HAWA NI WATU WALIOMDHIHAKI MUNGU NA KUPATWA NA SHIDA
1. JOHN LENNON (MUIMBAJI)
Wakati alipokuwa akihojiwa na mwandishi wa habari wa gazeti la American
alinukuliwa akisema hivi "Ukristo utakufa na kutoweka duniani, siwezi kuwa
na wasiwasi na hilo kwa kuwa nina uhakika nalo. Mafundisho ya Yesu yalikuwa
sahihi na wala sipingi hilo ila mafundisho yale yalikuwa mepesi sana ambayo mtu
yeyote anaweza kuyafundisha. Hebu angalia leo, tumekuwa maarufu hata zaidi yake
(Hapo alilitaja kundi lake la The Bettle). Ilikuwa mwaka 1966. Wiki moja baada
ya kutamba kwamba yeye na kundi lake lilikuwa maarufu hata zaidi ya Yesu,
akapigwa risasi sita na kufariki.
2. TANCREDO NEVES (RAIS WA BRAZIL)
Alisema kwamba endapo angepata kura laki tano kutoka katika uchaguzi mkuu wa
Brazil na kuwa rais, hata MUNGU asingeweza kumtoa katika urais huo.
Akafanikiwa, akapata kura zaidi ya hizo, akashinda uchaguzi, siku moja kabla ya
kuapishwa, akafariki dunia.
3. CAZUZA (MWANAMUZIKI WA BRAZIL)
Alipokuwa katika shoo yake ndani ya jiji la Rio De Janeiro, alichukua sigara,
akaanza kuivuta, akachukua nyingine na kisha kuirusha juu na kusema
"Mungu, hiyo yako, chukua nawe uvute". Alifariki akiwa na miaka 32 kwa
ugonjwa wa kansa ya mapafu ambayo iliyaharibu sana mapafu yake kuliko mgonjwa
yeyote yule.
4. MTENGENEZAJI WA MELI YA TITANIC.
Baada ya kutengeneza meli ya Titanic, mwanahabari akamuuliza ni kwa kiasi gani
ilikuwa salama nae akajibu "Ni salama sana, haiwezi kuzama na hata Mungu
hawezi kuizamisha" Nafikiri unajua kilichotokea kuhusu Titanic.
5. BON SCOTT (MUIMBAJI)
Mwimbaji huyu ambaye alitamba miaka ya 70 alitoa wimbo wake mmoja mwaka 1979
wenye maneno haya "Don't stop me; I'm going down all the way, down the
highway to hell'. Tarehe 19 February mwaka 1980, alikutwa amekufa baada ya
kupaliwa na matapishi yake.
6. Mwanamke mmoja alikuwa akihofia sana kuhusu ulevi wa marafiki wa mtoto wake. Wakati wanataka kuondoka na gari, akamshika mtoto wake mkono garini na
kumwambia "Binti yangu, Mungu awatangulie katika safari yenu" Yule
binti akajibu "Gari imejaa mama, huyo Mungu labda akae kwenye boneti la
gari". Baada ya masafa fulani ya safari yao, gari lile lilipata ajali
kiasi ambacho hata polisi hawakujua ni aina gani ya gari lilikuwa. Lilikuwa
limebondeka sana na watu wote walikutwa wamekufa. Kilichowashangaza polisi,
trey la mayai wala halikuonekana kuguswa na hakuna hata yai moja lililokuwa
limevunjika na wakati gari lilibondeka mpaka kutokutambulika.
7. CHRISTINA HEWITT (MWANDISHI WA HABARI)
Huyu alikaririwa akisema hivi "Nimesoma vitabu vyote duniani, ila hakuna
kitabu kibaya...kibaya na kibaya kama Biblia" Siku chache baada ya kusema
maneno hayo, mwili wake ulikutwa umeunguzwa na moto ambao haikujulikana mpaka
leo ule moto ulisababishwa na nini.
8. MARILYN MONROE (MUIGIZAJI)
Huyu alifuatwa na Bill Graham na kumwambia kwamba alitumwa na Roho wa Mungu kwa
ajili ya kumhubiria. Alimkaribisha ndani, akamsikiliza kwa makini, alipomaliza
akasema "Simuhitaji Yesu wako, unaweza kuondoka nae". Wiki moja
baadae, alikutwa amekufa katika makazi yake. Polisi walijaribu kuchunguza kipi
kilimuua, mpaka leo hawajapata jibu..!
Leave a Comment