MAELEZO YA KINA KUHUSU UBER, USAFIRI SALAMA NA WA BEI YA CHINI KWA MTANZANIA
Uber ni nini?
Uber ni application inayokuwezesha kupata usafiri wa bei ya chini na salama katika sehemu nyingi za mkoa wa Dar-es-Salaam, kwa kupitia simu yako ya mkononi. Usafiri huu ni wa kutumia magari madogo yanayoweza kubeba kuanzia mtu mmoja hadi watu wanne.
Kujisajili na Uber
Nenda playstore, search 'Uber' utaiona ina icon nyeusi, download kisha ifungue.
Fanya usajili kwa kutumia namba yako ya simu, email na pia utachagua neno la siri.
Kupata punguzo la Tsh6200 katika trip yako ya kwanza
- Nenda Menu kwa kubonyeza mistari mitatu iliyoko juu kushoto,Kisha bonyeza Payments, kisha bonyeza Add promo code , andika ubertz5
- Utaona maandishi ya kijani yakionyesha kwamba utapata punguzo la tsh6200 katika trip yako ya kwanza.
- Nitatoa mfano, safari yako ya kwanza ni kutoka posta hadi magomeni,na gharama yake ni shilingi 7200,basi utalipa sh1000 tu kutokana na hilo punguzo,lakini katika safari ya pili utalipa nauli kamili.
Zingatia
Unaweza kujisajili mara moja tu kwa kutumia hiyo promotion code, ukirudia kujisajili kwa namba nyingine kama baadhi ya watu wanavyopotosha mitandaoni, akaunti yako ya uber itafungiwa na hutaweza tena kutumia huduma za uber
Jinsi ya kutumia Uber kuita usafiri.
- Fungua app ya Uber, hakikisha umewasha GPS, itakuletea maandishi 'where to'.Hapo utajaza unapotaka kwenda,mfano 'Magomeni Mapipa'.
- Itakuonyesha kiasi cha nauli inayokadiriwa, na utabonyeza 'Request uberX'
- Hapo hapo,itakuonyesha jina na namba ya gari la dereva atakayekufata hapo hapo ulipo, na ndani ya dk5 atakuwa kashafika.
Malipo ya usafiri
- Ukifika 'destination' yako dereva atabonyeza 'Stop trip' kwenye application iliyoko kwenye simu yake, na hapo hapo itaonyesha nauli kwenye simu yako na kwenye simu ya dereva
- Unaweza kulipa kwa Cash(Taslimu) au kwa kutuma Kadi ya benki
Umuhimu wa kutumia Uber
- Ni gharama nafuu zaidi ukilinganisha na taxi za kawaida, kwa sababu bei inahesabiwa na mashine yenyewe kulingana na umbali wa sehemu unayoenda, na sio derevaa kujipangia bei kubwa
- Ni salama zaidi, hasahasa usiku, kwasababu dereva wa uber anakuwa amesajiliwa na endapo itatokea tatizo lolote mfano kusahau kitu kwenye gari, dereva anaweza kupatikana kwa haraka
- Inakusaidia kuokoa muda; mfano upo sehemu ambapo hamna taxi,bajaji wala bodaboda, unaweza kuita usafiri na ukakufata hapohapo kwa kutumia app hii.
UPDATE 1:
Uber inakuletea usafiri wa bajaji pia, ambao ni bei rahisi zaidi, sasa unaweza kuchagua kati ya UberX(taxi) na UberPoa(bajaji) kutokana na uwezo wako. UberPOA inapatikana maeneo ya Mwenge, Sinza, Kijitonyama, Mikocheni A, Mwananyamala, Kinondoni, Namanga, Msasani, Oysterbay, Masaki & Kigamboni ingawa huduma hii inasambaa maeneo mengi katika siku za baadaye.
UPDATE 2:
Kwa wale waliokwisha kutumia ofa yao ya kwanza(first ride), usiache kutumia Uber, endelea na unaweza ukapata punguzo la 25% au 50% kwa safari zako 4 mara kwa mara..!
Leave a Comment