JULIE GENTER: WAZIRI ATUMIA BAISKELI KWENDA HOSPITALI KUJIFUNGUA
Julie Genter kutoka chama cha kijani, Green Party, amesema kuwa ameenda kwa baiskeli kwakuwa hakukua na nafasi ya kutosha ndani ya gari, alipiga picha na mweza wake wakiwa katika safari hiyo ya baiskeli na kuiweka katika akaunti yake ya Instagram. Mwezi juni mbunge Jacinda Ardern alikua wa pili kujifunglia katika sehemu ya kazi, wote yeye na Bi Genter walikua wakihudhuria Clinic pamoja katika hospitali ya umma huko mji Auckland.
- Kifo cha Annan: Viongozi nchini Kenya watuma rambi rambi zao
- Kwa nini wanawake wasioolewa hupangishwa nyumba kwa shida?
Bi Genter 38, anajulikana sana pia kama mdau mkubwa katika kuendesha baiskeli, aliandika katika mtandao wake wa Instagram, ''mtuombee Baraka, mimi na mwenzangu tumepanda kwenye baiskeli kwasababu hakukua na nafasi kwenye gari kutokana na wasindikizaji kukaa kote.
Waziri huyo atachukua miezi mitatu ya likizo ya uzazi, ataungana na baadhi ya wanasiasa waliopata watoto wakati wanatumikia nafasi za kisiasa. Mbunge wa kwanza kupata mtoto akitumikia bunge la New Zealand, ilikua mwaka 1970, huku mwingine akinyonyesha kwa mara ya kwanza katika eneo la kazi mwaka 1983.
Nao Austalia walibadilisha kanuni mwaka 2016 kuruhusu watunga sheria kuweka sheria ya kunyonyesha katika eneo maalumu ndani ya bunge.
Katika miaka ya hivi karibuni, Sweden, Italia na Bunge la Ulaya wamegusa ulimwengu kwa upigaji kura wakiwa wamebeba watoto.
Chanzo: BBC Swahili
Leave a Comment