuu,Rais wa Tanzania,Uganda na Rwanda ndio wanamiliki ndege za "anasa" kutoka Gulfstream Aerospace Corporation.Iliyo "latest" zaidi ni ya Rais Kagame ambayo ni Gulfstream 650(G650). Kwa wachungaji wa Afrika,T.B Joshua na Prophet Bushiri wa Malawi ni kati ya wanamiliki wa aina hii ya ndege.Mwaka 2015 wakati T.B Joshua amefika Tanzania,alitua na ndege aina hiyo yenye usajili wa US.

No comments

Powered by Blogger.