JE, SERIKALI YA TANZANIA ITAFANIKIWA KUMKAMATA MWANADADA MANGE KIMAMBI?

Soma tafadhali tujifunze kitu

Siku kadhaa tumepata sikia, IGP Simon Siro akisema jeshi la polisi linatambua makosa ya kimtandao yanayofanywa na mwadada Mange Kimambi na wanayashughulikia huku mitandaoni kumekuwa na maswali mengi watu wakijiuliza kama sheria yetu ya mtandao (cyber crime act, No 14 ya 2015) kama inawahusu walio nje ya nchi au laa wengi ne wakijiuliza kama ni ya kimataifa au laa.

Ukiisoma sheria hii ya mtandao ya 2015 kifungu cha 30(1)d "mahakama ina nguvu ya kushughulikia kosa lilofanywa na raia wa nchi hiyo hata kama akiwa nje ya nchi, kama kosa hilo linatazamwa kama kosa katika sheria za nchi husika". Kwa ujumla tuseme sheria hii inaweza kumuhusu hata Raia aliye nje ya Tanzania.

Tuanzie hapo Mange Kimambi ni Mtanzania au mmarekani? Mange kimambi sio mmarekani ni Mtanzania, ila ni mkazi wa marekani (US Resident) wengine wanasema anaishije kwa Visa hapana, visa ni pass ya muda ya mtu kuingia marekani na kukaa kwa kipindi fulani kifupi cha Muda, hivyo Mange kimambi hatumii visa anatumia Green Card hii ni permit inayomfanya Raia ambaye sio wa marekani kuomba hii kwa kuonesha supporting documents na kulipia ada ,hii unaruhusiwa kukaa ndani ya miaka 10,unaruhusiwa ku renew miezi sita kabla ya mwaka wa kumi(kabla ya expire date).hufanywa na idara ya USCIS (united state citizens and immigration services).

Hivyo tunamalizia kusema *Mange ni Mtanzania* ila ni mkazi wa marekani kupitia Green card. Vipi kukamatwa kwake?.

Sheria ya ndani kusema ina muhusu hata Mtanzania aliye nje ,haitoshi ila huenda sambamba na sheria za kimataifa (international law).kuna sheria ya kimataifa inaitwa extraterritorial Jurisdiction uwezo wa nchi kumshtaki mtuhumiwa aliyenje.,ambapo zimegawanyika kuna "passive personality principle of jurisdiction" ,kuna universal principle of jurisdiction, na pia kuna Nationality principle of extraterritorial jurisdiction sasa Mange kimambi hii Nationality principle of Extraterritorial jurisdiction ina muhusu, kwanini?

Hii nationality principle ,ni aina ya sheria ya kimataifa inatoa haki kwa nchi fulani kushtaki Raia aliyetenda kosa la kihalifu nje ya nchi hiyo ila likawa na athari kwa Raia ya nchi hiyo fulani.mange ametenda kosa la mtandao akiwa US ambalo kosa hilo lina athari kwa Tanzania, Tanzania kisheria inaruhusiwa kwenda kumkamata ila.tuelewane hapa.

Katika sheria za kimataifa na Uhuru wa nchi husika,nchi hairuhusiwi kumkabidhi mhalifu au mtu aliyekosa katika nchi ya nje sababu kila nchi ina mamlaka ya Raia walio ndani ya nchi yake *Mange kimambi yupo chini ya mamlaka ya nchi ya marekani*

Ndio maana ili kupunguza mamlaka ya nchi juu ya raia wote waliondani ya nchi hiyo,nchi inayotaka kumkamata raia kutoka nchi ya nje lazima wawe wameingia makubaliano(mkataba) unaitwa *Bilateral extradition treaties*, .extradition nini ,ni hali ya nchi moja kuomba nchi fulani kuruhusu muhusika au raia wake aliyetenda kosa apelekwe kushtakiwa katika nchi hiyo(Tanzania inamuomba mange kutoka marekani).pia inahusu aliyeshtakiwa akakimbia ,aliyeshakiwa akiwa huko nje,au ambaye bado hajashtakiwa ila ametenda kosa.
Tanzania sijui kama imewahi ingia mkataba wa *extradition treaties*na marekani,hata kama bado katiba ya marekani na marekebisho yake ya 1996 ,18 USC,3181 na 3184 inaruhusu kukubali extradition kusafirishwa kwa mtu au mtuhumiwa bila hata extradition treaties (bila mkataba).

Ila sio asafirishwe kizembe kuna mchakato wake.

Mchakato ni serikali ya Tanzania, kutuma maombi ya kukamatwa kwa Mange kimambi katika ubalozi marekani (country embassy) ,ubalozi unapeleka maombi hayo US department of state,chini ya mwanasheria katika ofisi ya idara ya sheria na ushauri inapitia madai kwa undani zaidi ushahidi wa nchi unapotaka kumkamata muhusika huyo lazima maombi yawe na ushahidi wa kutosha pia idara hiyo inapitia madai hayo zaidi na kuangalia kitu kinaitwa *Dual criminality* or double criminality kwamba lazima kosa alilolifanya Mange TZ na kule liwe kosa.

Kosa alilofanya Mange la kimtandao TZ na marekani linatakiwa liwe kosa likitafsiriwa.sasa najua mnajua namna gani marekani wanaruhusu Uhuru wa maoni na kujieleza zaidi.kama hakuna Dual criminality hapo maombi ya kumkamata yanakataliwa,na kutupiliwa mbali.

JE ,MAOMBI YA TANZANIA KUMUOMBA MANGE MAREKANI ,JE MAKOSA HAYO TANZANIA NDIO MAKOSA MAREKANI? (jibu baki nalo wewe,mimi naendelea)

Tuchukulie kwa ugumu,Mange atakutwa na kosa ,katika hayo maombi (extradition demands),idara hiyo itapeleka maombi hayo kwa OIA (original request justice department of international Affairs) na idara hii itaangalia maombi haya na ushahidi kama unatosheleza au laa,baada ya kujiridhisha maombi hayo yatatumwa kwenda united States Attorney's office judicial district, katika ofisi ya mwanasheria wa ukanda anapoishi muhalifu au raia anaye takiwa.

Ofisi hii ya mwanasheria wa kanda anayoishi raia anayetakiwa itapewa mamlaka ya kumkamata mtakiwa(Mange kimambi) atakamatwa na kupelekwa mahakamani atasikilizwa juu ya shutma dhidi ya nchi inayomtaka na majaji( extradition judges)ili kuamua maombi ya nchi inayomtaka mtuhumiwa kumsafirisha au laa.

Mahakama ikijiridhisha mtu huyu kweli ametenda kosa mahakama inaandika order ya extraditability na kuandika taarifa yake inayotumwa kwa Secretary of state.ambaye ndiye mtoa maamuzi ya mwisho achukuliwe au asichukuliwe.

Ofisi hiyo ikikubali muhusika anayetakiwa anachukuliwa na kusafirishwa katika nchi anayotakiwa, ila nchi nyingi zinapata kikwazo maombi yao ya kumkamata mtu katika nchi Fulani kukataliwa kwa sababu hizi chini

1. Maombi hayo kugeuka haki za binadamu (violating the fundamentals of human right.,mfano.mange kimambi anashtumiwa kuandika mitandaoni kusema na kutukana viongozi, kwao wanaweza tafsiri huu ni Uhuru wa kujieleza ,na kutoka maoni hivyo kumkamata ni kuvunja haki za Uhuru wa kujieleza.

2. Kosa katika maombi kutokuwa na mfanano wa kosa hilo kwa nchi zote.(failing to fulfil Dual criminality) kosa la kutukana mtandaoni,kutukana viongozi pia liwe kosa marekani kuwa kutukana viongozi mtandao marekani ni kosa,

3. Aina ya adhabu inayoenda kutolewa kama ni ya kifo,au ya kutesa (death punishment or inhuman and torturing punishment),lazima maombi hayo yaseme kutokana na kosa lake ni adhabu gani inaenda kutolewa,sasa hapa Mange adhabu yake akikamatwa Mimi sijui.

4. Sifa ya kosa au uhalifu huo wa kisiasa(political nature alleged crime)

Kuna sababu nyingi hizi ni chache.

Hivyo kwa Mchakato unaweza hitimisha mwenyewe wapi maombi ya Tanzania yatapata kizuizi. Kutokana na Tafsiri ya makosa hayo marekani. Pia nitakuja elezea ,kuwa mange anaweza omba hifadhi ya kisiasa marekani inaitwa political asylum hata kuanzia sasa anaweza.

Shukran wote.


Chanzo: JamiiForums

Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.