Juzi nimetumiwa msg na bae eti nimuongezee hela anunue S9+. Ikabidi nichungulie inauzwa bei gani OMG 2.3m! Yaani 2,300,000! Over a $1000! Nikafikiria huyu Bae anakaa nyumba ya kupanga, kodi vile vile nanchangia na inawezekana tunachangia wengi, kweli hana cha maana cha kufanyia hio 2.3m!
Nikafikiria haraka haraka nini unnaweza kufanya na 2.3m
1.Unaweza kununua kiwanja. Kuna kampuni zinauza viwanja vilivyopimwa 5000/sqm anaweza kupata 1000sqm kwa 5m(hii kampuni unaweza kulipa nusu halafu iliobaki kidogokidogo kwa miezi sita)
2.Unaweza kununua matofali 2300 ambayo yanamaliza nyumba ya vyumba vitatu au viwili.
3.Unnaweza kununua madirisha zaidi ya 7 ya aluminium ukamalizia nyumba yako
4.Unaweza kununua bodaboda ikakuingizia hata 20,000 kwa siku.
5.Huu ni mtaji tosha kwa biashara ya tigopesa etc
6.Unaweza kununua mabati 100 au zaidi
Kuna vitu kibao vya kufanyia hio hela kuliko kununua simu. Leo nimekamilisha uchunguzi wangu kwake hafai kuwa mke.
NB:Hii haihusu those who CAN AFFORD that phone.
Leave a Comment