UFAHAMU JUU YA WEBSITE HOSTING NA TOFAUTI ZAKE

Katika dunia ya leo ya mapinduzi ya Internet, websiteApplication za simu na hata mifumo ya komputa (Systems), vimekuwa ni nyenzo thabiti katika maisha ya binadamu. Wengi wetu tumekuwa tukitumia mifumo hii bila kujua jinsi inavyofanya kazi au ni wapi inapokaa. Ingawa kwa mtumiaji, hiyo si kitu muhimu, muhimu ni kuwa, inapatikana pale anapohitaji. Ila, upatikanaji huu huweza kuathiriwa na wapi mifumo inakaa. Na, kitendo cha kuwezesha mifumo hii kupatikana kutoka pale inapokaa, ndiyo tunayoiita Hosting, ama wengi wanavyoita Website Hosting. Website Hosing, imegawanyika katika makundi mengi sana, kuna Shared, VPS, Dedicated Server au Cloud Hosting.
Kwa Tanzania, watumiaji wengi hutumia aina ya shared hosting (website zaidi ya moja kuwa sehemu moja), aina hii ya hosting imekuwa na msaada kwa wengi, hii ni kwa sababu ya urahisi wake katika gharama na hata uangalizi wa mazingira ya hosting kwakuwa kama mmiliki wa Website, hauhitajiki kuchunga mazingira hayo bali kwa yule anayetoa huduma (Website Hosting Company), mfano wa watoa huduma ni Duhosting.
Ili kuweza kuelewa, hebu tuangalie aina mbalimbali za Website Hosting.

Dedicated Hosting

Aina hii ya hosting ni ile ambayo, unakuwa na umiliki wa server nzima mwenyewe. Inaweza iwe kwenye sehemu yako (kama maofisi mengi wanavyofanya) au ya kukodisha server online. Aina hii ya hosting huwa tunaifananaisha na mtu kujenga ama kukodisha ghorofa nzima.
Faida ya dedicated server ni kuwa, unakuwa na hazina (resources) za kutosha, pia spidi na usalama unakuwa wa hali ya juu kama utaweza kufanya maboresho ya kiumfumo (optimization) yanayotakiwa.
Aina hii inawafaa sana, makampuni makubwa, watu binafsi wanaotaka kuanza biashara ya Hosting au wale wanaomiliki website zenye mahitaji makubwa ya resources, kama makampuni ya betting.
Hasara zake ni kuwa, unahitaji waangalizi na wataalamu wa kutosha watakaochunga server yako. Pia, gharama zake huwa ni za juu ukilinganisha na aina nyingine za Hosting.

Virtual private Server (VPS)

Aina hii, haina utofauti sana na Dedicated Hosting, kimsingi, VPS hutokea baada ya Server moja kugawanywa (partitioned) kwa kutumia software na kuwa server zisizo bayana (Virtual) zaidi ya moja zinazojitegemea kimfumo. Hivyo, hardware zitakazotumika ni zilezile isipokuwa kwenye software, kila VPS itakuwa inajitegemea kabisa. Hivyo, VPS kuna sehemu inakuwa kama Dedicated Hosting ila kuwa sehemu inakuwa siyo.
Faida kuu ya VPS ni kuwa, ina sifa nyingi za Dedicated ikiwa kama matumizi binafsi ya hazina (dedicated resources) na hata usalama (ingawa kuna mazingira hatarishi huweza kuathiri VPS kutokea kwenye VPS nyingine iliyopo kwenye server moja).
Mfano halisi wa VPS, ni sawa na ndani ya ghorofa moja, litakatwa wings, na kila wing ikawa inajitegemea kila kitu, hivyo kwa watu wa wing ile, wanajiona kama wapo kwenye ghorofa lao wenyewe.
VPS, huwafaa sana watu wenye website zenye kutembelewa na watu wengi (high traffic), mfano, website ya habari/blogs au zile zenye mahitaji maalumu, mfano kwa website zinahitaji kipachiko (extensions) nyingi kuliko zinazopatikana katika mazingira ya kawaida. Pia, aina hii ya Website hosting inawafaa sana watu wenye kuhitaji kuanzisha huduma ya Website Hosting ila hawana mtaji mkubwa kuweza kumiliki Dedicated server, au wale wenye mahitaji maalumu ambapo hawapendelei kuchanganyika na wengine.
VPS, pia inakupa uwezo mkubwa wa kujibrand, hii ikijumuisha kutumia IP na Name Server zako mwenyewe (Dedicated IP). Na pia, unakuwa na uwezo wa kuinstall program nyingi. Ingawa kuna baadhi ya program, hauwezi kuinstall kwenye VPs kama, VPN (Virtual Private network) Server.
Tofauti ya VPS na Dedicated server huwa kwenye utendaji kazi na hata ukuaji, mfano, ukiwa na Dedicated server na ujazo (storage/space) ikawa imejaa, ni rahisi kuongeza ujazo bila kuhama, kitu ambacho si rahisi kwa VPS za kukodisha.

Unaweza kujiunga kwa kubofya HAPA
Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.