FAHAMU AINA 16 ZA WATU DUNIANI

Personality Psychology ni tawi na saikolojia linahusika na sifa zinazoweza kumtofautisha mtu mmoja na mwengine kwenye saikolojia sifa hizi kuitwa traits.


Kumekuwa na nadharia tofauti zinazogawanya watu katika makundi ya mawili,manne mpaka ile ya watu kumi na sita. Nadharia inayonivutia zaidi ni ile ya 16,
Nadharia hii inagawanya watu kutokana na sifa kuu nne ambazo kila sifa inagawanyika kwenye makundi manne. Msingi mkuu wa mgawanyiko huu ni sifa zinazoamua uwezo wa kundi hilo lakini ni lazima kuzingatia uwezo huo huchochewa kutoka ndani kwa mtu mwenyewe au kutokana kwa watu waliomzunguka

Wale ambao uchochezi hutokea ndani huitwa Introvets sifa kubwa za Introvets huwa na aibu,wazito kuanzisha mazungumzo(wakimya) na hupenda kufanya vitu kwa kujitenga.
Wale ambao uchochezi hutokea kwa watu waliowazunguka huitwa Extrovets huwa hawana aibu,rahisi kuanzisha mazungumzo(wachangamfu) na hupenda kufanya kazi kwa pamoja.

Kundi la kwanza linabeba aina za watu ambao wana uwezo mkubwa wa kufiri na hutumia uwezo wao huu katika maisha yao ya kila siku pamoja na uwezo wao mkubwa kuimagine vitu na ideas.Member wa kundi hili ni introvets wawili Architects na Logicians pamoja na Extrovets wawili ambao ni Commanders na Debaters

Architects
Ni aina adimu zaidi ya watu wakiwa ni asilimia 0.8 tu ya watu wote,ni watu wakimya,wanaopenda kufanya vitu wenyewe,wanapenda kupanga kila kitu kwa usahihi na huwa na kiu kubwa ya kujua vitu vipya hii inatokana na uwezo wao mkubwa wa kuchambua vitu.Ni aina ya watu ambao huwa na uwezo wa kufikiria kwa haraka na hupenda kufanya mambo yaliyo tayari kwenye mpangilio.Ni watu wanaojiamini sana kwenye kile wanachokisimamia.
Udhaifu wao ni Arrogant(kujisikia) kutokana na sifa yao ya kujiamini sana na kuona wanajua vitu kuliko wengine,pia hupenda kujudge sana na kuchambua sana vitu kabla ya kuchukua uamuzi hii inawafanya kutokuwa implementers(watekelezaji) wazuri na tabia yao ya kupenda kuchambua sana vitu huwafanya kuwa na migogoro isiyoisha katika mahusiano ya kimapenzi haswa anapokutana na mpenzi ambae hisia ndio kipaumbele chake kwani hushindwa kutoa suport ya kihisia pale anapohitajika.

Logicians
Hii pia ni aina adimu ikiwa ni chini ya asilimia 3 tu ya watu wote.Logicians ni kundi la watu wenye uwezo mkubwa wa kufikiria kuliko kundi jengine lolote na ndio kundi linaloongoza kwa kutoa wagunduzi na wanasayansi wengi Logicians maarufu zaidi ni Albert Einstein,Bill Gates,Isaack Newton.
Sehemu yao ya ubongo inayohusika na kufikiri imejengeka vizuri kuliko ile ya hisia hii inawafanya wawe watu ambao kila kitu kwao ni lazima kwanza kilete logic ndio kiaminike au kifanyike,tabia za logicians huwashangaza wengi
kwa logician tukio la kijamii kama tamasha la muziki au harusi halina umuhimu kama kusoma kitabu au kuangalia makala ya kisayansi
kutokana na sifa yao ya kuwa na kiu isiyoisha ya kujifunza haswa vitu vilivyo kwenye mfumo wa nadharia.Si ajabu kumkuta Logician tarehe yake ya kuzaliwa ikimpita bila ya kushtuka kwani kwake birthday haina logic.
Nguvu kubwa ya logicians ni uwezo wao wa kufikiri kwa kina na kuchambua vitu na mara zote hujiuliza sana maswali kabla ya kuamua kuamini au kufata njia fulani,watu wengi wanaohoji uwepo wa Mungu wanatokea kundi hili.Ni watu ambao mara nyingi ukikaa nao wanapenda kuongelea zaidi nadharia mpya za kisayansi au teknolojia na mambo ambayo wengi huwa hawajishughulishi kuyafikria.
Udhaifu wa Logicians ni kupenda kufanya vitu kwa kujitenga ni watu ambao si rahisi kuomba ushauri.Hawapendi kufanya shughuli zinazotumia sana nguvu na za kila siku kama usafi wa nyumba n.k
Pia wanaudhaifu wa kutopenda kushindwa na kutabiri matokeo ya kila jambo hii huwafanya mipango yao mingi kuishia kichwani au kwenye makaratasi.Huwa hawana marafiki wengi hii ni kutokana na njia yao kuu ya kurelax pale wanapokuwa na stress na hobbie zao nyingi zinahitaji wawe wenyewe zaidi na kufikiria kiundani ndio huleta kurelax kwao
Kwenye mahusiano ya kimapenzi huwa ni wabunifu sana kwa kuwa wanauwezo mkubwa wa kusoma furaha ya wapenzi wao ipo wapi na udhaifu wao huwa ni kupenda kumchunguza sana mwenza wao hali inayopelekea migogoro mingi.

Commanders
Hili ni kundi la watu ambao wana vipaji vya kuzaliwa vya uongozi haswa wa biashara au makampuni 
wanauwezo mkubwa wa kusimamia kile wanachokiamini na kuongoza watu kukifikia.Huwa na uwezo mkubwa wa kufikiria na hupenda kutengeneza mfumo utakaofanya fikra zao ziishi muda mrefu
Ni aina ya watu utakao wakuta kwenye mafanikio ya makampuni mengi makubwa,wanapenda changamoto na huamini kama ukimpa muda na resources za kutosha anaweza kufikia mafanikio yoyote yale.Commander maarufu zaidi ni Muanzilishi wa kampuni ya Apple Steve Jobs na raisi wa 32 wa marekani franklin roosevelt
Kama kuna njia rahisi ya kujenga urafiki na Commander ni kuonesha uwezo wa juu wa kuchambua mambo na kuweza kuchambua malengo kama alivyo yeye,aina ya marafiki wanaopenda kufikiria maisha ya wengine huwa hawadumu na commander.Kwake cha muhimu ni kufocus kwenye mafanikio na sio maisha ya watu binafsi.
Nguvu kubwa ya Commander ni uwezo wao wakufanya vitu kwa mpangilio na kwa ukamilifu.Combination nzuri ni ile ya Logician na Commander kwani tofauti na Logician Commander ana uwezo mkubwa wa kutoa kile kilicho kwenye makaratasi ya logician kiwe kwa vitendo 
Udhaifu wa commander ni wasumbufu pale unapopanga nae jambo kwani huwa analazimisha ulifanye kama anavyopenda kufanya yeye na huwa hawana uvumilivu mtu anapokosea.Tatizo huwa kubwa anapoupeleka udhaifu huu kwenye mahusiano ya kimapenzi,Commander huwa hajali sana hisia bali huwa anaweka malengo fulani muda wote kwenye mahusiano na huweka muda maalumu wa kuyafikia,kwenye kuyafikia hayo huwa hajali sana maswala ya kihisia,commander ni aina ya mtu ambae kama mahusiano hayamletei faida ni rahisi kuachana nayo hata kama yana hisia kiasi gani.

Debaters
Hili ndi kundi la watu wenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo na kujenga hoja.Ni aina ya watu wanaopenda kufikiria kwa kupambanisha hoja,ni kundi linaloenjoy majibizano yanaohusisha kufikiria sana na kutumia akili kuliko kundi lolote.Ni watu wanaopenda utulivu na amani,hutumia kila njia kuepuka mitafaruku,debater ni wabunifu wa njia za kudumisha utulivu aidha kwenye mazingira ya kazi au jamii ikibidi hata kutengeneza uongo wenye faida.
Nguvu kubwa ya Debater ni uwezo wao wa kufikiri pengine baada ya Logicians wanafata wao na uwezo wa kuchimba taarifa mbalimbali na kuweza kutenganisha upande chanya wa taarifa na upande hasi kutokana na uwezo wao mkubwa kufikiria.Debater ni mtu ambae anahitaji point moja tu ili atengeneza kumi nyengine.Debaters maarufu ni Mark Twain na Thomas Edison
Udhaifu wa debater ni kupenda kutengeneza upande hasi wa kila kitu(kupinga kila kitu) pengine ata kusipo hitajika kupinga kabla ya kukubali kukifata au kukiamini hili pia ni kundi lenye watu wengi wanaohoji uwepo wa Mungu baada ya Logicians
Udhaifu mwengine ni kutokujali anaumiza kiasi gani hisia za wengine ili tu aonekane wazo lake limekubalika na huwa hana uvumilivu mtu anapoenda nje ya waliyoyapanga.
Udhaifu mwengine huwa hawapendi shughuli za kila siku na haswa zinazotumia nguvu.
Kwenye mahusiano Debater hufanana sana na Logicians kwa kuwa wabunifu sana wa njia za kuwaridhisha wapenzi wao na huwazid Logicians kwa kuwa Debaters hawana aibu
Udhaifu wao mkubwa ni kujaribu kuwa perfect kitu ambacho wakati mwengine huwaboa wapenzi wao.
Kundi la pili linabeba aina za watu ambao huwa na uwezo mkubwa wa kuimagine na kuiona jamii ikibadilika kitu cha ziada kwenye kundi hili ni sifa zao za kuweza kutumia hisia kama kichocheo chanya.Member wa kundi hili ni Introvets wawili ambao ni Advocate na Mediator,Pamoja na extrovets wawili protagonist na campaigner

Advocates
Ni kundi lenye watu wachache wakiwa chini ya asilimia 1 ya watu wote.Ni watu wanaozaliwa na kipaji cha kusaidia wengine kutatua matatizo yao,hakuna kitu Advocate wanapenda kama kuona wengine wamefanikiwa kwa kupitia aidha ushauri wao au jitihada zao.Ni aina ya watu wanaopenda kuelewana kwa kumfaidisha kila mmoja ni watu.Siku zote Advocate huamini matukio yanayotokea kwa sasa kwenye jamii ndio yataamua hatma ya jamii hiyo kwa wakati ujao.Japo huwa ni watu wakimya lakini Advocate huwa na uwezo mkubwa wa kuandika hotuba na kuongea mbele ya watu na kushawishi wengine.
Nguvu kubwa ya advocate ni ubunifu na uwezo mkubwa wa kushawishi wengine na kusimamia kile wanachoamini jamii inapaswa ifate kwa ustawi wake.Advocates wengi hupenda kusoma vitabu haswa vya falsafa na imani fulani.Viongozi wengi wazuri wa dini kama Mother Theresa na Martin Luther,wanasiasa wa ukombozi kama Mandela wapo kwenye kundi hili.
Udhaifu wa Advocate ni uwezo wao mdogo wa kuhimili challenges haswa kama zinatoka kwenye kundi wanaloegemea,udhaifu mwengine ni kuamua vitu wao wenyewe pasipo kushirikisha mawazo ya wengine hii ni kutokana na ukweli kwamba hawana vipaji vya asili vya uongozi lakini ni kiu yao ya kuona jamii inabadilika ndio huwafanya wawe viongozi
Linapokuja swala la mahusiano huwa wanachukulia kama jambo la muhimu sana,huwa wanachukua muda kuchagua mtu ambae ni sahihi na anaendana na yale wanayoyaamini ugumu huja pale Advocate anapopata mpenzi ambae sio mvumilivu wanaoshindwa kuvumilia mipango ya taratibu ya advocates.


Mediators
Hili ni kundi la watu wanaopenda maisha ya amani na utulivu siku zote hutafuta njia ya kupata uchanya hata kwenye mazingira yasiyochanya.Siku zote huwa ni watu wanaopenda kushawishi wengine na wengi huwa na vipaji asili vya kuwa motivational speakers.Hawa wana uwezo mkubwa wa kuwafanya watu wa imagine na huweza kutumia lugha vizuri hii huwafanya wawe watunga mashairi wazuri,waandishi na hata waigizaji wazuri.Mediator kuongelea au kujihusisha na vitu ambavyo vinavyoigawa jamii kama siasa,imani za wengine huwa sio tabia zao tofauti na Advocates.Mediators maarufu ni Alicia keys na Bob Marley
Nguvu kubwa ya mediator ni ubunifu mkubwa na uwezo wao mkubwa wa kutambua mahitaji ya wengine.Mediator hupenda kufanya kazi kwa bidii na kuwa mfano kwa wengine
Udhaifu wao mkubwa ni kuwa disapointed pale wanayoyatamani kutokea yanaposhindwa kutokea,udhaifu mwengine ni kuona wana jukumu kubwa la kuwa mfano wa kwa wengine hali inayiwafanya wawe na maisha ya kipeke yao na iwachukue muda kuendana na maisha ya wengine
Kwenye mahusiano ya kimapenzi mediator hutumia nguvu kubwa kuwa na mapenzi yaliyo perfect hii huwafanya kudemand vitu vingi kwa haraka hali inayoweza kuleta migongano.
Mediator huwa na marafiki wachache lakini walioshibana,tatizo jengine huwa ugumu wanaopata kujihusisha na shuguli za kijamii kama sherehe japo wanauwezo mkubwa wa kuwasoma watu wengine.

Protagonists
Hili ni kundi la watu wenye vipaji vya asili vya uongozi,mara nyingi huwa wanasiasa,walimu au viongozi wa makundi kama ya michezo.Kitu kikubwa kwenye maisha yao ni kuongoza maisha ya wengine.Protagonist huwa wavumilivu haswa kama mtu anafata yale wanayoyasimamia
Nguvu kubwa za Protagonist ni kuweza kuvumilia kukosolewa endapo tu malengo ya kukosolewa huko ni kutimiza kile anachokiamini.Siku zote hutafuta njia za kufurahi na kufahamika,wanajua kialisia jinsi ya kuvutia watu ukiongeza na uwezo wao mkubwa wa kuzungumza.Protagonist maarufu ni Obama na Oprah Winfrey
Protagonist huvutiwa zaidi na nafasi ya kuzungumza kuliko kuandika.Kama kuna muunganiko mzuri zaidi ni ule utakaomkutanisha advocate na protagonist.
Udhaifu wao ni kuwa disapointed pale wanayoyatamani yasipotokea,udhaifu mwengine ni hupenda kujali sana matakwa ya wengine hii hupelekea kupata ugumu kufanya maamuzi magumu kwani muda wote hupenda kupima madhara ya jambo.
Kama kuna kitu wanachokithamini basi ni uhusiano wao wa kimapenzi na moja ya nguzo zao huwa ni uvumilivu na kufanya vitu kwa utaratibu na umakini kwenye mahusiano.Udhaifu wao kwenye mahusiano ni tabia ya kujaribu kuepuka migogoto kwa njia yoyote hii huwapelekea kufake baadhi ya vitu.

Campaigners
Hii ni aina ya watu wanaopenda kuwa na furaha muda wote,huenjoy zaidi kutengeneza mahusiano na wengine.Hakuna kitu wanapenda kama kufanikisha jambo fulani la kijamii kutokea kama sherehe.
Huwa wanaona maisha kwa picha kubwa yenye mafumbo mengi ambapo kufumbua mafumbo hayo inahitaji kujihusisha na watu kwa kiwango kikubwa hii huwafanya kuwa na kiu kubwa ya kujifunza vitu vipya
Nguvu kubwa ya Campaigner ni kupenda kujua vitu vipya na kuweza kubadilika badilika kutokana na mazingira na mahitaji ya watu.Pia wanauwezo mkubwa wa kuwasiliana na wengine
Udhaifu wao ni waoga wakuanzisha kitu na huwa wanaudhaifu wa kusimamia jambo moja kwa muda mrefu ni aina ya watu unaokuta na wanamipango mingi lakini yote haioneshi kufanikiwa
Udhaifu mwengine ni kupata msongo wa mawazo kirahisi hii inatokana na attachment wanayojiwekea kwa watu wengine
Huwa wanafanya vizuri kwenye mahusiano ya kimapenzi haswa wanapopata mpenzi ambae hisia ni kipaumbele chake kwani siku zote huwa wanajali nini mpenzi wake anahitaji lakini kwa upande mwengine Campaigner huishi maisha ya stress kwenye mahusiano kutokana na kuwa mdhaifu wa kuumizwa na vitu vidogo vidogo.

Kundi la tatu linahusisha watu wenye uwezo mkubwa wa kufanya vitu kwa vitendo pamoja na uwezo wao wa kufanya maamuzi kwa kujudge mapokeo ya watu.Members wa kundi hili ni introvets wawili Logisticians na defenders pamoja na extrovets wawili Executives na Consuls

Logisticians
Hili ni kundi na la watu wanaominika kuwa na watu wengi likiwa na asilimia 13 ya watu wote.Linabeba watu wanaopenda kuaminika na kujishugulisha hii inawafanya wafanye kazi zaidi jeshini,kampuni za ulinzi na mamlaka mbalimbali za sheria kama za rushwa au madawa ya kuevya.Ni watu wanaopenda kuwajibika kwa vitendo vyao na kupata sifa kwa kile walichokifanya
Logisticians huwa ni wawazi kwenye vitendo vyao na huwa wagumu kupindishwa na chochote.Pia ni watu wanaopenda kutii uongozi unao waongoza
Udhaifu wao ni usumbufu pale wanapotaka lao litimie na huwa niwagumu kukubali wazo jipya lisiloingia kwenye akili yao au lisiloendana na maagizo aliyopewa.Udhaifu mwengine ni tabia yao ya kupenda kujilaumu wao wenyewe wakati mwengine pasipo ata sababu maalumu
Kwenye mahusiano ya kimapenzi logistician hupenda zaidi mahusiano ambayo yanampa nafasi ya kuonesha jinsi anavyoweza kuendesha maisha ya mpenzi wake,hii ni aina ya mtu ambae anapenda kuishi karibu na mpenzi wake na hupenda kujenga familia mapema katika maisha.Tatizo kubwa la logistician kwenye mahusiano ni tabia ya kupenda kuforce vitu vitokee kwa haraka.

Defenders
Hili ni kundi la watu wenye uwezo mkubwa wa kuchambua mambo nakupenda kusimamia upande mmoja wanaouamini.Ni watu wanaopenda kufanya vitu kwa wakati.Changamoto yao kubwa ni kile wanachokifanya kuweza kutambulika na kuheshimika hii inatokana na ukweli kwamba defenders huwa hawapendi kujisifia au kulazimisha mtu aone mchango wake kwenye jambo fulani.
Defenders ni watu wenye aibu japo huwa hawachoshwi sana na kujihusisha na shughuli za kijamii.Defenders hupenda kusuport wengine na huwa wavumilivu pale inapohitajika,wanapenda kujishughulisha na huwa sio vigeugeu
Udhaifu wa defender ni unyenyekevu wao uliopitiliza na aibu,ni aina ya watu ambao kwenye hatua nyingi za kimaisha huwa wanahitaji kujihusisha na jamii direct hivyo sifa yao ya iabu huwaangusha
Kwenye mahusiano ya kimapenzi Defenders hutumia nguvu kubwa kulinda penzi lao katika kila hali.Udhaifu mkubwa na defender kwenye mahusiano ni pale wanayoyafanya yasipothaminiwa na tabia yao ya kuepuka malumbano hali inayowafanya wakati mwengine kufake

Executives
Ni kundi linalobeba watu wanaopenda kuthamini uwazi na utu,watu wa kundi hili huthaminiwa kwa ushauri wao na muongozo na hupenda kutoa njia kwa watu pale mambo yanapokuw mabaya.
Ni watu wenye vipaji vya asili vya kusimamia sheria zinazoongoza jamii na usawa kwa kila mtu ni watu wanaopenda kufanya kazi na watu wengine kutimiza lengo fulani
Changamoto yao kubwa ni uwezo wao mdogo wa kujua kama kweli kila mtun anafata yale wanayoyasimamia au vyenginevyo
Nguvu kubwa ya executive ni uwezo wao wa kusimamia mambo fulani mpaka kuhakikisha yanafanikiwa pia huwa wawazi na wasioyumbishwa.Executive huwa wavumilivu na hupenda kuwaagiza wengine nini cha kufanya
Udhaifu wao mkubwa ni usumbufu pale wanapoona waliyoaagiza hayaendi kwa muda,udhaifu wao mwengine ni uwezo wao mdogo wa kuhimili hali zisizo za kawaida
Udhaifu mwengine ni tabia yao ya kufocus sana kwenye jinsi jamii inavyowachukulia hali inayowafanya wakati mwengine kufake maisha.
Kwenye mahusiano ya kimapenzi huwa wanapenda mahusiano yanayojengwa kwenye uwazi na kutokupindapinda.Kutoka mwanzo huwa wanapenda kuweka wazi jinsi walivyo na yale wanayotaka kwenye mapenzi.Tatizo lao kubwa huwa ni kwenye maswala ya kihisia kwani huwa wanayachukulia maswwala ya kihisia sawa sawa na maswala mengine yoyote yale hii hupunguza affection kwa wapenzi wao

Consuls
Hili linabeba kundi la watu wanaopenda kusuport marafiki na watu wanaowapenda,hakuna kinachomfurahisha consul kama kufaya wengine wawe na furaha.Consul huwa wanavipaji asili vya jinsi ya kuhusiana na wengine(kuchukua attention) na jinsi ya kuwafanya wengine wawapende.Mara nyingi hupenda kufanya kazi zinazowakutanisha na watu kama marketing,secretary,ma nurse na walimu haswa wa watoto wadogo.
Kudiscuss siasa au sayansi sio vitu ambavyo consul wanapenda,wao hupenda zaidi kudiscuss aina mpya za mitindo,muonekano wao na watu wengine.Kufanya shughuli za kila siku na Umbea ni kama mkate na siagi kwa consul.
Consul wanaenjoy kufanya shughuli za kila siku na haswa kama hizo shughuli zinawafurahisha wengine,sio vigeugeu na ni watu wasiobadilisha kirahisi misimamo yao kiimani,kazi au kundi.Kwenye kikundi consul ata hakikisha anajitoa kwa hali na mali kufikia malengo.Consul huwa wanajali sana hisia za wengine.
Udhaifu wao mkubwa ni kuishi kwa wasiwasi wa jinsi gani jamii inawachukulia hii huwafanya kushindwa kufanya baadhi ya vitu wakiogopa jamii kuwachukia.Pia huwa wanaathiriwa sana na kukosolewa vitu kama maisha yao au imani zao hii inaenda mpaka kwenye mahusiano yao moja ya makosa makubwa unayoweza kumfanyia consul ni kama utakuwa unamkosoa sana.
Vitu vinavyowapa stress sana ni jamii kuwanyooshea vidole na kile wanachokifanya kutokuthaminiwa.

Kundi la nne linahusisha aina ya watu wenye uwezo mkubwa kugundua fursa za mahitaji ya jamii na uwezo wao wakufanya vitu kwa vitendo.Kundi hili lina introvets wawili Virtuosos na Adventurers,pamoja na extrovets wawili entreprenuers na entertainers

Virtuosos
Hili ni kundi la watu wanaozaliwa na vipaji vya asili vya kutumia mikono yao na macho yao kuyabadilisha mazingira yao au dunia kwa ujumla.Mara nyingi hujihusisha na ufundi kwani hupata urahisi wa kutumia vipaji na kuweza kufanya shughuli mbalimbali zinazohitaji ujuzi wa mikono.Mara nyingi huwa ni maengineer wazuri wanaenjoy kuona kitu kikiwa bora zaidi ya mwanzo.Tangu utotoni huchukuliwa kama watundu na hawaribifu kwa tabia zao za kujaribu jaribu vitu kama kufungua redio,kuchezea vitu vya umeme n.k Virtuoso hutengeneza combination nzuri na commanders 
Virtuoso hupata shida kutambua hisia fulani za mtu zinamaana gani hii huwafanya kupenda kupingwa kuliko mtu kutokumuelewa mtu anachomaanisha au kupewa wazo jipya,kwao hakuna kitu kinaboa kama kila mtu kukubali mawazo yake.
Wanauwezo mkubwa wa kusimamia yale wanayoaamini kwa gharama yoyote ukijumlisha uwezo wao mkubwa wa ubunifu na kujua kipi kina umuhimu wa kuanza kabla ya kipi
Udhaifu wao ni usumbufu pale mambo yasipoenda kwa mda,chengine ni mood yao kubadilika kirahisi na tabia yao ya kutopenda kushare matatizo yao
Kuwa kwenye mahusiano na virtuoso ni kitu kigumu kidogo kwa twani tabia zao hubadilika badilka wakati mwengine za kuvutia na wakati mwengine za kuchukiza.Hakuna kitu kinawafurahisha virtuoso kama kupewa nafasi na muda wa kutosha kufanya vitu vyake kwa uhuru na mpenzi wake.

Adventurers
Hii ni aina ya watu wanaopenda kuenjoy maisha kwa gharama yoyote ile huwa ni aina ya watu wanaopenda kueleweka,kufanya vitu vyao wao wenyewe na kujali faida wanazopata wao wenyewe.Kwao maisha ya wengine si muhimu sana ilimradi ya kwao yanaenda vizuri.
Hupenda kujifunza vitu vipya na kuwa wabunifu wa vitu vipya kwenye jamii
Udhaifu wa adventurer huwa hawatabiriki hii ni kutokana na tabia yao ya kupenda kuenjoy maisha yao kwa wakati uliopo na sio kutumia nguvu kubwa kujenga yajayo,ni rahisi kukumbwa na msongo wa mawazo na ni rahisi kuwa addicted na tabia fulani.Udhaifu wao mwengine ni kupenda ushindani hata kwa vitu vidogo.Rafiki mzuri zaidi kwao ni yule anaependa kujishusha na anaeweza kujitolea kwa ajili yao haswa pale wanapohitaji,watu wa kundi la consul ndio huweza kuendana na aina hii ya watu
Kwenye mahusiano ya mapenzi huwapa tabu wapenzi wao kujua haswa wanapendelea vitu gani.Faida moja ni huwa wana hisia sana huwa wanapenda kusikiliza kuliko kutoa maoni yao na mara nyingi hupenda wapenzi wao ndio wawaongoze kwenye mambo mengi haswa mipango ya muda mrefu

Entrepreneurs
Ni aina ya watu wanaopenda kuenjoy maisha na haswa kuwa sehemu ya wengine kuenjoy na wanapenda kuzungumziwa na wengine(Attention).Kudiscus sayansi au maswala ya siasa za dunia sio sehemu ya maisha yao.Wanapenda mazungumzo yanayodiscus watu,yanayofurahisha na utani.
Entrepreneurs huwa hawapendi kuishi kwenye mazingira yaliyopangiliwa kwa kila kitu na yanayomlazimisha kufata utaratibu kama shule kwani kufata utaratibu kila siku huwaboa kwao utaratibu umeekwa ili uvunjwe.Chengine kinachowafanya wasipende mazingira kama shule ni tabia yao ya kupenda zaidi kuona kitu kikifanyika kwa vitendo kuliko nadharia za vitabu.
Huweza kutumia uwezo wao mkubwa wa kuhusiana na jamii kuweza kutambua fursa na kupatia faida ya vitu kama biashara n.k
Combination nzuri ni ile ya Campaigner na Entreprenuer
Hupenda kufanya kazi zisizowabana sana au kuwaeka sehemu moja kwa muda mrefu
Sehemu ya ubongo wao yenye nguvu zaidi ni inayocontrol hisia hii inawafanya wawe na udhaifu mkubwa wa kuamua kwa kufikiria,ni kwamba hucontroliwa zaidi na hisia huwa mara nyingi hawapimi hasara za matendo yao ikiwa tu matakwa yao ya kihisia yatatimia hii inaenda mpaka kwenye mahusiano yao ya kimapenzi ambapo kama watapata mtu anaetokea kwenye kundi la watu wasiojali sana hisia huwa ni rahisi kusaliti.Kama kuna aina ya watu ambao huwa na idadi kubwa ya wapenzi ni hii.
Pia hupenda wapenzi wachangamfu na watakao wafanya wa enjoy maisha.

Entertainers
Hili ni kundi la watu ambao kwao aibu haipo kabisa,ni aina ya watu ambao wataanza kujitokeza kucheza mziki kwenye sherehe.
kwao maisha yanapaswa kuishi kwa kuyaenjoy katika kwa kila nukta.Wanapenda kuongelewa na utani mwingi mara nyingi kama wakiwa wasanii maarufu na waigizaji hupenda watu kuwaongelea zaidi maisha yao binafsi zaidi kuliko vipaji vyao.
Entertainers wana kipaji asili cha jinsi ya kujenga urafiki kirahisi na kuzoeana na watu wengi kadri iwezekanavyo.
Huwa na uwezo wa kugundua fursa zilizowazunguka lakini niwaoga wa kujaribu tofauti na entrepreneurs.Entertainers hupenda kujenga mtandao mkubwa wa kufahamiana na watu kwani kwao ili waenjoy moments za maisha ni lazima wahakikishe wanazienjoy moments katika level ya juu iwezekanavyo.
Hupenda kufanya kazi zitakazo wakutanisha na watu wengi au zitakazo wafanya waridhishe matakwa ya wengine kwa urahisi.
Udhaifu wao ni kitendo cha kuepuka sana migogoro hii huwafanya wafake maisha,udhaifu mwengine ni rahisi kuwa bored japo ndio kundi linaloweza kubadilisha mood zao kwa haraka zaidi kuliko kundi lolote kwa kuwa sehemu yao ya ubongo inayocontrol hisia kuwa na utendaji mzuri na wa kasi
Pia wana udhaifu wa kutake risk za kitabia ambapo kinyume na watu wa kundi la kwanza kama logicians kwao ili kitu kifanyike lazima kilete kwanza faida kihisia mambo ya logic baadae hii hufanya uhusiano au urafiki unaokutanisha aina hizi za watu kuwa mgumu
Udhaifu mwengine tabia yao hii huwafanya kuwa na tabia ya kupanga mipango hafifu ya muda mrefu na kushindwa kusimamia jambo moja kwa muda mrefu(kufocus)
Kwenye mahusiano ya mapenzi Entertainer wanapenda mahusiano yatakayo wafanya wa enjoy maisha na sio kitu serious sana kwao, kwa watu aina hii mahusiano sio zaidi kwa ajli ya kujenga maisha kwani wanaamini wana mtandao mkubwa wa kujenga maisha yao na mapenzi lazima yatenganishe na hilo wakipata wapenzi wa aina yao au adventurers huwa ngumu kupanga mipango ya muda mrefu. Labda wapate wapenzi wanaoweza kuwashape haswa kutoka kundi la consuls, defenders, executives au logisticians.

Image result for animated download now gif
Powered by Blogger.