JIFUNZE JINSI YA KUTAFSIRI NDOTO ULIYOOTA

Katika Uislamu tumeambiwa Ndoto ni sehemu ya unabii tulioachiwa, pia uislamu unaeleza aina kuu mbili za ndoto yaani Ndoto zinazotokana na shetani na ndoto inayotoka kwa mwenyezi mungu. Pia Uislamu umeeleza ndoto ya kweli uotwa muda gani (Mfano amesema bwana Mtume, ndoto yeyote atakayeota muumini kabla ya swala ya alfajiri, ndoto hiyo ni ya kweli), kwa ufupi ndoto ya kweli ni ile mtu anayeota usiku wa manane akiwa hana msongamano wa mawazo na wala huna janaba la hawala.


Uislamu umesema kuwa kama mmoja wenu ameota ndoto nzuri basi amfuate mmoja wenu anayejua na amweleze ili apate maana yake. Kama uislamu umeelezea vizuri kuhusu ndoto Je ndoto hutafsiriwaje?. Kwa ufupi kuna watu wengi wanadai wana uwezo wa kutafsiri ndoto, ukweli ni kuwa utafsiri wa ndoto ni ngumu sana na hakuna mtu anyejua kutafsiri ndoto zote ukiondoa manabii ambao kwa sasa hawapo tena. Wengi wanaishia kudanganya maana halisi ya ndoto, kumbuka uislamu umesema, "KAMA MMOJA WENU AKIOTA NDOTO CHAFU NA MBAYA BASI ASIITANGAZE, MAANA NDOTO HIZO ZIMETOKA KWA SHETANI".

Leo nitawafundisha jinsi ya kutafsiri ndoto ili msije mkadanganywa na mtu lakini tafsiri nitakayowapa ni Based on Islam na sio dini nyingine, japokuwa baadhi ya ndoto inabeba maana sawa kwa muislamu na siye muislamu. Kama wanavyotafsiri wanazuoni wengine..

Ukiota ndoto yoyote katika wakati ulioelezwa basi angalia hiyo ndoto kama inafanana na Aya yeyote ya Kuran anu Hadith Yeyote ya Bwana Mtume PBUH. Hiyo itakuwa ndio maana yake:-

Mfano 1: Umeota umetumbukizwa kwenye Kisima, tafsiri yake ni surat Yusuf... Yaani Ndugu zako wanataka kukutendea uadui, lakini kwa uwezo wa Mwenyezi mungu hawatafanikiwa wanavyotaka na utakuja kuwa na uwezo wa mali na mamlaka kuliko wao.

Mfano 2: Umeota ndege amekudondoshea jiwe kichwani, Tafsiri yake Surat fil... Unaonywa kuwa unafanya yaliyovuka mipaka hivyo utaangamia.

Mfano 3: Umeota Ndege anaokuambia kitu, Tafsiri yake ni surat Naml.. Habari anayokuambia ni ya kweli hivyo unatakiwa uifanyie kazi haraka.

Mfano wa nne: Umeota unakurupuka na ukaambiwa kiama!, watu wengi wanakwenda wasipopajua, Tafsiri yake ni kuwa unapewa Onyo kuna jambo linalomchukiza Mungu unalifanya acha mara moja. kumbuka pale allah aliposema kuwaambia waovu "Hakuna wanachokisubiri ila ni kiama ambacho kitawakuta Ghafla". Inshaallah nisiwaboe kusoma ila hivyo ndivyo jinsi ya kutafsiri ndoto.... Kesho nitawaelezea maana ya kuota manabii... Ingawa kizazi cha sasa imekuwa ngumu sana mtu kuota nabiii yeyote yule..

Image result for animated download now gif
Powered by Blogger.