HATIMAYE DIAMOND PLATNUMZ NA RAYVANNY 'WAACHIWA HURU'
Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewafungulia wasanii Diamond Platnumz na Rayvanny wote kutoka lebo ya Wasafi kufanya shughuli zao za muziki nchini baada ya kufungiwa kufanya shughuli za muziki nchini Tanzania kwa sababu za kimaadili. Pia BASATA walifungia show za Wasafi festival ambazo nazo zimefunguliwa rasmi kuanzia tarehe 22/01 mwaka huu (2019). Baada tuu ya 'kuachiwa huru' na Basata, wasanii Diamond na Rayvanny walionekana studio wakifanya wimbo mpya ingawa haijafahamika utatoka lini.
BASATA yawafungulia rasmi Wasanii kutoka kwenye lebo ya WASAFI pamoja na tamasha lao la "Wasafi Festival 2018".#SanaaNiKazi https://t.co/BZ6kGvv24w— Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) (@BasataTanzania) January 22, 2019
Leave a Comment