VIKONGWE MAJAMBAZI WALIOTIKISA DUNIA YA UHALIFU (Part 2)

UTEKELEZAJI WA TUKIO

Baada ya mwezi mmoja mkakati ukawa umekamilika. Wakawa na mpango kamilo wa namna gani watakavyo ingia katika vault. Kilichokuwa kimebakia ni kuteua siku ambayo wataweza kutekeleza tukio hilo. Na kwa haraka tu walogundua kwamba kampuni ya H.G.S.D huwapa mapumziko wafanyakazi wake wote mpaka walinzi katika kipindi cha sikukuu yeyote ile. Hii ilidhihirisha ni namna gani walikuwa wanajiamini kupitiliza juu ya teknolojia yao ya ulinzi katika vault zao.

Habari njema zaidi kwa Wazee hawa ilikuwa ni pale walipogundua kwamba kwa mwaka huo 2015 sikukuu inayojulikana kama 'Bank Holiday' nchini Uingereza kwa mwaka huo 2015 inaungana na sikukuu ya Pasaka. Sikukuu hii ya 'bank holiday' huadhimishwa mara moja kila mwaka katika nchi nyingi za jumuiya ya madola ambapo wafanyakazi wa mabenki na sekta nyingine hupumzika kwa siku mbili.

Kwa mwaka 2015 sikukuu hii ilidondokea siku ya Jumatano tarehe 1, April. Hivyo hii ilimaanisha kuwa Jumatano na Alhamisi zingekuwa ni maadhimisho ya sikukuu ya bank holiday, Ijumaa itakuwa ni Ijumaa Kuu, na Jumamosi siku ya mapumziko na Jimapili itakuwa pasaka yenyewe na Jumatatu itakuwa ni Jumatatu ya Pasaka.

Hii ilimaanisha kuwa kulikuwa na siku sita za mapumziko ambazo wafanyakazi watakuwa majumbani. Huu ulikuwa ni mwanya mzuri ambao wazee hawa waliuona ili waweze kuyekeleza tukio lao. Hivyo wakakata shauri kwamba tukio lao watalitekeleza kuanzia siku ya Jumatano Tatehe 1, April 2015.

Siku ya Jumatano asubuhi tarehe 1 april, 2015 mafundi bomba wale wawili (Doyle na Lincoln)ambao walikuwa wafanyakazi katika jengo hili na majengo ya jirani na ambao walikuwa wameshawishiwa na Mzee Brian Reader na kukubali kujiunga na genge hili la wazee hawa kutekeleza tukio, walipewa maelekezo na mzee Brian kufanya jambo la msingi sana.

Walienda kwenye jengo la jirani na jengo lenye vault wakijifanya kama kuna mabomba wameenda kuyarekebisha. Wakafanikiwa mpaka kuingia sehemu ya chini ya jengo yenye mfumo wa mabomba ya gesi ya matumizi ya nyumbani ambayo mabomba hayo yanaelekea kwenye vymba vya jengo hilo na majengo ya jirani.

Walichokifanya mabwana hawa ni kufanya uharibifu wa makusudi kwa mabomba kadhaa ya gesi na kuzichuna baadhi ya nyaya za umeme na kuondoka.
Kutokana na uharibifu walioufanya ulisababisha gesi ianze kuvuja.

Muda si mrefu ukatokea mlipuko mkubwa wa moto kutokana ma uvujaji huo wa gesi. Hii ilisababisha polisi na zima moto kuwaondoa wakazi wote (evacuation) waliokuwa wanakaa kwenye jengo lililowaka moto ma majengo ya jirani likiwemo jengo lenye vault, wakiwataka watafute sehemu nyingine za kukaa au waende kukaa kwa ndugu au marafiki zao mpaka pale ambapo zima moto watakapofanikiwa kugundua chanzo cha moto huo na kukidhibiti.

Hii ilimaanisha kuwa kwa siku hizo za sikukuu majengo hayo ya karibu pamoja na jengo lenye vault hayatakuwa na wakazi isipokuwa kwenye jengo la jirani na jengo lenye vault kutakuwa na zima moto pekee wakiwa na pilika za kujua chanzo cha moto. Lakini kwenye majengo mengine likiwepo jengo lenye vault yatakuwa tupu kabisa bila wakazi wake.

Kwahiyo jioni ya siku hiyo Mzee Brian na genge la wazee wenzake wakaingia kazini.

Kama nilivyo eleza awali kwamba 'mchora ramani' wa tukio hili aliitwa Basil, ingawa jina hili alitungwa tu na polisi kwani hawamjui ni nani na wala hawajui jina lake halisi. Lakini inaonekana alikuwa ni mtu mwenyw 'access' na hili jengo.

Hivyo majira ya saa mbili usiku Basil akiwa amevalia nadhifu kabisa alifika mbele ya jengo hili na kufungua mlango wa mbele kwa kutumia funguo na kisha kuingia ndani. Mpaka leo hii haijulikani Basil alipata wapi funguo za jengo. Wenzake waliosalia walikuwa nyuma ya jengo ambapo baada ya yeye kuingia ndani aliwafungulia mlango wa nyuma na wote wakaingia ndani. Kama nilivyoeleza awali kwamba lifti katika jengo hiki ilitengenezwa katika mfumo kwamba haiwezi kushuka chini kwenye basement Bali ilikuwa inaishia 'ground floor'.
Badala ya hili kuwa kikwazo, wazee hawa walichukulia hili kama fursa kwao.

Baada ya wote kuingia ndani wakapandisha ngazi mpaka ghorofa ya pili. Walipofika ghorofa ya pili wakabonyeza kitutufe cha kuiita lifti kuja juu ghorofa ya pili. Lifti ikapanda juu mpaka ghorofa ya pili. Ilipofika wakaharibu nyaya na mtambo wa lifti kifanya ibaki hapo hapo ghorofa ya pili isishuke au kupanda juu au kwa ufupi lifti ikawa imeharibika haifanyi kazi but imeganda ghorofa ya pili.

Baada ya hapo wakashuka tena mpaka ground floor.

Hapa nieleze kidogo.

Mfumo wa lifti (elevator) ulivyo, ni kwamba kwenye kile kijichumba unachoingia baada ya milango ya lifti kufunguka ni kama kiberenge au kijikontena ambacho kina panda juu au chini kutegemea na unakoelekea. Sasa kiberenge/kikontena hiki kinauwezo wa kupanda juu au chini kwasababu kimewekwa kwenye eneo la jengo lililotengenezwa kwa kuacha uwazi/shimo kuanzia chini ya jengo mpaka juu. Kwahiyo ndio kusema kwamba, kama kiberenge kile kikiondolewa na ukifungua mlango wa lifti utakutana na uwazi/shimo refu linaloanzia chini ya f
Ghorofa mpaka juu. Uwazi/shimo hili linaitwa 'elevator shaft'.

Sasa, nimeeleza hapa kwamba wazee hawa walipanda mpaka ghorofa ya pili na kuita lifti ije juu kisha wakaiharibu igande hapo isishuke wala kupanda kisha wenyewe wakashuka tena ground floor. Sasa waliposhuka geound floor wakafungua mlango wa lifti na baada ya kuufungua mlango wa kifti wakakutna na shimo (elevator shaft) kuelekea chini kwenye basement kwa vile 'kiberenge' cha lifti kiliganda juu ghorofa ta pili.
Na hili ndilo lilikuwa lengo lao.

Kumbuka nimeeleza kuwa lifti ilitengenezwa kwa mfumo ambao ulikuwa haina uwezo wa kushuka chini kwenye basement, kwahiyo walifanya hivi kwa makusudi ili wapate upenyo wa kushuka chini kwenye basement.

Kwahiyo, baada ya kufungua mlango wa lifti na kukuta shimo ambalo lilikuwa na urefu wa kimo kama cha binadamu wawili (futi 12) ndipo hapa Basil ambaye ndiye alikuwa kijna zaidi ilibidi aruke kwa ustadi mpaka chini kwenye basement.

Wakati Basil akiwa tayari amefanikiwa kufikakwenye basement kwa kuruka, wenzake wakapandisha tena ghorofa la kwanza.
Hapa napo panahitaji kupaelewa kwa umakini.

Katika majengo yote ya ghorofa huwa zinawekwa njia/ngazi (stairs) maalumu kwa ajili ya mtu kupita pale inapotokea hali ya taharuki, na hasa taharuki ya moto. Njia/ngazi hizi zinaitwa 'Emergency fire exit'.

Katika jengo hili ngazi hii ilijengwa katika namna ambayo kama mtu akipita anatokea chini kabisa ya jengo (kwenye basement) lakini anakuwa hayuko ndani ya basement kwani kunakuwa na mlango wa lifti unao mtenganisha yeye na ndani ya basement, na mlango huu wa lifti unaoukuta hapo haufunguki kwa kuwa lifi haifiki huku kama nilivyoekeza. Kwahiyo hapa unakuta mlango wa lifti (ambao haufunguki) na mlango mwingine mbele yako ambao unaweza kuufungua na kutoka nje.

Lakini kitu ambacho wengi walikuwa hawajui na wazee hawa walikigundua baada ya kufanya utafiti kipindi wanapanga mikakati yao ni kwamba, mlango huu wa lifti ulikuwa una funguka kwa ndani. Na hii ilitengenezwa hivi makusudi na wenye jengo ili kusaidia kufanya usafi au marekebisho kwenye shimo la lifti (elevator shaft).

Kwahiyo wazee wale walipopanda mpaka ghorofa ya kwanza wakatumia njia ya dharura (emergency fire exit) na kushuka nayo mpaka chini ya jengo na kufika nje ya basement (mbele la mlango wa lift kwenye basement) na Basil ambaye tayari yupo ndani ya basement akawafungulia mlango wa lifti (nimeeleza mlango huu ilikuwa unafunguka kutokwa ndani). Pia kumbuka hapa hakuna shimo la lifti ka kwenda chini (elevator shaft) kwa kuwa ndio mwisho wa jengo ila kuna shimo/uwazi kwenda juu.

Kwahiyo baada ya Basil kuwafungulia tayari wote wakawa wako ndani ya basement. Kisha wakafungua ule mlango wa kioo nilioueleza mwanzoni, na baada ya kufungua hapa unakuwa uko mbele ya mlango wa Vault yenyewe, ambao ukiufungua tu unakuwa uko ndani ya chumba cha vault. Lakini kama nilivyoeleza awali kwamba ukifungua tu mlango wa kioo unakuwa na sekunde 60 kuingiza tarakimu za siri ukutani kwenye keypad ili kuifanya alarm isitoe mlio kuashiria uvamizi (intruder alart) na kutuma meseji kwenda polisi.

Kwa kuwa hawakuwa na tarakimu hizo za siri, Basil akaifungua haraka haraka hiyo keypad ukutani na kukata nyaya kadhaa kwa ufundi ili kuifanya alarm hiyo isifanye kazi. Hii ikifanikiwa kwa 50% pekee kwani ni kweli alarm haikulia lakini meseji ilitumwa kwenda polisi.

Polisi wakawasiliana na kampuni ya H.G.S.D ambao wakatuma MTU kwenda kwenye jengo na alipofika kwenye jengo na kukuta mlango wa mbele haujavunjwa, akachungulia ndani milango pia haijavunjwa (kumbuka wazee walitumia mbinu nyingine kuingia sio kuvunja milango) na wala hakuona purukushani yeyote akawapigia simu polisi na kuwaeleza kwa kifupi tu "false alarm" (kwamba ni matatizo tu ya kiufundi ila Vault iko salama.
Hakujua kabisa kwamba wanaume wako ndani wanashughulika.

Baada ya Basil kukata nyaya za alarm, mioyo yao ikatulia wakajua wako salama.
Sasa walikuwa mbele ya vault na kizingiti pekee kichobakia mbele yao kilikuwa ni mlango wa vault. Mlango huu ulikuwa wa Chuma na ni mnene sana ukiwa na sentimita 50 na ulihitaji uingize mfululizo wa tarakimu za siri (combination) ili uweze kuufungua.

Hapa ilikuwa ni dhahiri kabisa kuwa wasingeweza kuufungua mlango huu, hivyo njia pekee ambayo walikuja wakiwa wamejiandaa kifanya ilikuwa ni kutoboa ukuta. Walikuwa wamekuja na mashine kabisa ya kutobolea (drill) ambayo ilikuwa na ncha ya almasi.

Walikuja na Mashine hii maalumu yenye ncha ya almasi kwasababu ukuta wa vault pia ulikuwa na unene mkubwa (sentimita 50) na ulijengwa kwa tofali nzito. Hivyo kazi ya kuanza kutoboa ikaanza. Iliwachukua takribani masaa matatu kutoboa matundu matatu ya mduara yanayo ingiliana (overlaping circles). Baada ya kutoboa wakakutana na jambo ambalo hawakulitegemea kabisa. Mbele ya ukuta (ndani ya vault) kulikuwa na mgongo wa kabati la visanduku vya watu kuhifadhia Mali zao. Kabati hili lilitengenezwa kwa kkunganishwa moja kwa moja kwenye ukuta hivyo haijalishi unalisukuma vipi haliwezi kudondoka.

Wazee wakachoka. Hili hawakulitegemea na hawakujiandaa nalo. Wakabishana sana kuhusu wafanye nini lakini mwishowe wakakubaliana waondoke kwenda kufikiri zaidi wanakabiliana vipi na changamoto hiyo. Kumbuka hii ilikuwa ni "weekend ndefu" karibia siku sita za mapumziko, hivyo hawakuwa na wasiwasi kwani wafanyakazi wa vault hawaji mpaka sikukuu zipite.

Hivyo wakaondoka eneo la tukio na kurejea makwao. Kesho yake wakakutana na kufanya kikao kujadili namna ya kulisukuma lile kabati ndani ya vault ili waweze kuingia. Baada ya majadiliano marefu wakaafikiana kuwa watumie Mashine ya mtetemo/msukumo yenye uwezo mkubwa kwa ajili ya kufannikisha hilo.

Wakamuagiza Mzee Jones kwenda kununua Mashine hiyo, na akanunua Mashine murua kabisa yenye uwezo wa kusukuma kitu chanye uzito hadi wa tani kumi (10 ton hydraulic ram). Usiku wake wakarejea tena kwenye vault, kazi ikaendelea. Iliwachukua dakika kumi pekee kutumia Mashine waliyokuja nayo kuweza kudondosha kabati iloyokuwa inawazibia njia ya kuingia.

Baada ya kudondosha kabati hiyo. Mzee Carl wood (yule nadhifu) ambaye ndiye alikuwa mwembamba kuliko wote pamoja na mzew Jones ambaye alikuwa na stamina na fiti zaidi ya wore wakajipenyeza kwenye uwazi waliotoboa na kuingia ndani ya vault.

Wakatumia siku nzima iliyofuata (jumamosi) kufungua visanduku vya kuhifadhia mali ndani ya vault. Ndani ya vault vault kulikuwa na jumla ya visanduku 966 na mpaka kufikia jumapili walifanikiwa kufungua visanduku 396 na ilikuwa inatosha.

Walifanikiwa kuchukua kiwango kikubwa cha madini ya dhahabu, alamsi na fedha taslimu vyote vikiwa na thamani ya zaidi dola milioni 200 za marekani.
Kwahiyo wakafunga mzigo na kuondoka kwenda kugawana mzigo na kuka pasaka na familia yao jumapili hiyo.
Tukio lilikuwa limefanikiwa kwa asilima 100.

* * * * * * * * * * * * * 

Jumanne baada ya wafanya kazi kuja kazini ndipo walipogundua kuwa vault imevunjwa na kuibiwa. Taarifa ikatumwa polisi na upelelezi ukaanza mara moja. Lakini kwa miezi minne ya upelelezi polisi hawakufanikiwa kung'amua lolote kuhusu kesi hiyo.

Ndipo hapa ambapo kesi ikahamishiwa kitengo maalumu cha weledi wa hali ya juu ndani ya jeshi la polisi nchini uingereza, kitengo kinachojulikana kama Flying Squad.

Baada ya miezi minne ya uchunguzi huku wakitumia picha za CCTV camera za jengo lililopo mkabala na jengo lenye vault iliyoibiwa wakafanikiwa kupata picha y ya gari iliyoonekana kupaki katibu na jesngo la vault usiku wa siku ya tukio na walifuatilia gari hii ilikuwa inamilikiwa na Mzee Collins "kenny" (yule mtoto wa mjini mjanja mjanja) na hii ilipekekea mwezi january mwaka huu 2016, mzee Collins kukamatwa na baada ya mahojiano marefu kwa wiki kadhaa akakiri kuhusika na tukio hilo na kuwataja wenzake.

Baadae wenzake wote walikamatwa na mwezi march mwaka huu wakafikishwa mahakamani na mwezi june wote wakahukumiwa miaka sita jela.

Lakini mastermind mwenyewe wa tukio hili ambaye hajulikani jina lake halisi mpaka leo na polisi wamembatiza jina la Basil, hajulikani alipo mpaka leo hii na vitu vyote vilivyoibwa vyenye thamani ya zaidi ya bilioni 400 za Tanzania havijapatikana.

Tukio hili linaingia kwenye vitabu vya historia kama tukio la ujambazi lenye thamani kubwa zaidi, lakini historian kubwa zaidi ni kwamba lilitekelezwa na wazee vikongwe.

Kipindi bado wahusika wa tukio hili hawajakamatwa, zilizagaa habari katika mitaa ya London kuwa kutokana na weledi na akili kubwa iliyotumika kutekeleza tukio hili, iliaminika kuwa tukio hili lazima lilitekelezwa na majambazi sugu ambao yawezekana wamewahi kutumikia kwenye vikosi maalumu vya kijeshi kama SAS au Navy SEALs… Ulimwengu ulishikwa na butwaa siku wahusika wamekamatwa na kutangazwa kwamba ni vikongwe vyenye miaka zaidi ya 70 na wengine 60.

Mwisho.

Mwandishi: The Bold

No comments

Powered by Blogger.