MWANAMUZIKI NGULI OLIVER MTUKUDZI AFARIKI DUNIA

Mwanamuziki mkongwe barani Afrika, Oliver Mtukudzi amefariki dunia. Mtukudzi ambaye alizaliwa mwaka 1952 amezaliwa nchini Zimbabwe na amekuwa akifanya muziki ambao ni mchanganyiko wa pop ijulikanayo kama "jit" kutoka nchini Zimbabwe na "Township pop" ya Afrika kusini. Nchini Tanzania Oliver Mtukudzi atakumbukwa zaidi kwa kufanya wimbo na mwanadada Lady Jaydee "Mimi ni Mimi" wakati nchini Afrika ya kusini amehusika katika movie ya Neria ambapo Mtukudzi alifanya soundtrack ya movie hiyo inayofahamika kwa jina la Neria. Taarifa kamili ya kifo chake itatolewa leo 24/01 na familia yake huku taratibu za mazishi zikifuatia. MUNGU ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, AMEN!!
Image result for animated download now gif

No comments

Powered by Blogger.