NA HII NDIYO VIDEO YENYE 'DISLIKES' MILIONI MOJA YOUTUBE

Wakati wasanii wengi nchini Tanzania wakifurahi pindi video zao zinapofikisha views zaidi ya millioni, huko kwa wenzetu hali ni tofauti kabisa kwani imekuwa kitu cha kawaida kwa msanii kupata views zaidi ya millioni 100 endapo nyimbo ni kali na msanii husika ana mashabiki wengi. Leo katika pita pita zangu mitandaoni nimekutana na video ambayo ina dislikes milioni moja (huenda na zaidi). Unaweza kushangaa kwanini msanii mkubwa kama Ed Sheeran video yake ina dislikes millioni moja lakini kitu unachotakiwa kufahamu ni kwamba video hiyo mpaka sasa ina views Billioni 3,817,818,081 (mpaka kufikia leo 27.09) huenda ikaongezeka na kufikia billioni 4 hivi karibuni..!

Video ya shape of you ya Ed Sheeran ndiyo video ya 2 kuangaliwa zaidi kwenye mtandao wa Youtube ikiongozwa na Despacito yenye views billioni 5 na nusu (5.5b). Unahisi msanii gani nchini Tanzania atakuwa wa kwanza kufikisha views millioni 100 kwenye mtandao wa YouTube? Comment hapo chini jina lake
Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.