KAMA HUKULIONA TUKIO HILI JANA, SUBIRI MIAKA 107 IJAYO
“Tukio la kupatwa kwa mwezi limetokea leo ambapo nuru ya mwezi mkamilifu (full moon), imezuiwa na dunia hivyo mwezi kuonekana kuwa na rangi nyekundu katika kipindi cha saa kadhaa kuanzia saa 4:30 usiku hadi saa 6:14 usiku,” Tukio hilo ambalo limechukua muda wa saa tatu mpaka kukamilika kwake ni la kwanza katika karne ya 21.
Habari zaidi...
Mnamo tarehe 27.07.2018 usiku, kutakuwepo kwa tukio kubwa duniani la Kupatwa kwa Mwezi, linalotarajiwa kuchukua muda wa saa moja na dakika 43. Kupatwa huko kutakuwa kwa Giza Totoro. Kupatwa kwa Mwezi huhusisha Dunia kuwa katikati ya Jua na Mwezi. Chanzo cha kupata huko kuchukua muda mrefu, kunatokana na kwamba, Mwezi utakuwa katika eneo lake la mbali (farthest distance) la mzingo wake.
Wataalamu wanaeleza kuwa, kupatwa huko kwa muda mrefu ni matukio ya nadra ambapo tukio lingine litakalochukua muda mrefu, linatarajiwa kutokea miaka 107 ijayo, mwaka 2123, ambapo karibia wanadamu wote waliopo sasa, watakuwa hawapo tena duniani. Kupata kwa Mwezi hakuna madhara ya kiafya, so watu wanaruhusiwa kuangalia tukio hilo bila kuhitaji miwani.
Leave a Comment