ALIYEKUWA KATIBU MKUU WA UMOJA WA MATAIFA (UN), KOFFI ANNAN AFARIKI DUNIA

TANZIA: Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa(UN), Kofi Annan afariki dunia akiwa na miaka 80. Mwanadiplomasia huyo mashuhuri amefariki asubuhi ya leo huko nchini Uswisi baada ya kuugua kwa muda mfupi. Kutokana na umahiri wake Kofi Annan alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Desemba 1996. Na alianza kazi rasmi Januari 1, 1997.


Mwaka 2001 alichaguliwa kwa mara ya pili kuuongoza tena Umoja wa Mataifa. Oktoba 12, 2001 alitunukiwa Tuzo ya Amani ya Nobel. Annan alianza kutumikia nafasi mbalimbali ndani ya Umoja wa Mataifa(UN) tangu mwaka 1974 ingawa aliacha kazi na kurudi kuiongoza Kampuni ya Utalii nchini kwake (GHANA). Mwaka 1976 alirudi tena kwenye ulingo wa siasa za kimataifa na safari yake ndani ya Umoja wa Mataifa ikaanza rasmi. Kofi Atta Annan alizaliwa mnamo Aprili 8, 1938.

May his soul Rest In Peace.

Mwandishi: MK254

Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.