NJIA SAHIHI ZA KUACHANA NA MPENZI WAKO KWA AMANI

Mdau wetu ameainisha njia zifuatazo kuwasaidia wadau kumaliza mahusiano na wenzi wao kwa amani.
1. Kuwa na Uhakika na unachotaka kufanya: Kama huna uhakika juu ya hisia zako kwa mwenzi wako unapotaka kuvunja uhusiano bora usifanye hivyo maana utafanya moyo wako usiwe na maamuzi dhabiti.
2. Fikiria Sababu za Kuvunja Uhusiano: Unapojua sababu zinazopelekea wewe kuvunja mahusiano itakusaidia kutoa majibu ya uaminifu pale unapoulizwa.

3. Maliza Mahusiano wewe Binafsi: Kama umekuwa na mpenzi wako kwa muda mrefu au kipindi chochote uliwekeza muda na nguvu zako za kujenga mapenzi, basi ni busara mahusiano hayo ukayamaliza mwenyewe.
4. Msikilize mwenzi wako: Hata kama umeshaamua huwezi kubadili mawazo juu ya kuvunja mahusiano yenu haina maana kuwa usimsikilize mwenzi wako.
5. Kuwa Mtulivu na Makini: Unahitaji kuumaliza uhusiano na kuondoka mahali mlipo. Hata hivyo ni busara kuwa mtaratibu na mpole.
Je, nini uzoefu wako kuhusu kuacha au kuachwa katika mahusiano?

Leave a Comment