MAMBO USIYOFAHAMU KUHUSU MNYAMA FISI

MFAHAMU FISI.
Fisi ni myama aishiye mbugani, ambaye ana sifa kemu kemu kwa wanadamu, pengine hii ni kutokana na kutokeza katika simulizi nyingi tulizokuwa tukijifunza katika hadithi, pindi tulipokuwa shule ya msingi, ana umaarufu wa jina la bwana afya wa porini, hii ni kutokana na sifa yake ya kula mizoga, lakini pia ni mnyama ambaye amepata sifa nyingi za kuwa bwege kutokana na kusumbuliwa sana sungura katika hadithi hizo za shule ya msingi.

Mnyama huyu ni maarufu na pengine ndiye mnyama pekee mwenye kufahamika zaidi katika bara la Afrika, hususani hapa nyumbani, kwani mbali na kutokea katika hadithi, lakini pia mnyama huyu baadhi ya makabila humtumia wanapocheza ngoma za asili, pia ana sifa ya kuhusishwa sana na imani za kishirikina, baadhi ya jamii anapoonekana hupigwa mpaka kufa kwa imani kwamba ni mtu amejibadilisha kuwa fisi.

Jamaa hawa yaani fisi huishi kifamilia na kwa taarifa yako ni kwamba hujenga kabisa sehemu wanazokaa, urefu wao ni zaidi ya nchi 35, huwa na uzito wa kilo zaidi ya 75 inategemea na umri, huishi zaidi ya miaka 20, hubeba mimba kwa miezi mitatu na akizidisha ni siku chache sana,huzaa watoto kuanzia wawili mpaka wanne, kichwa chake hufanana na mbwa ila tofauti yao ipo katika muonekano, fisi ni mnyama ambaye miguu yake ya nyuma ni mifupi zaidi, hivyo unaweza ukamgundua kwa jinsi anavyotembea na matendo yake, huishi popote sehemu kame, vichakani na hata sehemu ambazo zina majani yenye ukijani sana, hivyo ni mnyama ambaye popote kwake ni kambi.

Pamoja na kwamba ni mnyama ambaye jina lake linakuzwa sana kwamba anatabia ya kula mizoga, lakini fisi ni mnyama anayewinda na hula nyama fresh, akikosa mawindo yake hufanya uporaji kwa wanyama kama simba na inapokosekana hata nafasi hiyo, basi akikutana na mfupa,mzoga yeye hana neno.

Wakati wanyama wengine wengi wakiwa wanaongozwa na madume, ukifika katika koo za fisi majike ndio viongozi, lakini mbali na uongozi pia fisi jike ana nguvu za mwili kuliko dume, bahati waliyonayo mbaya wanyama hawa hupata tabu sana ya uzazi pindi jike lijifunguapo, watoto wao wengi hufa wakati mama yao anapozaa, hivyo kama jike atazaa wakati dume halipo ana nafasi kubwa ya kuzaa watoto wafu, kwani fisi dume hutoa msaada kwa jike wakati wa kuzaa hasa ulinzi.
SIFA ZAKE ZA KIPEKEE

Mosi ni mnyama mnyonge lakini huweza kupola chakula kwa wanyama wakali kama simba.

- Fisi ni mnyama anayeweza kukimbia umbali mrefu kwa taratibu, we tangulia na spidi 120 yeye atakuja na 30 na atakukuta tuu njiani ukiwa umeanguka either kwa kuishiwa nguvu au misuli kukaza na hapo ndio atafanya biashara yake kwa urahisi, na sifa hii ndio watu husema eti anasubiri mtu adondoshe mkono wala sio kweli, ana akili zake.
- Fisi huzaliwa akiwa macho ujue.
- Fisi jike huwa na maamuzi yote kuanzia mahabani mpaka mgawanyo wa kazi.
- Fisi dume ni mnyama bwege anatawaliwa na jike lake.
- Fisi ni kiumbe asiye na mbio za kasi.
- Fisi hunguruma, hucheka pia hutoa milio mbali mbali inategemea na alipo, na hiyo huwa ni lugha wanayotumia kuwasiliana akifanya hivyo wenzie wakisikia wanajua tuu kuna jambo gani limemsibu mwenzao.
- Fisi jike huwa na muonekano wa jinsia mbili, katika uke wake kwa juu au sehemu ambayo mwanamke hukeketwa, ile sehemu kwa fisi huwa na ukubwa mkubwa sana inaweza fika nchi saba, jambo hilo humfanya aonekane na muonekano wa jinsia mbili.
- Fisi wakikosana kwa kuibiana chakula au dume, na kwa bahati mbaya mmoja awe Mdogo, hupigana mpaka Mdogo kufa, na kama wapo sawa mnyonge hukimbia, wakati huo dume hubaki likishangaa tuu na kushindwa lianzie wapi.
Usisubutu kumvizia fisi kwa nyuma, namna pekee ya kujirinda hurusha kinyesi chake kwa ghafla na atakuacha ukiwa umechanganyikiwa huku yeye akikimbia.
- Uoga kwake huisha akiwa na njaa Kali, kwa mfano hawezi kumuwinda binadamu mkubwa, lakini litokeapo suala la njaa Kali huwa hajali umri wa mtu.
- Watoto wake wanapofikisha umri wa miaka miwili mama yao huwatimua, wakajitegemee.
- Fisi anapokutana na watoto wa simba huwaua pasina huruma.
- Fisi dume halitakagi kusikia habari za watoto, huwa linaamini ni Mali ya jike, hivyo hanaga nao msaada kabisa.
- Fisi jike huwa na mwili mkubwa kuliko dume.
Adui yao mkubwa ni mbwa mwitu, kwakuwa huwapora nyama ambazo wao wametafuta kwa tabu sana, pengine kwa kuhatarisha maisha yao.
- Fisi wanaogopa sana dume la simba, wanaweza kuwasumbua majike wa simba watatu lakini likija dume huwa linahakikisha mmoja kati yao anachechemea, hivyo wanapomuona simba dume hupiga kelele za kupeana habari kuna hatari.
- Fisi ana uwezo mkubwa wa kunusa, hivyo ukifukia kitu hata chini anaweza kukitambua endapo tuu kina harufu ya damu damu.
Viumbe hawa wakijihakikishia akiba ya chakula katika himaya zao, basi hufanya sherehe na sherehe zao huwa na ufanano na sherehe za binadamu, hucheza, hufurahi, hufanya ngono na ugomvi huzuka pia wakati huo watoto wote hufichwa ndani ya nyumba.
- Fisi jike huweza kupiga dume mpaka likahama nyumba, na hutumia sana ujanja huu endapo jike linataka kuishi na mchepuko wake ndani.
Fisi huamini pia katika umoja.

WANYAMA WABABE KWA FISI 

Fisi ni mnyama mnyonge sana na ni mnyama ambaye karibia wanyama wote wawindaji ni wababe kwake, kinachowasaidia ni hali ile ya kutembea makundi makundi yaani kifamilia, ndio huwafanya na wao waonekane kidogo wanajiweza.

UKIKUTANA NAYE UFANYE NINI?

Kwanza kaa ukijua fisi sio mnyama wa kumchezea, naye ana uwezo wa kukurarua vile vile, usijeanza fikiria zile hadithi za shule ya msingi ukamchukulia pia, sungura mwenyewe akimuona anafungua njia vibaya sana, japokuwa si kiumbe anayevamia moja kwa moja, huuma kwa kuvizia, jihami vya kutosha na uwe na silaha nzuri kama fimbo nzito, mawe yenye ujazo mzito, na usimpe nafasi ya kumuonesha unamuogopa japokuwa kicheko chake chaweza kukutia hofu Mara dufu.

Ukumbuke anapotoa sauti hizo, wenzie wanaposikia hujua kina jambo, hivyo hakikisha haumpi nafasi hiyo, vinginevyo wakiwa zaidi ya wawili andika na wosia kabisa. Wanyama hawa wapo wa kutosha sehemu kama ngorongoro ni zaidi ya uchafu, mikumi, Serengeti ndio usiseme, hapo hujamalizia na katavi, ni wanyama ambao kibali cha kumuweka kwenye zoo unaweza ukakipata ndani ya muda mfupi sana.




Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.