KIJANA ADUKUA TAARIFA ZA APPLE ILI AFANYE NAO KAZI
Kijana mmoja kutoka nchini Australia amekiri kuudukua
mtandao wa Apple na kuiba nyaraka kadhaa. Kijana huyo wa kiume mwenye
miaka 16 aliingia kwenye mtandao huo mara kadhaa mwaka huu kutoka nyumbani kwao
huko Melbourne, Australia kwa mujibu wa gazeti la Age. Alisema alihifadhi
nyaraka hizo kwenye ghala linalofahamika kama 'hacky hack hack'..!
Apple inasema
kuwa hakuna taarifa za wateja wake zilifuja. Lakini gazeti la Age linasisitiza
kuwa kijana huyo aliingiakwenye akaunti za wateja. Kwa mujibu wa taarifa zilizowasilishwa
mahakamani, kampuni ya simu ililijulisha shirika la ujasasi la Marekani wakati
ilifahamu kuhusu udukuzi huo na kuwajulisha polisi wa Australia AFP. Polisi hao
kisha wakafanya uvamizi kwenye nyumba ya kijana huyo ambapo walipata kompiuta
mbili zenye namba sawa na za vifaa vilivyotumiwa. Polisi pia walipota simu na
vifaa vingine. Kijana adukua Apple kwa sababu alitaka kufanya kazi nao.
Kwa mujibu wa Age, kijana huyo alikuwa amejigamba kuhusu udukuzi huo kwenye
ujumbe wa WhatsApp. Age liliripoti kuwa alidukua kwa sababu alikuwa shabiki
mkubwa wa Apple na alikuwa na ndoto ya kufanya kazi huko. Wakili wake alisema
alikuwa amepata umaarufu mkubwa kwenye jamii ya wadukuzi duniani. Jina la
kijana huyo halijafichuliwa kwa sababu za kisheria. Atahukumiwa tarehe 20
Septemba.
Chanzo: BBC
Leave a Comment