JINSI MADEREVA WA UBER WANAVYOIBIA WATEJA WAO
Kwa wale tunaopenda kutumia usafiri wa Uber, madereva wamekua wakituibia bila sisi kujua.
Mimi ni mtumiaji mzuri wa uber, bahati nzuri nina jamaa yangu hua ni dereva wa uber, nina muda sijafanya nae routes za hapa mjini Daslam, juzi hapa nikamuita akaje twende mahala. Katika mazungumzo akaniuliza sijawahi kupewa gharama za ajabu kwa route za kawaida nazozifaham, nimamwambia nishapewa nyingi tu ila hua nalipa. Akaomba nimuonyeshe kwenye my trips, ndio akanionyesha ujinga unaofanyika na madereva wa uber kuibia wateja.
Iko hivi, madereva wanachokifanya baada ya kuanza safari wanawezesha mfumo wa simu wa kuhifadhi matumizi ya betri(power saving). Huo mfumo kwenye sim ukiwezeshwa kitu cha kwanza unachoanza nacho ni navigation system na vitu vingine. Kwa kua mfumo wa uber unatumia navigation, hvyo unachanganyikiwa unakua hausomi vizuri barabara mliopitia, ukifika mwisho inakupa bei ya ajabu ila ukiangalia ramani utakuta safari yenu haikua straight, mmezunguka zunguka sana kitu ambacho sio kweli.
Angalia huu mfano.
Hii picha ya kwanza ni safari yangu ya mara kwa mara na iko straight. Picha ya pili ndio magumashi. Angalia na gharama zake.
Huu ndio wizi mpya wa madereva wa uber, wao wanadai wamefundishwa na madereva wa taxify.
Chanzo: JamiiForums
Leave a Comment