ALICHOONGEA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KUGUNDUA HAMISA ANAMROGA
Msanii wa muziki Diamond Platnumz amefunguka kuzungumzia sakata la kutaka kurogwa na mzazi mwenzake Hamisa Mobetto ikiwa ni siku chache toka audio inayodaiwa kuwa ya mrembo huyo isambae mtandaoni akisikika kuzungumza na mtu anayeadaiwa kuwa ni mganga kuhusu familia ya rais huyo wa WCB.
“Unapotaka kwenda kwa mganga uniroge mimi na mama yangu, unaonekana wewe haushindwi hata kumuua mama yangu, kama unawaza sijui nikupe nyumba". "Voice notes zinasambaa sambaa hata mimi nilitumiwa, ninazo ,unasikia kitu, halafu unajua huyu ni yeye[Hamisa Mobeto], halafu nikamwambia huyu ni wewe,” alisema Diamond kupitia Refresh ya Wasafi TV.
”Watu kuna vitu wanaongea ongea halafu wanajaribu kuvipindisha aonekane Mama yangu na dada yangu wana matatizo, Mama yangu na dada yangu hawawezi kuwa na matatizo." "Halafu hao watu wako unaowatuma wakatukane, nimeshakuona ukiwatuma wakatukane kwa watu wengine kwa sababu pia uliwatuma pia wamtukane na Zamaradi,” alisema Diamond Platnumz.
Source: Bongo 5
Leave a Comment