ZITAMBUE SIKU HATARI ZA KUPATA MIMBA


Ili kufahamu vizuri ni siku zipi ni hatari kwa mwanamke kupata mimba,ufahamu thabiti kuhusu mzunguko wa hedhi[menstrual cycle) ni jambo la muhimu sana.
Kwa wastani,mzunguko wa hedhi ni siku 28.

Mzunguko wa hedhi unaanza kuhesabiwa kuanzia siku ya kwanza mwanamke anapoanza ku bleed (label it as day one).

MZUNGUKO WA HEDHI WA KAWAIDA UNA SIFA MADHUBUTI [CHARACTERISTICS OF NORMAL MENSTRUAL PERIOD]

1.IDADI YA SIKU KATIKA MZUNGUKO MMOJA (cycle length).
Kwa kawaida idadi ya siku katika mzunguko ambazo huhesabika kama ni mzunguko wa kawaida ni siku 21 hadi 35 (ambapo hapo ndipo unapata wastani wa siku 28 yaani [(21+35)÷2]. Kwahiyo ndugu msomaji usikariri kuwa mzunguko wa kila mwanamke una siku 28,hiyo ni big no.wengine wana siku 27,wengine 25,wengine 35,wengine 29.

2.SIFA YA PILI NI UWIANO WA IDADI YA SIKU ZA MZUNGUKO KATI YA MZUNGUKO MMOJA NA MWINGINE(REGULAR VS IRREGULAR CYCLES).
Hii ni miongoni mwa changamoto kubwa sana katika suala zima la ngono kwani inaweza kuwa vigumu kuzitambua siku hatarishi kwa mwanamke kupata mimba.
Ili tuseme mwanamke anamizunguko ya hedhi iliyo sawa[regular cycles],idadi ya siku za mizunguko ya hedhi isitofautiane kwa zaidi ya WIKI MOJA[7 days].

Kwa mfano,kama mwezi wa kwanza aliona siku zake baada ya siku 28,mwezi wapili akaona baada ya siku 30,mwezi wa tatu akaona baada ya siku 35 na wanne akaona baada ya siku 21,bado mzunguko wake uko kwenye uwiano mzuri[regular cycle] kwasababu mzunguko mmoja na mwingine haujatofautiana kwa zaidi ya siku 7.

Usikariri kuwa siku za mzunguko kwa kila mwanamke ni siku 28,hiyo ni big NO.Hiyo 28 ni wastani tu. Wengine wana bleed kila baada ya siku 21,wengine25 wengine,29,wengine 35 na bado tunasema mizunguko yao bado ni regular [uwiano sahihi].

Pia tambua ya kuwa si lazima idadi ya siku katika mzunguko mmoja ilingane na mzunguko mwingine kwa mwanamke huyohuyo,kwa mfano usitarajie kuwa kama mwezi march ame bleed baada ya siku 28 na mwezi april pia ata bleed baada ya siku 28,sio lazima iwe hivyo lakini pia inaweza tokea.

Kwa mfano mwanamke mzunguko huu anaweza kuona siku zake baada ya siku 28,mzunguko unaofuata baada ya siku 27,mzunguko mwingine baada ya siku 30,mzunguko mwingine baada ya siku 29,mzunguko mwingine baada ya siku 25 na bado yuko kwenye uwiano sawa(tofauti si zaidi ya siku 7).

3.IDADI YA SIKU ZA KUBLEED[MENSTRUAL PERIOD]

Usichanganye kati ya menstrual period na menstrual cycle,hivi ni vitu viwili tofauti kabisa.

Siku ya kwanza ya kubleed ndo siku tunayoanza kuhesabu mzunguko wa hedhi[day one],sio siku ya kumaliza ku bleed. Kwa kawaida idadi ya siku za ku bleed ni kati ya siku 3 hadi 7,kila mwanamke ana idadi yake kati ya hizo.

4. Sifa ya mwisho ya mzunguko wa hedhi ni WINGI WA DAMU inayotoka wakati wa hedhi[amount of menstrual blood],ambapo mwanamke anaweza ku bleed kawaida [normal bleeding] au ku bleed sana[heavy bleeding].


ILI KUZIFAHAMU VIZURI SIKU HATARI KWA MWANAMKE KUPATA MIMBA HEBU TUANGALIE KIDOGO JINSI MAYAI YANAVYOKOMAA NA KISHA KUTOLEWA KWENYE OVARY.

Tufahamu mzunguko wa ovary (ovarian cycle).
Mzunguko wa ovary [ovarian cycle) ndio unaoleta mabadiliko katika mfuko wa uzazi (menstrual cycle).
Mzunguko wa ovary una hatua zifuatazo
Follicular phase, ovulation na luteal phase.

1.FOLLICULAR PHASE: Sehemu hii ya mzunguko huanza siku ya kwanza ya mwanamke ku bleed mpaka yai linapokuwa limekomaa[graafian follicle)
Mayai ya mwanamke huanza kutengenezwa wakati akiwa tumboni mwa mama.

Mpaka kufikia balehe [puberty],mwanamke anakuwa na mayai yapatayo 400,000 ndani ya ovary,mayai haya huwa katika hatua ya uchanga[primary oocyte].

2.OVULATION; katika hatua hii ya mzunguko wa ovary,yai lililokomaa[graafian follicle] hutoka kwenye ovary na kuingia kwenye mirija ya fallopian.

Sasa tutaitambuaje siku ya yai kutoka[ovulation]?.
Kiuhalisia ni ngumu kujua siku halisi yai lilipotolewa lakini tunaweza kuzitambua siku nyeti ambazo zitatupa nafasi kubwa ya kutokulikosa yai ndani ya siku hizo.Fuatilia hapo chini.

3.LUTEAL PHASE: hii ni sehemu ya mzunguko wa ovary ambayo huanza baada ya yai kutoka[ovulation] na kuishia kabla ya kuanza ku bleed[mwanzo wa mzunguko mwingine).

ZINGATIA HAPA, idadi ya siku kati ya ovarian cycle na menstrual cycle ni sawa[mfano,28,30,35,25).
Idadi ya siku katika luteal phase ni sawa kwa mizunguko yote na ni siku 14.

ANGALIA HESABU HII RAHISI
Folicular phase +luteal phase =Idadi ya siku katika mzunguko[the cycle length).

Lakini tayari tumeshajua luteal phase ni constant,haibadiliki,[ni siku 14 katika kila mzunguko].ovulation phase hapo iondoe maana ovulation hutokea masaa machache tu. Sasa ili kuipata siku ya ovulation,tunachukua idadi ya siku katika mzunguko mmoja - idadi ya siku katika luteal phase,ambayo haibadiliki[14 days].

Kwa mfano kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 28,kuipata siku ya ovulation tunachukua 28-14 tunapata 14,kwahiyo kutoka siku ya kwanza mwanamke alipoanza kubleed ni siku ya 14 ndipo yai linakuwa tayari kurutubishwa.

Kwa mwenye mzunguko wa siku 30,tunachukua 30-14(luteal phase)=16,kwa hiyo mwanamke mwenye mzunguko wa siku 30,ovulation inauwezekano mkubwa wakutokea siku ya 16 na si ya 14(kuwa makini hapo).

Yule mwenye mzunguko wa siku 35,ovulation day ni 35-14 = 21,kwa hiyo kwa mwanamke mwenye mzunguko wa siku 35,ovulation ina nafasi kubwa ya kutokea siku ya 21 na si ya 14.

Sasa baada ya kuijua siku ya ovulation lazima uwe makini na siku zinazokaribiana na siku ya ovulation kwani nazo ni siku hatari pia.

KWANINI?

Mbegu ya kiume inauwezo wa kuwa hai hadi masaa 48 (2 days) tangu shahawa zimwagwe[ejaculation] na yai lina uwezo wa kuwa hai hadi masaa 24[one day] tangu lilipotoka kwenye ovary.

Kwaiyo kama mwanaume akijamiiana na mwanamke siku mbili kabla ya yai kutolewa kwenye ovary, mbegu inaweza kuwa hai bado na kutungisha mimba endapo yai litatolewa ndani ya siku mbili zijazo kwa mfano kama siku ya ovulation ya mwanamke ni siku ya 14, mwanamke akijamiiana na mwanaume siku ya 12, uwezekano wa kupata mimba ni mkubwa. Kadhalika kama mwanamke ametoa yai siku ya 14 kisha akajamiiana ndani ya masaa 24 mbele, pia anaweza kupata mimba kwasababu kipindi mbegu zinamwagwa zinaweza kulikuta yai bado lipo hai na kutungisha mimba.

Kwa ufupi,ni siku tatu tu ndizo hatarishi sana kwa mwanamke kupata mimba,yaani,siku mbili kabla ya ovulation na ndani ya masaa 24 baada ya ovulation [narrow but dangerous window].

Kwa kuongezea,kipindi cha ovulation mwanamke anapata nyege kali sana kwasababu ni kipindi ambacho kuna homoni fulani[androgens] ambazo huchochea nyege huzalishwa kwa wingi. Pia kipindi hicho cha ovulation au karibia ovulation joto la mwili la mwanamke hupanda,anajihisi mwili kuchemka tofauti kidogo na ilivyo kawaida yake.

SASA BASI KWA KUWA NIMESEMA HATUWEZI KUWA NA UHAKIKA WA 100% WA SIKU YA OVULATION NDO MAANA HUWA TUNATUMIA KANUNI YA KUEPUKA NGONO KWA KIPINDI CHA WIKI NZIMA[7 DAYS] AMBAZO NI SIKU ZILIZO KARIBU SANA NA SIKU YA OVULATION KWA WALE WANAOTUMIA CALENDER METHOD.

Mfano,kama una mzunguko wa siku 30,kuipata siku ya ovulation chukua 30- 14=16,kwa hiyo siku ya ovulation ni ya 16 tangia ulipoanza kuona damu siku ya kwanza.sasa kama ni siku ya 16,ondoa siku nne kabla ya hiyo siku ya ovulation.kwahiyo kuanzia siku ya 12 hapo, acha ngono.
Pia jumlisha siku 3 mbele,ambapo mwanamke atatakiwa kuanza ngono kuanzia siku ya 19 huko ili kuepuka mimba..!

NI HAYO TU WADAU

SOURCES: 1.WILLIAM'S OBSTETRICS 25 EDITION
2.GYNECOLOGY BY TEN TEACHERS, 19 EDITION.
3.DUTTA, OBSTETRICS AND GYNECOLOGY.

Image result for animated download now gif
Powered by Blogger.