BUNGENI, DODOMA: WABUNGE WALIOBANDIKA KUCHA NA KOPE MARUFUKU KUINGIA BUNGENI
Dodoma. Spika wa Bunge, Job Ndugai, amepiga marufuku wabunge
wanawake wenye kucha na kope za kubandika wasiingie bungeni.
"Kwa mamlaka niliyopewa, napiga marufuku wabunge
waliobandika kucha za bandia na kope za bandia kwamba ni marufuku na hilo la
kujipodoa bado najadiliana na wataalam wangu," amesema Spika. Spika Ndugai alitoa kauli hiyo leo bungeni muda mfupi baada
ya Naibu Waziri wa afya, Dk Faustin Ndugulile kutoa majibu ya madhara makubwa
wanayopata wanawake wanaotumia kucha na kope za bandia. Naibu Waziri alisema takribani wagonjwa 700 hupokelewa kwa
mwaka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa na matatizo ya ngozi
yatokanayo na kumeza vidonge vinavyobadili sura pamoja na vipodozi vyenye
kemikali na kuwa watu hao wapo kwenye hatari ya kupata magonjwa ya saratani na
ya ngozi.
Katika swali la msingi, Mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Fatuma
Toufiq alihoji ni wanawake wangapi wameathirika macho kutokana na matumizi ya
kope bandia.
Naibu Waziri alisema kucha na kope za kubandika si vipodozi
kwa mujibu wa sheria ya chakula, dawa na vipodozi sura ya 219 inayosimamiwa na
Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA). "Kwa mujibu wa sheria hiyo, kipodozi ni kitu chochote
kinachotumika kwenye mwili au sehemu ya mwili," alisema Dk Ndugulile.
For the English Audience
The Speaker of Tanzania's National Assembly, Job Ndugai, has
banned women Members of Parliament with artificial nails and eyelashes to
participate in the legislative house activities. Speaker Ndugai said that on
Monday, September 10, 2018 and he also said that he will continue to receive
opinions on the issue of skin bleaching.
"By the powers vested in me, I hereby ban the MPs who
are wearing artificial nails and eyelashes extensions from participating in the
parliament sessions and I am still discussing with experts regarding the
excessive use of makeup," said the Speaker.
Speaker Ndugai gave the statement today in the parliament
shortly after Deputy Health Minister, Dr. Faustin Ndugulile gave out a report
on the negative effects of nail and eyelash extensions on women. Dr. Ndugulile
was responding to a question from Ms Fatuma Tawfiq (Special Seats - CCM) who
wanted to know the number of women who have been adversely affected by the use
of these eyelashes.
Dr. Ndugulile said that approximately 700 patients are
received annually at the Muhimbili National Hospital with skin problems which
are caused by the use of skin bleach pills and other chemicals and that these
people were at risk of getting skin cancer and other health effects.
Leave a Comment