MFAHAMU MTU PEKEE ALIYEPONA KWENYE GHARIKA LA NUHU NA HAKUWEPO KWENYE SAFINA
Mfalme OG anatajwa kwenye vitabu vya dini kuu tatu za mashariki ya kati i.e uislam, ukristo na uyahudi.... Inaelezwa alikuwa ni mfalme aliyetawala eneo la Canaan (palestina/israel ama jordan ya sasa )katika ulimwengu wa kale takriban miaka zaidi ya 6000 iliopita.... Na inaelezwa ndio mwanadamu aliyeishi zaidi kutokana na kuwa na mwili mkubwa sana aliishi zaidi ya miaka 3500!!! Alikuwa ni mfalme aliyeogopeka sana mashariki ya kati maana alikuwa jitu lenye nguvu na mrefu zaidi ya minazi kama anavyoelezwa na Nabii Amos.
Amos 2:9
9 Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini.
Umaarufu wa Mfalme Ogu wa bashan umekuja baada ya historia kubainisha kwamba ndio binadam pekee aliyesalia kwenye gharika nje ya Nuhu na familia yake!!
JE ALIPONAJE GHARIKA
1. Nadharia ya kwanza inasema alikuwa mrefu sana kiasi kwamba maji ya gharika yalimfikia kiunoni!!!!
2. Nadharia ya pili inasema kuwa alikuwa na ukaribu sana na Nuhu hivyo alipewa kazi ya kuiangalia safina kwa nje kuhakikisha haigongi mwamba au mawe makubwa ambayo yangeweza kuipasua safina na hiyo ndio ikawa pona yake!!! Inadaiwa alijishikiza pembeni ya safina ya nuhu ivo hakubebwa na maji ya gharika. Nadharia hii ina mashiko sababu hata baada ya gharika tunaona safina hii ilitua palepale ilipokuwa kabla ya gharika yaani haikuenda mbali kabisa kitu ambacho hakiwezekana kama nguvu ya mafuriko ikizingatiwa lazima boti ingesukumwa maili kadhaa mbele. Kingine kwa akili ya kawaida tu dunia nzima izame alafu ww pekee uwe kwenye boti hivi wanaokufa watakuacha kweli?? Lazima wangetaka kuivamia boti waingia na ukizingatia yalikuwa majitu marefu yangeweza kuipasua pasua ila kwa uwepo wa OG walishindwa maana wangekutana na kipigo cha mbwa mwizi!!
3. Nadharia ya tatu inasema kipindi cha gharika Ogu alikuwa bado hajazaliwa ila mimba yake ilikuwa imeshatungwa na mama yake aliekuwa mke wa Ham hivyo ham asingeweza kumuacha nyuma ingawa inadaiwa mimba hiyo haikuwa ya Ham bali ya Malaika aliyeitwa shamael!! Hivyo damu ya wanefili ikaweza kuvuka gharika kwa staili hiyo kupitia mtoto aliyezaliwa yaani mflame ogu ama canaan ambae watoto wake kwenye biblia wanatajwa kma majitu makubwa ambayo yaliona wanadamu kma panzi!!! Mfano amori aruba anak hivi gilgal amoni yebusi n.k
4. Nadharia ya tatu inasema alienda milimani hivyo gharika haikumkuta. Biblia iko wazi kuwa maji yalifunika MILIMA mirefu kwa futi 15 kwenda juu ina maana kma hyu OG alikuwa na futi zaidi ya 13 pengine 28 kama inavyoelezwa kwenye biblia ina maana kama alipanda milima mrefu zaidi basi hakuweza kumalizwa na gharika!! Simple logic
Mwanzo 7:20 Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano.
Najua kufikia hapa wengi mtasema ni upotoshaji na kwamba ni stori za kijiweni ila hoja hii inapata mashiko kupitia biblia kuwa mfalme OGU alikuwa ndio mnefili pekee aliyepona gharika.
Kumbukumbu la torati 3:11
11 (Kwani aliyesalia katika mabaki ya Warefai ni Ogu pekee, mfalme wa Bashani; tazama, kitanda chake kilikuwa kitanda cha chuma; kitanda hicho je! Hakiko Raba kwa wana wa Amoni? Urefu wake ulikuwa ni mikono kenda, na upana wake mikono minne, kwa mfano wa mkono wa mtu). Hapa biblia inasema OG NI MREFAI ALIYESALIA tafsiri ya kiingereza inasema LAST OF THE REPHAIMS ikimaanisha ni mnefili pekee aliyesalia baada ya gharika!!!!
BAADA YA GHARIKA
Kupitia vitabu vya dini na kihistoria tunaelezwa kuwa baada ya gharika aliendelea kutawala maeneo ya mashariki ya kati eneo la bashan huko Canaan walipoishi majitu mengine kma wayebusi waamori waamaleki wagilgashite n.k na inasemekana aliishi miaka 3500!! Yaani alikuwepo toka kizazi cha adam hadi kipindi wana wa israel wanarudi canaan !!
MWISHO WAKE
Vitabu vya kidini na historia vinasema mfalme OG au UJ BIN ANAQ kiarabu.... Alipambana na waisraeli waliokuwa wametoka misri kuelekea canaan na katika vita hiyo inaelezwa mfalme Og aliweza kunyanyua mlima mzima!!!! Na kutaka kuutupa kwenye kambi ya waisraeli lakini Inadaiwa kwa bahati mbaya au nzuri mlima ukavunjika katikati hivyo ukamnyima balance akaangukiwa na kipande cha mlima hivo kuumia vibaya na ndipo musa akapata fursa ya kumchoma na mkuki na vita ikawa kma imemalizwa na wanajeshi wake kwa hofu wakakimbia huku na kule na waliobaki wakamalizwa na waisraeli
Kumbukumbu la torati 3
1 Ndipo tukageuka, tukakwea njia ya Bashani; na Ogu, mfalme wa Bashani, akatutokea juu yetu, yeye na watu wake wote, kuja kupigana huko Edrei.
2 BWANA akaniambia, Usimwogope; kwa kuwa nimemtia mkononi mwako, yeye na watu wake wote na nchi yake; nawe utamtenda mfano wa ulivyomtenda Sihoni, mfalme wa Waamori, aliyekuwa akikaa Heshboni.
3 Basi BWANA, Mungu wetu, akamtia mikononi mwetu na Ogu mfalme wa Bashani, na watu wake wote; tukampiga, asisaziwe cho chote.
4 Tukatwaa miji yake yote wakati huo; hapakuwa na mji tusiotwaa kwao miji sitini, nchi yote ya Argobu, ndio ufalme wa Ogu ulio katika Bashani.
NB: Kwenye vitabu vya kiyahudi vinadai Mungu wao Israel yaani YHWH alishusha nzige/nyuki wakaula ule mlima kutokea katikati ndio ukagawanyika nusu ila najiuliza nyuki waule mlima ndani ya dakika??? Aseee!!!
Anyway hicho ndio kifo cha mfalme huyu aliyetikisa dunia kwa miaka yake na mpaka leo waisraeli wanatambua ushindi ule kma mkubwa kabisa kwenye historia ya taifa lao!! Hata amos na mfalme daudi huwa wanakikumbuka kisa hiko miaka zaidi ya 600 baadae!!!
Amos 2:9
9 Lakini nalimwangamiza Mwamori mbele yao, ambaye urefu wake ulikuwa kama urefu wa mierezi, tena alikuwa na nguvu kama mialoni; lakini naliyaangamiza matunda yake toka juu, na mizizi yake toka chini.
Zaburi 135:
10 Aliwapiga mataifa mengi,Akawaua wafalme wenye nguvu;
11 Sihoni, mfalme wa Waamori,Na Ogu, mfalme wa Bashani,Na falme zote za Kanaani
USHAHIDI WA KISAYANSI/KIHISTORIA
Rujm-El hiri or Circle of the rephaites
Hii inaelezwa ndio ilikuwa kasri au jumba la ibada la mfalme ogu na mpaka leo masalia yapo huko golan heights, syria (linakaliwa kimabavu na israel).... Mawe yaliyobaki kwa sasa ni zaidi ya 40,000 yamepangwa hadi futi 15 kwenda juu je kuna mtu wa miaka ile angeweza kupanga mawe mazito kwa urefu wa zaidi ya futi 50 kwa wakati huo kama hakua JITU la mfano wa OGU.
2. Karne ya 20 mwanzoni watafiti wa kijerumani waligundua makaburi makubwa ya mawe ambayo yanafanana na hesabu zilizopigwa kuhusu urefu wa mfalme ogu kwenye kitabu cha kumbukumbu la torati..... Kaburi hilo lilipatikana eneo la mto Jabbok, Bashan ambako ndipo mfalme ogu alifia. Na kwa hesabu zao kaburi hilo lina umri wa zaidi ya miaka 6000!!! Muda ambao ndio inasemekana og aliishi hapa duniani
3. Mfalme ogu pia alifanikiwa kuandika kitabu chenye sura 7 ambacho kilipatikana takriban miaka 1400 kabla ya kristo ila kilifichwa huko maktaba ya vatican kuaniza karne ya 5 ila baadae kilivujishwa je huu ni ushahidi mwingine kuwa JITU hili liliexist kweli na kuutesa ulimwengu!!!
Leave a Comment