WAFAHAMU WAARABU / USIYOFAHAMU KUHUSU WAARABU

Leo tupate kujua kidogo kuhusiana na hawa watu tunaowaita "Waarabu"...Nimepitia pitia kidogo nchi zao na pia kusoma vitabu vyao vinavyoelezea maisha yao...haya yafuatayo ndio niliopata kuyafahamu kutoka kwa "waarabu":-


1. Neno "uarabu"-"arab" ni neno linalowakilisha asili / tamaduni / culture na sio rangi kama wengi tujuavyo.

2. Duniani kuna nchi 22 za kiarabu,yani waishipo waarabu nazo ni- Lebanon, Syria, Morocco, misri, Tunisia, Iran, iraq, Jordan, kuwait, Qatar, Saudi arabia, Somalia, Djibouti, Comoro, Sudan, Palestina, Mauritania, Algeria, Oman, UAE, Bahrain na Yemen.

3. Waarabu wote sio Waislamu,Na Waislamu wote sio waarabu..ingawa kundi kubwa la waarabu ni waislamu,wachache sana ndio wakristo na Wayahudi.

4. Waarabu ni watu ambao wanawaheshimu sana Wazee na Watawala wao...Ni mwiko sana kukosoa,kudhihaki na hata kumfokea mtu aliyekuzidi umri au aliye mtawala wako.Wana Heshima yenye hofu kubwa yaweza ikawa kuliko taifa zingine zote.

5. Sio Mataifa yote ya kiarabu vazi lao la utamaduni ni kanzu,la hasha,bali yapo mataifa ya kiarabu ni nadra sana kumuona mtu kavaa kanzu nayo ni mojawapo Syria,Misri na Lebanon.

6. Kwenye Lugha ya kiarabu,lugha/ishara ya mwili(body language) ni kitu muhimu sana kuliko hata maongezi yenyewe..Pata muda tizama clips zao.

7. Lugha ya kiarabu ni miongoni mwa lugha inayozungumzwa kwa mfanano karibia mataifa yote ya kiarabu..mfano kwenye kiingereza kuna kiingereza cha wales, australia, marekani 

8. Sifa kubwa ya waarabu katika ulaji chakula ni "kutumia mkono" yaani no kijiko no uma..hata awe tajiri kiasi gani dhana yake ya kwanza kwenye kula ni "mkono wake"..Hii imepelekea kupenda kuwa na hotel/migahawa yao mahsusi.

9. Ukiwa kwenye mkutano/meeting ni mwiko kutizama saa iwe ukutani au mkononi,ukifanya hivyo ni ishara ya kuwadharau walioko kwenye mkutano.

10. Mahusiano ya kifamilia/undugu yana nguvu sana kwa waarabu..kwa mfano unaeza kuta nyumba moja wanaishi karibia ukoo/yani bibi wa bibi mpaka babu wa babu na wajukuu wake.

11. Umri hauna nafasi katika kujitegemea yani kuwa huru na makatazo au amri au huduma za wazazi..yani mtu anaweza akafika hata miaka 40 lakini akawa anahudumiwa na wazazi wake.

12. Kwa kawaida uchukua zaidi ya mwaka na miezi saba kujua lugha ya kiarabu kwa ufasaha.

13. Kinywaji kikubwa katika nchi za waarabu ni kahawa...
Image result for animated download now gif
Powered by Blogger.