MALAYSIA: WACHAPWA VIBOKO KWA KUJIHUSISHA NA MAPENZI YA JINSIA MOJA


 
Wanawake wawili nchini Malaysia waliopatwa na hatia ya kujaribu kufanya mapenzi ya jinsia moja ndani wamechapwa viboko kwenye mahakama ya kidini.


Wanawake hao waislamu wenye umri wa miaka kati ya 22 na 32 kila mmoja alichapwa viboko sita kwenye mahakana ya Sharia katika jimbo la Terengganu. Kulingana na afisa mmoja ni kuwa hiyo ndiyo hukumu ya kwanza inayohusu mapenzi ya jinsia moja na ndiyo adhabu ya kwanza ya kuchapwa hadharani. Makundi ya kutetea haki za binadamu yamekosoa vikali hatua hiyo ya kuchapwa kwa wanawake. Kuchapwa huko kulishuhudiwa na zaidi ya watu 100 kwa mujibu wa vyombo vya habari..!
Mwanachama mmoja wa baraza kuu la Terenggau, Satiful Bahri Mamat, alitea adhabu hiyo, akiliambia shirika la Reuters kuwa hatua haikuwa na ya kutesa au kuumiza, na ilifanyika hadhari ili iwe funzo kwa jamii.

Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.