HATIMAYE DOGO JANJA ABWAGWA RASMI


Muigizaji wa Bongo movie Mrembo Irene Uwoya ametoa kauli ambayo imethibitisha kuachana kwake na mume wake staa wa Bongo fleva Dogo Janja.

Kwa mwezi sasa kumekuwa na tetesi kuwa Irene Uwoya ameachana na Dogo huku tetesi hizo zikichangiwa na Safari aliyoifanya Uwoya wiki chache zilizopita nchini Dubai ambako ilisemekana alikuwa na mwanaume mwingine.

Ingawa wawili hao walishawahi kukataa tetesi za kuachana Lakini sasa inaonekana kama wameamua kuweka mambo hadharani kwani Uwoya ameandika maneno ambayo yameleta sintofahamu.

Kupitia page yake ya instagram, Uwoya ameweka comment kwa shabiki mmoja aliyemhoji Kuhusu Dogo Janja ambapo ameandika kuwa ameamua kumuacha Dogo Janja na kutafuta mwanaume anayeendana naye kiumri.

Irene Uwoya aliandika maneno haya: "Simlisema wenyewe nitafute wa umri wangu yeye bado mdogo? Sasa nimefata ushauri jamani…..au kaishakuwa."


Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.