JINSI YA KUSAJILI KAMPUNI YA UJENZI (BUILDING AND CIVIL CONTRACTOR)
Kumekua na sintofahamu nyingi sana kwa wadau wengi wanaotaka kufungua kampuni za ujenzi kutokana na ufinyu wa habari zinazohusiana na mambo haya ya ujenzi,sasa leo nitawajuza namna ya kusajili kampuni yako ya ujenzi kirahisi kwa kufuata taratibu nitakazoziainisha hapa.
1. Hatua ya kwanza ni lazima usajili kampuni yako BRELA,hapo BRELA utapata usajili wa kampuni yako na utapata namba ya usajili,hapo BRELA baadhi ya nyaraka muhimu watakazozihitaji ni pamoja na MOU (MEMAT) watahitaji pia taarifa binafsi za wamiliki,pamoja mahali ofisi ilipo.
Katika wamiliki watakaoainishwa BRELA ni lazima umuweke Mtu atakaekuwa na qualification katika fani ya ujenzi na awe amesajiliwa na Bodi zao,either ARCHITECT,ENGINEER au QUANTITY SURVEYOR usipomuweka hapa utapata usumbufu mkubwa sana mbeleni.
Angalizo (a): kwa urahisi wa BRELA tafuta wakala yoyote akusaidie kwa gharama nafuu na pia katika kuokoa Muda,hawa mawakala wapo na kwa kiasi cha sh 80,000 atakufanyia kazi yote bila usumbufu.
2. Hatua ya Pili nenda TRA uombe kupata TIN no ya kampuni yako,hii kiuhalisia ni bure kabisa na haina usumbufu kabisa,ukishapata TIN namba yako tayari utakua sasa umekamilisha nyaraka muhimu sana kwenda kwenye hatua inayofuatia.
3. Hatua Ya tatu hakikisha unafungua Account ya Bank ya kampuni yako,kama una kampuni ambayo inaexist na ina account inayofanya vizuri hiyokigezo kizuri sana cha kupata daraja la juu la kampuni ya ujenzi wakati wa usajili.
4. Hatua ya nne sasa unakwenda kwenye Bodi ya wakandarasi kwa ajili ya kuchukua form zao,pia unaweza kuzipakua kwenye Website yao Contractors Registration Board(CRB), katika form hizi kuna vitu vingi sana na viambatanisho vingi mno,siwezi kuvitaja vyote ila naomba nitaje vile vya muhimu unavyotakiwa kuwa navyo na pia kuviambatanisha,nitaandika vile vinavyowakwaza watu na kuwakatisha tamaa na namna ya kufanya.
- Technical Director,Ni lazima uwe na engineer au Architect au Quantity surveyor aliesajiliwa na Bodi zao na ambae hajaariwa mahali popote,hawa ni ngumu mno kuwapata na ukiwapata huwa wanademand hela nyingi mno,kuanzia 5 to 20 million tsh, option rahisi ni wewe kutafuta wale wazee wazee ambao wamestaafu,na uwape share(wakati unasajili BRELA)
- Ofice,Godown,Vehicles; lazima uonyeshe una office,uwe na mikataba ya upangaji au umiliki,na pia uwe na magari na kadi originals,pia kama una godown ni added advantage,ukiwa na truck pia unajiongezea uwezekano mkubwa sana wa kusajiliwa madaraja ya juu,hapa jua unapojaza kwenye form jiandae kuja kukaguliwa.
- Plants and tools: Inabidi pia uonyeshe una plants kama bulldozer,catapilars,compactor na nyinginezo pia vitu kama wheelbarrow,helmet,safety gears ni muhimu pia vyote hv utajaza kwa idadi yake kwenye form.
- Staff Team: hapa ni muhimu sana,inabidi uwe mjanja kuattach staff ambao ni muhimu kwenye sekta ya ujenzi kama technicians,engineers,arhitects,qs na staff wa kawaida kama acountants na wengineo,huwa wanaangalia sana aina ya staff ulionao kupata usajili.(hawa staff sio lazima wawe wamesajiliwa)
- Referees: hawa wawe ni registered engineers au architects ambao wamesajiliwa,hawa hawana restriction,watakujazia vizuri tu unawatoa.
- Bank Statement,hapa inabidi uwe mwangalifu mno maana wengi unakuta unaanza na bank statement haina chochote,inabidi utumie akili ya mjini,cha muhimu hakikisha namba ya account na jina ni vyako kweli,na iwe smart
- hakikisha una MOU,Certificate of Incorporation kutoka BRELA,TIN no kutoka TRA, share certificate (hizi zinauzwa kwenye stationaries zote then unajaza unacertify) halafu na mikataba ya wafanyakazi na miaktaba ya upangaji.
5. Ukimaliza kujaza form zote na kuomba daraja linalofaa,na kupiga copy zote zinazohitajika,hakikisha unacertify every documenti iliyopigwa copy,kila karatasi,jaza cv za wamiliki,na vyeti vyao,cv za wafanyakazi na certified certificate zao weka kwenye file then rudi na usubmitt brela utalipia sh 80,000 kwa ajili ya processing fee kwa kila kampuni uliyomba,kwa hiyo kama ni civil,na building utalipa 160,000 ikiongezeka hivyo hivyo.
6. Ukishasubmitt unaweza kuamua kuikimbiza document yako (hapa ni mjini) na ikaenda haraka na ukapangiwa tarehe ya kuja kukaguliwa,jitahidi kujiandaa kwa hali na mali na vifaa siku unayokuja kukaguliwa,unatakiwa ukawachukue wakaguzi,kwa usafiri wako...(for more details za nani ni poa UtaniPM)
pia uwe na document original za kila kitu kuanzia certificate hadi kadi za magari. jitahidi kutoa shukrani kwa wakaguzi( maana wamepoteza muda wao mwingi mno)
7. Jitahidi kujua siku ya kikao cha bodi kinakaa lini halafu kuanzia hapo fuatilia.
Kwa information zaidi,jaribu kutembelea website ya BRELA, na CRB na pia unaweza kuniuliza maswali na nitakua nikiyajibu kwa kadiri ninavyopata muda
- samahani kwa kuandika kitabu,lakini naamini kuna watu kitabu hichi kitabadilisha maisha yao
- mtu yoyote anaweza kuwa mkandarasi,sio lazima uwe na technical knoweledge
Chanzo: JamiiForums
Leave a Comment