UTARATIBU WA KUSAJILI KIWANDA
1.0 Utangulizi
Wakala wa usajili wa Biashara na Leseni BRELA inawatangazia
kuwa usajili wa viwanda unafanywa
chini ya Sheria ya Kusajili
na Kusimamia Viwanda ya Taifa
na. 46 ya 2002.
2.0 Kiwango cha
Mtaji
Sheria hii inamtaka kila mwenye
kiwanda kuwa na leseni ya kiwanda, kuna aina mbili ya usajili wa viwanda ambao ni
kama ifuatavyo:-
a) Viwanda vikubwa ambavyo mtaji wake ni zaidi ya
shillingi million mia moja (100,000,000)
Tanzania shillingi
b) Viwanda vidogo ambavyo mtaji wake chini ya shillingi million mia moja (100,000,000) Tanzania shillingi
2.1 Taratibu za kusajili Viwanda Vikubwa
a) kujaza fomu ya
maombi
b) kuwasilisha Memorandum and Articles of Associations
c) kuwasilisha hati
ya usajili ya kampuni
d) mchanganuo wa
mradi
Baada ya maombi kupitishwa na Bodi ya Leseni
ya Viwanda na ada kulipwa leseni ya kiwanda
hutolewa.
2.2 Taratibu za
kusajili Viwanda Vidogo.
Hivi ni
viwanda vyenye mtaji wa chini ya
shilingi milio mia moja(100,000,0000)Tsh,aina hii ya kiwanda hupata cheti
cha Kiwanda na cheti hiki hutolewa
na Msajili wa Kiwanda bila ya
kupitia bodi ya Leseni ya Viwanda.
3.0 Maombi ya kuhamisha kiwanda.
Utaratibu wa kuhamisha viwanda kutoka eneo moja kwenda lingine,kuongeza au
kubadlisha unatakiwa utoe taarifa
kwa njia ya barua na kujaza fomu ya uhamisho.
KWA
MAELEZO:
HIVYO
BASI WAMILIKI WOTE AMBAO WANA ENDESHA VIWANDA BILA KUWA NA ,LESENI YA KIWANDA INAYOTOKA BRELA , AU AMEHAMISHA KIWANDA KUTOKA ENEO MOJA KWENDA LINGINE BILA KUTOA TAARIFA , MNAOMBWA MFIKE
OFISINI MTAA WA LUMUMBA KWENYE JENGO LA USHIRIKA (TFC )GHOROFA YA 3 CHUMBA NAMBA 306 NA
307 KWA KUSAJILI KIWANDA CHAKO.
AU KWA MSAADA ZAIDI PIGA NAMBA ZIFUATAZO
+255 222 2180141,
0754285137, 0784411777 au tuma
Email: brela@brela-tz.org
Tovuti: www.brela-tz.org
Leave a Comment