HUYU HAPA MWANAMKE WA GHARAMA ZAIDI BARANI AFRIKA
Mfanyabiashara aitwaye Mr. Kok Alat (pichani mwenye suti nyeusi) amefanikiwa kuwashinda wanaume wengine watano akiwemo Gavana wa Jimbo hilo waliotaka kumuoa binti wa miaka 17 aitwaye Nyalong Ngong Deng Jalang kutoka Sudan ya Kusini kwa Kulipa mahali ya Ng'ombe 530 zenye thamani zaidi ya mil 450 na magari Matatu Toyota Land Cruiser V8 yenye thamani ya Tshs 750 milioni na $ 10,000 au Tshs Milioni 22.
Mr. Kok Alat amelipa MAHARI hiyo kwa baba mzazi wa binti Huyo ambaye ni bikra kutoka Dinka kijiji cha Awiel jimbo la South Eastern nchini Sudan Kusini kutokana na historia ya utamaduni wao, heshima, ukarimu, unyenyekevu, na utu walionao. "Baada ya wapinzani wake nao kufika dau la NG'OMBE 520 na magari matatu aina ya V8, Mr. Kok Alat alifunga mjadala huo na kutoa NG'OMBE hao 530, V8 tatu na Dola 10,000 na kutishia kuwa kama wataendelea kumpinga atatoa mahari hizo Mara mbili (NG'OMBE 1060, V8 sita, $ 20,000) na kuongeza ndege aina ya Jet aliyokuja nayo.
Hivyo amefanya binti huyo kuwa bibi harusi mwenye gharama kubwa barani Africa. Mrembo huyo, Nyalong Ngong Deng (17) kutoka eneo la Awerial, alikuwa na wachumba sita waliokuwa wanamtaka, ambapo kila mmoja alikuwa tayari kutoa mahali kubwa ikiwa ni pamoja na shilingi milioni moja za Kenya ambazo ni sawa na shilingi milioni 20 za Tanzania...!
Akiwa amekaa kwa utulivu kando ya mumewe, tajiri mkubwa aitwaye Kok Alat katika ukumbi wa Freedom Hall jijini Juba, Ijumaa iliyopita Nov 9, binti huyo wa kabila la Dinka aliibua mshangao kwa watu waliokuwa katika sherehe hiyo.
Kulingana na utamaduni wa Dinka na Nuer, bei ya mahari kwa kawaida ni ng'ombe 20 hadi 40 hivyo binti huyo amendika historia ya pekee katika kabila lake kwa kuolewa kwa mahari ya ng'ombe 530 na vitu vingine vya thamani.
Leave a Comment