KILLSHOT YA EMINEM YAWEKA REKODI MPYA 'BILLBOARD HOT 100'

Killshot ya Eminem yaweka rekodi, yawa diss-track iliyoshika namba za juu zaidi kwenye chart za ‘Billboard Hot 100’.
'Killshot’ sio diss-track tu bali ni diss-track iliyoweka rekodi ya kushika namba za juu zaidi kwenye chart za ‘Billboard Hot 100’ imeshika namba 3. Diss-track hiyo ya Eminem kwenda kwa Machine Gun Kelly pia imekuwa ngoma ya 20 ya Eminem kuingia kwenye Top 10 ya #BillboardHot100. Killshot imesikilizwa zaidi ya mara Million 100 kwenye mtandao wa YouTube.
Kwa upande mwingine pia ngoma ya ‘Girls like you’ ya Maroon 5 na Cardi B imeichoma ‘In my feeling’ ya Drake namba moja kwenye chart hizo hivo kuifanya iwe track ya tatu ya Cardi B kushika namba moja, ni rapper pekee wa kike aliyeweka rekodi hiyo.
Leave a Comment