MNARA WA BABELI NA HISTORIA YA KUTISHA
Historia ya mnara wa Babeli inaelezwa kwa undani kwenye biblia katika kitabu cha Mwanzo 11 katika mistari michache tu.Hii ni stori fupi tu ya mnara wa babeli unaweza kusoma kwa undani katika mistari au maandiko hapo chini ili kujua zaidi juu ya babeli na maana yake katika biblia.
Kizazi cha Nuhu kilikuwa kinaishi katika Mesopotamia ndani ya Babeli na kuchagua kuishi katika nchi ya Shina.Kizazi chao kikazidi kukuwa huku wakiwa wanongea lugha moja wote.Mda ulivyozidi kwenda watu wa Babeli wakaaamua kujenga mnara mkubwa kama alama ya nchi yao na kujionesha kwa mataifa mengine ukuu wa nchi yao ya Babeli.Watu wa babeli walitaka kujenga mnala ambao uneweza kufika mpaka mbinguni,ili wawe kama mungu na wasimuhitaji tena mungu kwenye maisha yao ndipo hapo wakaanza ujenzi wa mnara huo na kuuita mnara wa babeli.
Babeli ni mji maarufu sana ndani ya mesopotamia ambako kwa miaka ya sasa mji huu unapatikana maili 59 iraq kusini magharibi mwa Baghdad ambao ni mji mkuu wa Iraq. Jina hili linatokana na lugha ya ki-akkadian (Bav-ill) lenye maana mlango wa mungu 'Gate of God'. Historia ya biblia inatuonesha maeneo mbalimbali ya mabadiliko ya dunia mfano Uumbaji,anguko na gharika la NUHU.Kwa kufuatilia mfululizo mzuri wa matkio ya kibiblia ambayo yalishawahi kutokea na ni ya kweli tunaweza tukaelewa asili ya maisha yetu na kuachana na mambo ya EVOLUTION OF MAN.Babeli ndiyo ulikuwa mwanzo wa mgawanyo wa mataifa na mkanganyko w lugha ulimwenguni.
Baada ya Nuhu na familia yake kushuka kwenye safina katika milima ya arafati, Mungu aliwaagiza waende kuzaana na kutawanyika mbele ya uso wa nchi. (\mwanzo9:1) ,wao wakaamua kuishi Babeli nchi iliyokuwa chini ya Nimrodi (Mpinga kristo) ambapo hapo ndipo ujenzi wa mnara wa babeli ulipoanzia. (Baadae tutaona ni kwanini Nimrodi alikuwa mpinga kristo). Mnara huu wa Babeli ndio uliokuja kuwa makutano ya kuabudia miungu na sio Mungu muumbaji.
KWANINI MUNGU ALIAMUA KUANGAMIZA BABELI?
Katika utawala wa Nimrodi,miaka mingi baada ya uumbaji kukamilika,Ndipo ujenzi wa mnara wa babeli ulipoanza,Ikumbukwe mpaka muda huu nchi ilikuwa sehemu moja.Baada ya gharika kutokea na Nuhu na familia yake kusalimika,ulimwengu mzima ulikuwa sehemu moja kwa sababu dunia/nchi haikuwa na watu wengi na ndio maan Mungu alimwagiza Nuhu baada ya gharika kuisha kuwa waende wakaijaze nchi.
Hapo ndipo Nimrodi na wenzake walipoamua kujenga mnara mkubwa sana kwa malengo makubwa mawili.
1. Kujitafutia jina wao wenyewe juu ya nchi
2. Kufika mbinguni
Nimrodi akaanza kujenga mnara ambao ulikuwa mkubwa sana mpaka hapo mungu aliposhuka chni na kuamua kuuangamiza huo mnara kwa kuwachafulia lugha zao.
Mungu hakuiangamiza babeli kwa sababu aliwaogopa wanadamu au labda aliona kuwa wanadamu wanaweza kufika mbinguni,hapana.Dunia sasa hivi ina maghorofa makubwa sana hata tunaona ndege zikienda hewani lakini hakuna ambayo imeshawahi kufika mbinguni ambako mungu yupo,kwa hiyo mungu hakuwahofia wanadamu kabisa ila kulikuwa na sababu za msingi zilizofanya mungu afanye vile.
Mungu hakupendezwa na kiburi na kutokutii kwa wanadamu.Ikumbukwe kuwa dhambii hii hii ya kiburi ndiyo kwanza ilimuangusha shetani kutoka mbingu mpaka nchi,pia dhambi hiyo hiyo ilimuangusha adamu ndani ya Edeni na dhambi hiyo hiyo iliangusha babeli kuu ya Nemrodi. Watu wa babeli walitaka wakae sehemu moja kinyume na matakwa ya mungu.Ikumbukwe mungu alimuagiza Nuhu waende wakatawanyike mbele ya uso wa nchi,lakini wao wakaamua kufanya kinyume na amri ya mungu ili wajitwalie utukufu wao wenyewe (KIBURI). Dhambi kubwa iliyofanya mungu awachafulie usemi wao ilikuwa "Na tujifanyie jina wenyewe" Je, wakati huo kulikuwa nchi ambayo walikuwa wanataka kushindana nayo?je walitaka nani awasifu?kulikuwa na nchi ya jirani? ila walikuwa wanashindana na Mungu mwenyewe.
Nimrodi alikuwa na makundi matatu
1. Kundi la kwanza lilikuwa kwa ajiri ya kumuua mungu
2. Kundi la pili walikuwa na kazi ya kutengeneza mishalie kwa ajiri ya kumuua mungu
3. Kundi la mwisho kwa ajiri ya ujenzi wa babeli
Tembelea (skiba 2012) kwa mapitia..
Hapo ndipo utakapogundua kuwa Nimrodi alitaka kwenda kukaa kwenye kiti cha enzi cha mungu. Hayo yote ndiyo yaliyomchukiza mungu na kuamua kuwachafulia usemi wao ili wapate kujifunza na kuwalazimisha kugawanyika mbele ya uso wa mungu
HII INAENDA SAMBAMBA KABISA NA ANGUKO LA SHETANI KWA KUTAKA KUWA KWENYE KITI CHA ENZI CHA MUNGU.
Leave a Comment