ELIZABETH MICHAEL "LULU" AKUTWA NA HATIA YA KUUA BILA KUKUSUDIA, AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MIWILI

Mahakama kuu imemhukumu msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu baada ya kumtia hatiani kwa kosa la kuua bila kukusudia aliyekuwa muigizaji mwenzake, Stephen Kanumba Julai 4, 2012 eneo la Sinza Vatican jijini Dar es Salaam.

Asubuhi ya Novemba 13, Jaji Sam Rumanyika alisoma maelezo ya mwenendo wa kesi yaliyotolewa na upande wa serikali ukiongozwa na wakili Faraja George na upande wa utetezi ulioongozwa na wakili Peter Kibatala.Jaji Rumanyika alisema mshtakiwa Lulu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na marehemu kwa miezi minne na alikuwa mtu wa mwisho kuwa na marehemu Stephen Kanumba kabla ya kuanza mzozo uliosababisha kifo chake.

Katika hukumu yake, Jaji Rumanyika amesema Lulu alijichanganya katika maelezo yake mahakamani na alishindwa kuiambia mahakama historia ya marehemu jambo lililotazamiwa ni kutokana na muda wa uhusiano waliokuwa nao.

Mahakama imeonyesha kushangazwa na madai ya mtuhumiwa kwamba alipigwa na marehemu kiasi ya kitishiwa kuuawa lakini hakuna alichofanya kujitetea, ameshindwa kuiambia mahakama iwapo Kanumba alianguka wakati akimburuza kumrudisha chumbani kufuatia alichodai Kanumba alikuwa amelewa wakati wa tukio.Kuhusiana na umri mdogo wa Lulu wakati tukio hilo linatokea mwaka 2012, Jaji Rumanyika amesema sheria ya kumlinda mtoto haimpi kinga Lulu kwa sababu huo alikuwa akifanya mambo ya watu wazima.

Akihitimisha, Jaji Rumanyika alisema hakuna mashaka na mahakama imejiridhisha kuwa kifo cha Kanumba kilitokana na ugomvi.Wakili wa Lulu, Peter Kibatala amesema wanatarajia kukata rufaa dhidi ya hukumu hio na na wakati rufaa inafanyiwa kazi wataomba dhamana.

Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.